NAO WANIABUDU BURE!
Nawasalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu kristo, Na karibu tujifunze maarifa ya mbinguni. Siku tunazoishi ni siku za mwisho, Bwana alisema atakuja kama Mwivi! Sio kwamba anakusudia kuja namna hiyo ili kutukomoa kwamba tusiende mbinguni; bali ni kwa sababu watu wapo gizani, wamelala usingizi wa kiroho, hao ndio atawajilia kama mwivi. watakuwa hawajui majira ya kujiliwa kwao. watakuwa wametingwa na shughuli na masumbusu ya mali. watalewa na mali, watalewa na mvinyo, watakuwa walafi wa mambo ya dunia. 4 Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi. 1 Wathesalonike 5:4 Walio katika nuru wataitambua siku hiyo. Mwivi huja wakati mwenye nyumba amelala, na kama angekesha asingeibiwa. Ndio maana sisi wenyewe tukeshao; hapa haimaanishi mikesha, bali Kutokusinzia kiroho. Usilale kiroho usiku na mchana. Na Siku inayozungumziwa hapo ni siku ya Unyakuo wa kanisa . Lakini watu wengu kutokana na mafundisho ya wanadamu; hawajui jambo hili na wengine wamesikia na kuamini ku...