UMEMKATAA MUNGU KAMA WAISRAELI PASIPO KUJUA!

Neema ya kristo na iwe nanyi; karibu tujifunze hekima ya Mungu itupayo uzima wa milele.

Israeli baada ya kufika kaanani wakitokea misri, walikuwa chini ya waamuzi. Hawakuwa na mfalme bali Mungu ndiye alikuwa mfalme wao akiwatumia waamuzi. Lakini BWANA akijua utafika wakati waisraeli watataka mfalme kama jinsi yalivyo mataifa yasiyomcha Mungu yanavyofanya. Hivyo alimpa Musa maagizo kuwa watakapotaka mfalme waruhusiwe kumweka mfalme ambaye Bwana atamchagua (kumb 7:14-15). Ilifika wakati mmoja, Samweli kama mwamuzi wa wakati ule aliona amezeeka na hivyo akawateua wanawe wawaamue Israeli badala yake. Wanawe hawakwenda katika njia ya haki hata kuwafanya Wazee wa israeli wamwendee Samweli ili kumsihi awafanyie mfalme kama ilivyo kawaida ya mataifa mengine. (1samweli 8:4-5), jambo lile halikumpendeza Samweli. Lakini aliende kumsihi Mungu juu ya ombi lao na Mungu vile vile alighadhabishwa na shauri lile kutoka kwa wale wazee. Akasema; 1samweli 8 7Bwana akamwambia samweli, isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hawakukukataa wewe, BALI WAMENIKATAA MIMI, ILI NISIWE MFALME JUU YAO.

Bila shaka ni jambo la kushangaza, kwamba jambo hilo halikumpendeza Mungu, wakati aliwapa ruhusa miaka mingi iliyopita kwamba wakihitaji mfalme wapewe, na wao kwa kusoma maandiko waliona ni sawa, maana Mungu aliliruhusu. Pamoja na kuwa Mungu hakupendezwa na ombi lao la kutaka mfalme badala ya Mungu, bado Mungu aliwapatia huyo mfalme sawa na haja za mioyo yao(1samweli 8:22). Akawaambia sifa zake zitakavyokuja kuwa na kisha akamchagua Sauli awe mfalme wao. Kwa habari nzima unaweza kusoma 1samweli kuanzia sura ya 8 hadi 10. Sauli baada ya kusimikwa kuwa mfalme alianza kutawala kwa ushujaa lakini baadae kwa jinsi alivyokuwa wa kimwili alienda kinyume na maagizo ya Mungu na Mungu akamwadhibu kwa kumwondolea ufalme. Alimwagiza Sauli akawapige WAAMALEKI na kuangamiza kila kitu; yaani watu wote katika mji na mifugo yao yote, yaani asisaze chochote. Sauli aliwapiga kweli Waamaleki kwa mkono wa Bwana, lakini akasaza nyara; kondoo na ng’ombe walionona na kuja nazo Israeli. Kwa AKILI zake alijua ataupendeza moyo wa Mungu. kumbe ndio akaharibu kabisa na kukataliwa. (1samweli 15:12-23).
23Kwani kuasi ni kama Dhambi ya uchawi, na Ukaidi ni kama Ukafiri na Vinyago; kwa kuwa umelikataa NENO LA BWANA, Yeye Naye Amekukataa wewe usiwe Mfalme.
Unaweza ukajiuliza swali, Kwa nini Mungu alisema WAMENIKATAA MIMI, wakati aliwaruhusu toka huko nyuma?
Hilo lipo hata leo tunalitenda sisi nyakati hizi, maana lile lilikuwa kivuli cha hili la rohoni, ambalo ni baya zaidi kuliko lile.

*JAMBO HILO LILIKUWA LINAFUNUA NINI?*
Kama tunavyofahamu, agano la kale ni kivuli cha hili jipya; yaani kila kilichokuwa kinatendeka kule kimwili kinatendeka kiroho huku kwetu leo kwenye agano jipya hadi kwenye utawala wa miaka 1000 unaokuja hivi punde maana dunia ipo karibu kuharibiwa kwa hasira ya Bwana.
Mfano utaona yule pasaka yaani mwana kondoo alikuwa anamfunua Yesu, zile sikukuu za wayahudi pia, mahali pengine Paulo anasema mwamba waliounywea Israeli ulikuwa kristo, Pia Esta anamfunua bibi harusi na wale masuria wengine wakiwafunua madhehebu, Yusufu akimfunua kristo kukataliwa na watu wake na kupokelewa na mataifa kisha baadae akapatanishwa na watu wake. Mpinga kristo pia amechorwa na kazi zake zote atakazokuja kufanya wakati wa dhiki kuu. Na mifano mingine mingi maana Agano jipya lote limechorwa kimwili katika agano la kale.

