NA TUMFANYE MTU KWA MFANO WETU!.
Hujambo? karibu tujifunze maarifa ya mbinguni.
Kanisa limepita katika nyakati mbalimbali, tumeanza na nyakati za EFESO yaani wakati wa injili ya mitume, huko kote hutaona wanataja Mungu kuwa ni utatu wala ana nafisi tatu mpaka baada ya madhehebu kuanza. Pale ambako kughoshi injili kulipoanza na nafsi tatu zikaanza. Biblia inasema baadhi ya maandiko yalifungwa yasijulikane katika ufahamu wa mwanadamu hadi wakati wa mwisho ambao ni nyakati za LAODIKIA. Nyakati hizi zilianza miaka ya 1900 na zitakoma baada ya unyakuo tu. Kwa hiyo siri hizi zinakuwa zinafunuliwa nyakati hizi, madhehebu hayakubaliani na ufunuo huo maana yametoka rohoni na kuingia mwilini na kukalili mapokeo. Madhehebu yanafuata zaidi theolojia inasema nini na sio Mungu anasema nini! Kama tungefuata Mungu anasema nini hakuma mtu angejiita M-KATOLIKI, M-TAG, M-FPCT, M-EAGT, M-ANGLICAN N.K. Sawa na 1kor 1:12-13, 1kor 3:4.
Mgawanyiko huu umetufanya kulikaribisha giza kwa sehemu maana tunaamini tu theolojia yetu inasemaje na sio Neno la Mungu linasemaje, na kwa sababu theolojia ni tafsiri ya maandiko kwa kutumia akili za mwandamu hivyo ni vigumu mtu kugundua makosa yako wapi.
Inabaki tu kuwa kama umezaliwa chini ya theolojia fulani unakuwa kama hiyo theolojia tu, huwezi kuwa kitu kingine; maana mpapai utazamaa papai, mtango utazaa tango, mwembe utazaa embe.
Sasa ili ujue makosa yako wapi rudi kwenye Biblia(Neno la Mungu) kwa usaidizi wa Roho mtakatifu ndio utajua.
Maana mitume kumi na mbili ukiongeza na Paulo wakiwa chini ya Roho mtakatifu injili yao ni moja.
Hakuna mtu leo anaweza kusema sisi ni wa Petro ama Paulo maana hakuna utofauti wa injili zao. Yapo mambo mengi leo yanayotufanya tutofautinae kwa jinsi theolojia zetu zinalalia wapi na Neno la Mungu linasemaje. Sitasema zote ila nataka leo tuangalie tofauti moja ambayo imeanzia kwa kahaba mkuu(katoliki) na kuingia kwa binti zake(madhehebu yaliyosalia).
Wote husema Mungu ni nafsi tatu yaani kuna nafsi ya Baba na nafsi ya mwana na nafsi ya Roho mtakatifu.
Lakini jiulize swali, hapo alikuwa anaongea Mungu yupi, Baba, Mwana, au Roho mtakatifu? Bila shaka utasema Baba maana yeyote mwenye mawazo ya utatu lazima amwone Mungu Baba ni mkubwa kuliko wale wengine wawili.
Mara nyingi Mungu alikuwa anatumia neno “sisi” kama wingi kuashiria kuwa hakufanya mambo yote peke yake, bali alikuwa na wengine aliowashirikisha mawazo yake,lakini Uumbaji alifanya peke yake.
hebu tazama mstari huu unaofuata,
Kumbuka kuumba aliumba yeye peke yake lakini mawazo yake ya kufanya baadhi ya mambo aliwashirikisha wengine, hivyo hapo aliposema na tumfanye mtu kwa mfano wetu alikuwa anaongea na malaika zake, na hakuwa anazungumza na nafsi ya tatu katika uungu wake,kama wengi tunavyodhani.
Mungu ni mmoja tu na hana nafsi tatu, neno “TUMFANYE” halimaanishi ni watatu tu! bali linaweza likamaanisha wawili, au watano, au mia au milioni n.k.
