WANA JUHUDI YA KUMTAFTA MUNGU LAKINI SI KATIKA MAARIFA!

Nawasalimu katika jina la mwokozi wetu. Karibu tujifunze maarifa ya mbinguni ambayo wengi huangamia kwa kuyakosa.

Mimi ni mwanafunzi wa Yesu, nami nakushudia katika habari hizi za ufalme wa mbinguni kuwa ni njema na hupaswi kuzikosa. Maana uangamivu wa dunia upo karibu.

Siku hizi za mwisho kuna mambo mengi yalitabiliwa kutukia, mojawapo ni kuwa watu wa kujipenda wenyewe, Upendo kupoa(upendo wa kumpenda Mungu)
Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,
2 Timotheo 3:2
Haya yote yanatukia kila kukicha na ni dhahiri mbele za macho yetu, hatuhitaji kusimuliwa. Baada ya kuingia injili ya manabii wa uongo, hayo mambo yaliyotajwa yakapata nafasi kanisani/hekaluni. Kuna jambo hapa nataka ulipate/ulielewe, kwamba Hekalu la Mungu linapaswa kuwa takatifu na Hekalu ni kuanzia mwili wako.
16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
1 Wakorintho 3:16

17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.
1 Wakorintho 3:17

Ipo dhana siku hizi za mwisho kuwa Mungu haangalii mwili bali Roho! Kwa kiasi fulani ni kweli lakini maana yao wanaotumia hiyo fasili siyo ile inakusudiwa juu ya maneno hayo. Ni kweli Mungu hana haja na mwili wako, maana hata tukifa tutavaa mwili mpya, lakini ule mwili mpya tunaouvaa ni kama huu ila ule ni wa mbinguni yaani usioharibika(hekalu jipya)! Ina maana kuwa Roho hii tuliyonayo ndio hiyo hiyo tutakuwa nayo ila mwili tofauti. Kanisa linaanza kwa mtu mmoja, tukiwa wengi tunakawaida ya kutafta mahali pa kukutania kwa ajili ya kubwabudu Mungu. Hivyo mwili wako ni hekalu. Kusema Mungu haangalii mwili ni makosa, imewafanya watu wengi kutenda dhambi makusudi wakitumaini Mungu haangalii mwili. Mungu amesema atamharibu mtu huyo anayeuharibu mwili wake.

Lazima tuelewe kuwa najisi inatoka ndani, mawazo mabaya ni najisi hiyo! Mwili hauna amri juu yake bali huishawishi Roho itende jinsi mwili utakavyo. Kwa hiyo mwili hauwezi kujivika mavazi ya kikahaba wala kujichubua kama Wazo hilo halikutoka ndani ya ile Roho iliyo ndani. Kwa hiyo ndani yako ambamo kuna chemichemi ya uhai ndimo hutoka hizo fikra potofu kulingana na roho/moyo wa huyo mtu alichoujaza. Hapo ndipo inakuja tofauti ya mtu mwenye maarifa na asiye na maarifa
Ukiwa umejaza maarifa ya Mungu, picha ya maarifa ya ndani inaanzia nje.

Leo ukiambiwa acha mavazi wa kikahaba(nguo za kubana na kuchora umbile, Vimini, kufuga kucha na kuweka kucha bandia, kupaka wanja, kunyoa kiduku, wanawake kuvaa suruali na kaptura, kupaka rangi kucha, kuoshwa miguu na wanaume, kupaka rangi nywele, fashion, n.k.) unasema usihukimu, wewe hubili tu injili, hayo mengine Mungu ndio anajua! Wengi wamewafanya hata wahubili wakageuka na kufuata mapenzi ya waumini kwa kuangalia mifuko yao maana injili yao ni tumbo.