Ndivyo hata wazee wa israeli kutaka mfalme mfano wa mataifa inafunua KUKATALIWA ROHO MTAKATIFU ambaye ndiye ROHO WA YESU yaani MUNGU MKUU katika agano jipya. Shika vizuri hapo, kwamba Mungu ni mmoja na Roho yake iliuvaa mwili kama jinsi tulivyo na kukaa pamoja nasi na huo mwili ukafanyika njia ya upatanisho kati yetu na Mungu.
2kor 5:19 yaani, MUNGU ALIKUWA NDANI YA KRISTO, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.
Kwa hiyo Roho ya Mungu ndio Roho ya Yesu na ndio Roho mtakatifu.
Tulianza nae katika mitume na akatenda kazi kwa miujiza na watu wakamtukuza Mungu, lakini baadae kama miaka 200 au zaidi, wazee wetu wakakaa pamoja wakakubaliana kuwa mawazo yao au namna wanavyoielewa Biblia wayaandike na ndio iwe msingi unaopaswa kufuatwa na kila mtu yaani THEOLOJIA. Wazee wakakaa katika baraza la NIKEA na kuanzia hapo ikawekwa misingi kwa jinsi ya kibinadamu kabisa na Mungu hakukataa, aliacha dhamira ya watu hawa itimie sawa na alivyowaruhusu wale wazee wa israeli; lakini mwisho wake ni kama mwisho wa mfalme SAULI.
Ilionekana ni jambo ambalo liliwapendeza watu na kuwapa uhakika fulani hata wakati wa vita. Hata leo ipo hivyo. Ni kweli Theolijia imesaidia wengi kumjua Mungu, maana hata wakati ule walitokea wafalme wazuri kama wakina Daudi, Hezekia, Asa, Yosia n.k. Lakini mfumo ule haukuwafaa kitu ndio maana mji ule uliteketezwa na israeli kupelekwa utumwani kwa kukoseshwa na wafalme wao. Mfano mmoja mtazame huyu mfalme alivyowakosesha Israeli wakati akitawala;
2wafalme 17:21 Maana aliwatenga mbali Israeli na nyumba ya Daudi; nao wakamfanya Yeroboamu mwana wa nebati kuwa mfalme; Yeroboamu AKAWAVUTA ISRAELI WASIMFUATE BWANA, AKAWAKOSESHA KOSA KUBWA.
Umeona jambo hilo? Kwa sababu ya moyo mkengeufu wa mfalme, aliwavuta na wengine wakafanya kama alivyofanya. Kumbuka hapa ni baada ya Israeli kutengana na kabila ya Yuda na huyu mfalme aliwazuia waisraeli wasiende kumwabudu Mungu Yerusalemu akihofia Yuda atawashawishi wawe kinyume na Yeroboamu, hivyo akachonga sanamu ili waibudu wakiwa israeli huko huko kana kwamba wanamwabudu Mungu. Kwa hiyo akaweka utaratibu na amri pia, ndio Bwana baadae aliwaambia watu,
Mika 6:16 Kwa maana AMRI ZA OMRI NDIO ZISHIKWAZO, na matendo yote ya nyumba ya Ahabu, NANYI MNAKWENDA KATIKA MASHAURI YAO; ili nikufanye kuwa ukiwa…..
Hata leo hii, kanisa limegeukia theolojia na halina mpango na Roho mtakatifu huku wakijidanganya ndiye, yaani wamechonga sanamu katika mawazo yao yatokanayo na theolojia. Hapa ndipo utakuta theolojia inachukua mfano mmoja wa Paulo akisema nanena maneno machache KWA AKILI ZAKE ili kuwafundisha wengine, theolojia imegeuza kuwa ndio kunena kwa lugha kulivyo(kutumia akili zako).
Sasa hivi mtu hahitaji tena kushukiwa na Roho mtakatifu anene kwa lugha bali wewe mwenyewe KWA MANENO YATOKAYO KWENYE AKILI ZAKO tu tayari umenena kwa lugha, ilimradi ni maneno yasiyojulikana maana yake, huko ndiko wanakosema kunena kwa lugha! Biblia inasema Kunena kwa lugha ni karama na si wote tunatanena kwa lugha, Kuna AMRI zingine kama kubatiza kwa jina la Baba na la Mwana na Roho mtakatifu badala ya kwa jina la Yesu kama jinsi Roho mtakatifu alivyowafunulia mitume andiko la Math 28:19, wakabatiza kwa jina Yesu. (Matendo 2:38, 10:46-48, 19:5 n.k),
lakini hadi leo madhehebu yanashika amri hiyo ya kubatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho mtakatifu ya theolojia.