Sasa tutazame ufunuo huu ambao mitume waliupata na baadae dhehebu/theolojia ikageuza.
Petro na mitume wengine wanatuambia kwa roho kuwa jina la Baba na la Mwana na la Roho mtakatifu ni YESU KRISTO. Kubatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la roho mtakatifu ni utoto wa kiroho(uchanga), hakuna Baba asiyekuwa na jina, hakuna Mwana asiyekuwa na jina, ila wakati ukiwa mtoto ulikuwa unajua jina la Baba yako ni Baba, lakini leo unamwita Baba kama cheo chake kwako ila unalifahamu jina lake kuwa ni Petro ama Magufuli ama Charles. Lakini haya yote yalifanywa na dhehebu na wadhehebu(theolojia), Si watoto wa Mungu. Sasa dhehebu lenyewe linasema hapana, haiwezekani; mitume walifanya hivyo kum-promote Yesu, hawakujua theolojia wale ndio maana. sisi tunao ujuzi kuliko wao, tunao watu mashuhuri wa maandiko kuliko wao.
Itazame nafsi moja ya Mungu kwenye Maandiko.
Baadae Mungu akatamka Neno lake kuwa iwe nuru ikawa nuru, iwe hivi ikawa ndivyo, Mwanzo 1.
Baadae Yule Neno(wazo la Mungu) akauvaa mwili;
Na ule mwili akauita jina lake Yesu, ule mwili unao mwanzo maana una miaka 2021 mpaka sasa, lakini ile roho ndani yake(Roho takatifu au Roho mtakatifu) ni Mungu mwenyewe. Akaja duniani na kuwa ni mwana wa Mungu ili wale wana wa ufalme(israeli) walioiacha njia yake wasikie lakini wasielewe na ndivyo ilivyokuwa.
Walipovushwa macho ili mataifa ambao ni sisi tupokee nasi ile neema kama wao walivyoipokea wakiwa misri na halafu nasi tumewekewa nyakati saba za kutembea kwenye ile neema, hivi sasa tupo ukingoni.
Musa anajua Mungu ni mmoja na kashawahi kukutana nae, israeli wanajua Mungu ni mmoja ndio maana hata leo wanasubili ufunuo huu ili watubu na kulia na kuomboleza kuwa walimsulubisha mwokozi wao, aliyewatoa misri nakuwapa mana jangwani. ufunuo 7:1-8. Mitume wanajua Mungu ni mmoja aliyekuja duniani kwa njia ya kristo.
DHEHEBU PEKE YAKE NDIO LINATAMBUA UTATU, jambo ambalo halipo kwenye maandiko isipokuwa kwenye vitabu vya theolojia.
Yesu mwenyewe anasema torati na manabii waliandika habari zake, soma..
Agano la jipya lote linazungumzia kristo, Mungu mkuu; Mungu wa pili na wa tatu wapo agano lipi? Hamna kitabu kingine kinachowaonesha Mungu wa pili na wa tatu zaidi ya theolojia(roho mtakatifu wa madhehebu).
Si kwamba theolojia ni dhambi, bali theolojia ndio iliyowafanya wengi kugeukia injili ya namna nyingine, watu wenye elimu hii leo tumeifanya nyumba ya Mungu kuwa Empire(ngome) yatu, yaani tunajiona sisi ndio watawala mahali pale wala hatuwaachi wengine karama zao zikue. Masadukayo na mafarisayo yamerudi tena ila kwa namna tofauti kidogo ili kuwapofusha macho waliokalili yale majina(sadukayo na farisayo).
Dhehebu halitatubu(Biblia inasema hivyo), katoliki hatatubu na kuacha uasherati wake, wala binti zake hawatasema tutubu na kuacha uasherati wa mama yetu katoliki, bali kila mmoja atazaidi kujihesabia haki kuwa yeye yupo sawa kuliko mwingine. Anayetubu ni mtu mmoja mmoja, madhehebu sehemu yake ni dhiki kuu, ndipo hapo wengi watakaposhituka na kusema tulipofushwa macho namna gani hata siku ya kujiliwa kwetu ikatupita? Mungu wetu ni mmoja na jina lake moja na nafsi yake moja. Shalom!

Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchiUkiwa tayari umeshamgawanya Mungu kuwa watatu, andiko hilo litakupa kuamini mtazamo wako upo sawa.
Lakini jiulize swali, hapo alikuwa anaongea Mungu yupi, Baba, Mwana, au Roho mtakatifu? Bila shaka utasema Baba maana yeyote mwenye mawazo ya utatu lazima amwone Mungu Baba ni mkubwa kuliko wale wengine wawili.
Mara nyingi Mungu alikuwa anatumia neno “sisi” kama wingi kuashiria kuwa hakufanya mambo yote peke yake, bali alikuwa na wengine aliowashirikisha mawazo yake,lakini Uumbaji alifanya peke yake.
hebu tazama mstari huu unaofuata,
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.Je, hiyo aya inaleta maana gani kwako? Hiyo ina maana kuwa jambo la kutaka kuumba aliwashirikisha hadi malaika, lakini kwenye uumbaji akafanya peke yake.
Kumbuka kuumba aliumba yeye peke yake lakini mawazo yake ya kufanya baadhi ya mambo aliwashirikisha wengine, hivyo hapo aliposema na tumfanye mtu kwa mfano wetu alikuwa anaongea na malaika zake, na hakuwa anazungumza na nafsi ya tatu katika uungu wake,kama wengi tunavyodhani.
Mungu ni mmoja tu na hana nafsi tatu, neno “TUMFANYE” halimaanishi ni watatu tu! bali linaweza likamaanisha wawili, au watano, au mia au milioni n.k.
Sasa tutazame ufunuo huu ambao mitume waliupata na baadae dhehebu/theolojia ikageuza.
mathayo28:19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;Huo hapo utatu kwa jicho la kimwili; lakini kwa jicho la kiroho tuwatazame hao wanafunzi maana wakati Yesu anaongea hayo maneno alikuwa pamoja nao.
matendo 2:37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.Tazama pia matendo 10:46-48, 19:5, 8:16, warumi 6:3
Petro na mitume wengine wanatuambia kwa roho kuwa jina la Baba na la Mwana na la Roho mtakatifu ni YESU KRISTO. Kubatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la roho mtakatifu ni utoto wa kiroho(uchanga), hakuna Baba asiyekuwa na jina, hakuna Mwana asiyekuwa na jina, ila wakati ukiwa mtoto ulikuwa unajua jina la Baba yako ni Baba, lakini leo unamwita Baba kama cheo chake kwako ila unalifahamu jina lake kuwa ni Petro ama Magufuli ama Charles. Lakini haya yote yalifanywa na dhehebu na wadhehebu(theolojia), Si watoto wa Mungu. Sasa dhehebu lenyewe linasema hapana, haiwezekani; mitume walifanya hivyo kum-promote Yesu, hawakujua theolojia wale ndio maana. sisi tunao ujuzi kuliko wao, tunao watu mashuhuri wa maandiko kuliko wao.
Itazame nafsi moja ya Mungu kwenye Maandiko.
yohana 1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. 3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. 4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. 5 Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza...Tazama sasa Mungu alivyo; mstari wa kwanza; Hapo mwanzo alikuwapo Mungu na ndani ya Mungu kulikuwa na Neno(wazo la Mungu) kumbuka hapo kaanza kusema HAPO MWANZO kulikuwako Neno kana kwamba kulikuwa kwanza na mwanzo halafu Mungu; mstari wa pili ndio unaeleza mwanzo na Mungu nani alianza.
Baadae Mungu akatamka Neno lake kuwa iwe nuru ikawa nuru, iwe hivi ikawa ndivyo, Mwanzo 1.