Utabiri wa mambo haya ulitolewa miaka mingi iliyopita, Mungu kupitia mtumishi wake Isaya mwana wa Amozi alisema;
10 wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo;
Isaya 30:10
Maneno laini ndio hayo utabarikiwa/utakuwa tajiri tena kwa mifano ya watu wa mataifa kama wakina Bilgate, sanders, Obama n.k, utamiliki uchumi mkubwa kana kwamba ni moja ya vigezo vya kwenda mbinguni wakati ni kitanzi cha kuuona ufalme wa mbinguni. Yote haya yameleta usingizi wa kiroho; watu wakazidi kuupenda na kuutumaini ulimwengu kuliko Mungu.
Hapa ndipo tunakuta wanawake wengi wenye utauwa lakini wakikana nguvu za Mungu wamejaa kwenye masinagogi ya manabii wa uongo; maana huko hamna injili ya toba bali maneno laini na maneno yadanganyayo ndio mahubili ya kila siku. Na wengine walio na moyo wa kumtafta Mungu nao wanafungiwa nira ngumu huko wasikue na kuufikia utimilifu wa imani ya kweli, wamedumaa kimo maana kila siku ni kunywa maziwa, na kutumainishwa kwa maneno ya mwanadamu. Wanawafungia mizigo mikubwa kuliko hata ya kwao, Yaani upofu uliowakumba ni mkuu, shetani anajizolea makundi makundi maana hawana maarifa. Ni kweli wapo kanisani kuutafta uso wa Mungu lakini si katika maarifa. warumi 10:2

Upofu ule ule kama uliowapata israeli, Juhudi zile zile bila maarifa. Mungu anasema usiupende ulimwengu lakini mtu anashindwa kutofautisha Ya ulimwengu ni yapi na Ya mbinguni ni yapi! U nadhani Neema iliondoka israeli kwa sababu alitupenda kuliko wao? Hapana, hata sisi tunaelekea pale pale, yaani Neema kuondoka kwetu na kurudi israeli kwa sababu ya mioyo ya jiwe tuliyonayo. Tumebaki kumwita Mungu kiunafiki, tunachukua uzinzi wetu na uasherati(wa kiroho) na kwenda mbele za Mungu kuuliza shauri kwake! Nje kahaba na uso wake umeandikwa Mzinzi halafu tunaenda mbele za Mungu kuomba rehema!!!
1 Ndipo baadhi ya wazee wa Israeli wakanijia, wakaketi mbele yangu.
Ezekieli 14:1
2 Ndipo neno la Bwana likanijia, kusema,
Ezekieli 14:2
3 Mwanadamu, watu hawa wametwaa vinyago vyao na kuvitia mioyoni mwao, nao wameweka kwazo la uovu wao mbele ya nyuso zao. Je! Ni laiki yangu niulizwe na wao katika neno lo lote?
Ezekieli 14:3
Hivyo vinyaho ndio hayo mavazi, fasheni na mitindo ya dunia hii ya leo.

Mungu hazihakiwi; Chagueni leo kati ya mawazo mawili, kati ya Mungu na shetani. Fanyeni maamuzi ili msishindane na Mungu! Amueni kumwabudu shetani ama Mungu! Tazama mmejaa chuki na matukano, Mtu yupo radhi kukanya mafuta, kunywa mafuta, kumbeba mchungaji mgongoni, kumsujudia mchungaji/nabii(wa uongo) ila sio kusikia injili hii. Atanyenyekea kwao kwa juhudi ila Kwa injili kama hii anarusha matusi! Biblia imesema lazima mtafanana nao hao manabii. Yaani mbuzi hawezi kuzaa kondoo; Huwezi kuwa kondoo wakati Baba yako ni Mbuzi, kwa sababu wao wamevaa ngozi lakini ndani ni mbwa mwitu; ndivyo mlivyo hata ninyi!

Tokeni kwenye madhehebu yao, maana mmerishwa maarifa ya yule ibilisi

8 Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami.
Mathayo 15:8

9 Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.
Mathayo 15:9

Wapendwa bado Neema tunayo kwa kitambo kidogo sana, Biblia ipo wazi kuwa tupo karibu na unyakuo, Ikimaanisha usipokidhi vigezo vya kunyakuliwa utaingia kwenye dhiki kuu. Kumbuka hakuna kinyonge kitaingia mbinguni. Kama maarifa yako yanaishia mlangoni, utaishia mlanhoni, kama wale wanawali 5 wapumbavu. lakini maadamu tumaini bado lipo tubu leo na kuacha kumzoelea Mungu, acha mavazi ya kahaba, Acha fasheni, acha unafiki, acha kwenda kwa manabii, Roho mtakatifu atosha na ndiye pekee tuliachiwa kama msaidizi hakuna mwingine.

shalom!

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NAO WANIABUDU BURE!

NIMEWAPELEKEA TAUNI KAMA YA MISRI (CORONA) LAKINI HAMKUNIRUDIA MIMI

JE! NAWEZA KUWA SAFI NAMI NINA MIZANI YA UDHALIMU!!