Theolojia inasema Mungu ana nafsi tatu na amri hiyo mama(katoliki) na binti zake(madhehebu yote) wanashika hata sasa lakini Roho mtakatifu anasema
2kor 5:18 lakini vyote vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na NAFSI YAKE KWA KRISTO, naye alitupa huduma ya upatanisho; 19 yaani, MUNGU ALIKUWA NDANI YA KRISTO, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.
Nafsi ya Mungu(Roho mtakatifu), ni iliyokuwa katika mwili wa nyama kama jinsi tulivyo uitwao Yesu.
Tunda la Theolojia ni Mpinga kristo, ambaye Bwana alinena habari zake,
yoh 5 43Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo.
Na Mpinga kristo atakuja kwa kutumia cheo cha juu sana theolojia imewahi kuwa nacho, yaani upapa.

Matunda mengine ni watoto wake ambao ndio manabii na makristo wa uongo walio na roho hiyo ya mpinga kristo. Na roho ya mpinga kristo kuijua ni rahisi, ni pale inaposhindwa kukiri kuwa MUNGU ALIKUWA NDANI YA KRISTO.
1yohana 4:2 katika hili MWAMJUA ROHO WA MUNGU; kila roho ikiriyo kwamba YESU KRISTO AMEKUJA KATIKA MWILI YATOKANA NA MUNGU. 3 na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya Mpinga kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.

Umaweza kuwa na roho ya mpinga kristo pasipo kujijua.
Theolojia inakulazimisha uwe na dhehebu lakini Neno la Mungu linataka tuwe mamoja maana tupo chini ya kristo sote.
1kor 1 12Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, mimi ni wa Paulo, na, mimi ni wa Apolo, na, mimi ni wa Kefa, na, mimi ni wa Kristo. 13JE! KRISTO AMEGAWANYIKA? Je! paulo alisulubiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?
Maneno hayo yapo wazi kabisa, kwamba kanisa linapaswa kuwa mamoja, sio huyu anajiita mimi ni mkatoriki, mimi ni TAG, mimi FPCT, mimi EAGT, mimi wa ufufuo, mimi wa ELIYA, mimi wa efatha, mimi anglican, mimi mlutheri, mimi MSABATO! Je! Mlibatizwa kwa majina hayo? Ni mambo ambayo yanafanana kwa karibu sana na ile kweli, maana hata uongo ni ukweli uliogeuzwa.