Baadae Yule Neno(wazo la Mungu) akauvaa mwili;
yohana 14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.Hapo Mungu aliamua kuacha mamlaka yake mbinguni na kujitwalia mwili wa kibinadamu kabisa, ila roho ni ya Mungu, utashi ni wa Mungu isipokuwa tu ule mwili ndio wa kibinadamu.
Na ule mwili akauita jina lake Yesu, ule mwili unao mwanzo maana una miaka 2021 mpaka sasa, lakini ile roho ndani yake(Roho takatifu au Roho mtakatifu) ni Mungu mwenyewe. Akaja duniani na kuwa ni mwana wa Mungu ili wale wana wa ufalme(israeli) walioiacha njia yake wasikie lakini wasielewe na ndivyo ilivyokuwa.
Walipovushwa macho ili mataifa ambao ni sisi tupokee nasi ile neema kama wao walivyoipokea wakiwa misri na halafu nasi tumewekewa nyakati saba za kutembea kwenye ile neema, hivi sasa tupo ukingoni.
Musa anajua Mungu ni mmoja na kashawahi kukutana nae, israeli wanajua Mungu ni mmoja ndio maana hata leo wanasubili ufunuo huu ili watubu na kulia na kuomboleza kuwa walimsulubisha mwokozi wao, aliyewatoa misri nakuwapa mana jangwani. ufunuo 7:1-8. Mitume wanajua Mungu ni mmoja aliyekuja duniani kwa njia ya kristo.
DHEHEBU PEKE YAKE NDIO LINATAMBUA UTATU, jambo ambalo halipo kwenye maandiko isipokuwa kwenye vitabu vya theolojia.
Yesu mwenyewe anasema torati na manabii waliandika habari zake, soma..
luka 21 Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipotendeka mambo hayo; 22 tena, wanawake kadha wa kadha wa kwetu walitushitusha, waliokwenda kaburini asubuhi na mapema, 23 wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosema kwamba yu hai. 24 Na wengine waliokuwa pamoja nasi walikwenda kaburini wakaona vivyo hivyo kama wale wanawake walivyosema, ila yeye hawakumwona. 25 Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! 26 Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? 27 Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.Ukiachilia mbali habari za vita na ukombozi, torati na manabii(agano la kale) vinazungumzia kristo.
Agano la jipya lote linazungumzia kristo, Mungu mkuu; Mungu wa pili na wa tatu wapo agano lipi? Hamna kitabu kingine kinachowaonesha Mungu wa pili na wa tatu zaidi ya theolojia(roho mtakatifu wa madhehebu).
Si kwamba theolojia ni dhambi, bali theolojia ndio iliyowafanya wengi kugeukia injili ya namna nyingine, watu wenye elimu hii leo tumeifanya nyumba ya Mungu kuwa Empire(ngome) yatu, yaani tunajiona sisi ndio watawala mahali pale wala hatuwaachi wengine karama zao zikue. Masadukayo na mafarisayo yamerudi tena ila kwa namna tofauti kidogo ili kuwapofusha macho waliokalili yale majina(sadukayo na farisayo).
Dhehebu halitatubu(Biblia inasema hivyo), katoliki hatatubu na kuacha uasherati wake, wala binti zake hawatasema tutubu na kuacha uasherati wa mama yetu katoliki, bali kila mmoja atazaidi kujihesabia haki kuwa yeye yupo sawa kuliko mwingine. Anayetubu ni mtu mmoja mmoja, madhehebu sehemu yake ni dhiki kuu, ndipo hapo wengi watakaposhituka na kusema tulipofushwa macho namna gani hata siku ya kujiliwa kwetu ikatupita? Mungu wetu ni mmoja na jina lake moja na nafsi yake moja. Shalom!
Maoni
Chapisha Maoni
Tafadhali, share kwa wengine ili kuisambaza injili kwa watu wote na Mungu wa mbinguni atakubariki.
Unaweza kutumia namba hii 0755251999 kuwasiliana kwa njia ya whatsapp