Mambo haya yanaonekana yana Hekima sana kwa namna ya kimwili lakini mbele za Mungu ni UASI na UKAIDI.
Roho mtakatifu wa dhehebu leo ni THEOLOJIA, mitindo mingi makanisani ni kinyume na neno la Mungu, lakini mbele ya theolojia ni sawa. Theolojia hairuhusu mtu kuchunga kundi bila kuoa, theolojia hairuhusu mtu kubatiza wala kufungisha ndoa hadi awe na DIPLOMA ya theolojia husika. Jambo lile lile kuwa tunashika amri za OMRI(THEOLOJIA) badala ya Neno la Roho mtakatifu tuliyepewa atutie katika kweli yote.
Theolojia haina haja na utakatifu wala TOBA.
Ulimwengu leo umekuwa chunvi ya kanisa badala ya kanisa kuwa chunvi ya ulimwengu. Utakuta mwanamke anavaa surua, kunyoa kiduku/denge na dhehebu linaruhusu. Wasanii wa kidunia ndio mfano wa kuigwa kwa kanisa leo. Tena wana manabii na mitume wao wanaowatia nguvu mikono yao ya udhalimu wazidi kutenda uovu na machukizo hayo.
1YOHANA 4:5 HAO NI WA DUNIA; KWA HIYO WANENA YA DUNIA NA DUNIA HUWASIKIA.
Roho wa Yesu ananena waziwazi kuwa mwili wetu ni Hekalu la Mungu.
1kor3 16Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? 17Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.
LAKINI THEOLOJIA INASEMA MUNGU ANAANGALIA ROHO TU NA SIO MWILI, kwamba kupaka lipstick, kuvaa mavazi ya kuonyesha maungo, kusuka, kuweka kucha bandia, kuoshwa miguu isivyopaswa, kuvaa vimini n.k ni sawa, Haijalishi Mungu anasemaje maana wanatheolojia wameruhusu.
Kama jinsi sifa za wale wafalme zilivyokuwa na THEOLOJIA nayo. Kama vile Mungu alivyomkataa Sauli, vivyo hivyo na Theolojia.
Mat 15 8Watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila mioyo yao ipo mbali nami.
Leo karibu 90% ya wakristo ni wale wanaokiri kuwa ni wakristo kwa midomo lakini matendo yao yanamkana kristo. Hao ndio wale wanawali WAPUMBAVU wa mathayo 25. Maovu yapo ndani na nje ya kanisa, ndio maana Mungu ameagizia CORONA duniani kote kwa maana tumestahili.
Hosea 13 10“BASI, YUKO WAPI MFALME WAKO, APATE KUKUOKOA KATIKA MAJIJI YAKO YOTE, NA WAAMUZI WAKO, AMBAO ULISEMA HIVI KUWAHUSU, ‘NIPE MFALME NA WAKUU’? 11 NDIPO NILIKUPA MFALME KATIKA HASIRA YANGU, nami nitamwondolea mbali katika ghadhabu yangu.”
Swali kama hilo jiulize wewe unayeshika dhehebu maana kichwa chake ni theolojia na sio Roho wa kristo, iko wapi theolojia yako mwisho wa siku, itakayo kufanya kulijua Neno? Ama itakayokupa uwezo wa kuziacha dhambi zako na kukufanya kuwa Mwana wa Mungu? Badala yake imekufanya mwana wa mpinga kristo! Unafanya dhambi leo kisha unatubu kesho unairudia tena. Israeli iliishia utumwani kwenye mikono ya maadui na wakawa zomeo la mataifa. Na hata theolojia nayo mwisho wake upo karibu, na wengi itawapeleka kwenye DHIKI KUU.
wanatazamia nuru, na kumbe latokea giza(Isaya 59:9) na hii ndiyo itakuwa hatima ya wengi. Wengi wanajua watanyakuliwa siku ya UNYAKUO, Na wengine wanasema hamna unyakuo, maana maana theolojia yao ikikili hilo basi itabiki waokoke wote siku moja. lakini Biblia inasema, watashangaa kujikuta siku hiyo wameachwa na wanaenda kwenye dhiki kuu, wakati huo wengi walio katika udhehebu watajaribu kugonga mlango(kutubu) siku watakapojua wenzao wamenyakuliwa, Biblia inasema; watatamani kuingi lakini wasiweze.

TUBUNI SASA, Yesu anarudi hivi karibuni kulinyakua kanisa yaani Bibi harusi (wanawali wenye busara), walio na mafuta (Roho mtakatifu). MKIONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU MTAJUA HAYA NIWAAMBIYO NI NENO LA MUNGU NA SI USHUPAVU WA KIDINI.

MAWASILIANO.
Ikiwa utapenda uwe unapata mafundisho ya mara kwa mara ya Neno la Mungu katika simu au utahitaji UBATIZO au Muongozo baada kumpokea Kristo ndani ya maisha yako.
Basi wasiliana nasi kwa njia zifuatazo
Kupiga simu: +255755251999
Whatsapp : +255789001312

Kanisani: Tegeta-Kibaoni
Karibu na kituo cha daladala cha Nyuki.
Pia kama utawiwa kumtolea Mungu, tunauhitaji wa ku-print vipeperushi ili sauti ya injili ya kuja kwa Bwana mara pili ifike mbali na kwa haraka, basi tuma mchango wako namba hii 0755-251-999.
Mungu akubariki!

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NAO WANIABUDU BURE!

NIMEWAPELEKEA TAUNI KAMA YA MISRI (CORONA) LAKINI HAMKUNIRUDIA MIMI

JE! NAWEZA KUWA SAFI NAMI NINA MIZANI YA UDHALIMU!!