TOFAUTI KATI YA PETRO NA PAPA

Jina la Bwana litukuzwe.
Mpendwa nakusalimu kwa jina la Yesu kristo Bwana wetu. Karibu tuongeze maarifa ili sote tuwe tayari kupokelewa katika Ufalme wa Mbinguni.

Wengi huwa hatuelewi kama Madhehebu tuliojifungamanisha nayo tayari tumetengeneza dhambi ya udhehebu. Mara nyingi sana Watu leo hawana haja na Injili ya Toba bali ile nyingine isiyokuwepo katika Maandiko, ila tamaa ya mwanadamu ameileta kwa kufungua mianya;
Mwingine kwa ajili ya ukuu
Mwingine kwa ajili ya mali
Mwingine kwa ajili ya umaarufu n.k.

Hayo tuyaache, leo tuongelee hasa Madai ta Dhehebu la Katoliki ambalo hasa hudai ndio kanisa la Mitume. Sitakupa hisyoria nzima ila nitakupa UTOFAUTI KATI YA MTUME PETRO NA PAPA

Mara nyingi tumekuwa tukihubili juu ya Mpinga kristo kama ndiye Papa wa katoliki.
3 Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;
2 Wathesalonike 2:3

4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.
2 Wathesalonike 2:4

Hili andiko linafunua mpinga kristo kuwa ni mkristo kutokana pia Na ufunuo wa Yule KAHABA MKUU ama Mama wa makahaba(Dhehebu la romani katoliki) wa ufunuo 17
Unaweza pia kumsoma huyu mpinga kristo katika Danieli 9:26-27.

Sasa madai ya katoliki kukataa ukweli huu ni Mengi lakini Kumbuka Dhehebu lote halitatubu hadi mwisho. Bali mtu binafsi ndio anaweza kutubu. Na biblia inasema tokeni kwake Enyi watu wangu.

Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.
Ufunuo wa Yohana 18:4
Unaweza kuona kuwa Huyu mpinga kristo(PAPA) na dhehebu lake Atabadili majira yaani kutoka majira Ya Neema kwenda Majira ya Dhiki kuu. Ni yeye ndiye atayefanya hivyo na Mapigo ya Ufunuo 16 yatatimizwa katika ghadhabu kali ya Bwana.

Sasa kabla ya wakati huo Mungu ametufunulia katika majira haya kabla ya ile dhiki kuu na Kazi iliyobaki kwetu ni kuihubili injili sawa na Ufunuo ule.
Si kwa kuanzisha Dhehebu bali kwa Injili isiyogoshiwa.
Si kwa mapenzi ya mwanadamu ya kutaka utajiri, mafanikio bali TOBA.

Hamna andiko lolote likionesha Petro alikuwa Papa wala cheo hiki hakikuwepo mpaka Petro anakufa. Andiko linalofanya mkanganyiko ni hili;
16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.
Mathayo 16:16

17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
Mathayo 16:17

18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Mathayo 16:18
Utafasiliji wake ndio umefanya tofauti kubwa.
Kama ukitumia damu na nyama kutafsiri hilo andiko utatoka na majibu mengi jinsi ya ufahamu wako. Lakini katika Roho ipo tafsiri moja tu, nayo ni ufunuo kutoka kwa kristo ndio mwamba.

MADAI YA KANISA KATOLIKI

Katika damu na mwili (akili ya mwanadamu) ni rahisi tu akasema Ule mwamba aliousema hapo Ndiye Petro. Na kanisa alilolisema ndio hilo la waromani katoliki. Hii haina tofauti kubwa na yule anayeshika SABATO. Jambo ni lile lile; Mwenye kushika Sabato Anashika siku na kuutaabisha mwwili wala si Sabato kama ilivyokuwa katika Torati ambayo ilikaa kama kivuli cha lile agano la kweli la Rohoni(NEEMA).Ukisoma Warumi 7 utaona jinsi tulivyolivua agano la kale kwa maana matendo ya sheria ambayo katika ile sheria; Dhambi ilipata nguvu kwa kuwepo kwake ile sheria na mauti ikanena kwa nguvu ya ile dhambi. Si kwamba sabato imefutwa, hapana! Bali katika kuishika si kwa jinsi mwili.

Huyu wa kanisa naye ndivyo alivyo kama wa Sabato. Kanisa liloongelewa si jengo ama usitaarabu wenu bali La Rohoni. Kila aliye wa Rohoni amefanyika mjori katika kanisa. Jengo ni mahali Mwili unapaswa kumtumikia Mungu katika ushirika wa kindugu katika kristo na kuyanena mapenzi yake ili kila mtu aenende Katika Roho na kweli.
Sasa hapo huwezi kuona Tabaka ikiwa tu Mtakaa katika Uongozi wa Roho mtakatifu maana wote mmezaliwa katika Roho yule yule.
Jengo halibadiliki lakini Ustaarabu wa kanisa ndio unaweza kubadilika. Ustaarabu ni jumla ya mambo yote katika ibada. Tumeambiwa na tumehakikidhiwa kuwa lipo neno liligoshiwa na mwanadamu kwa werevu na akili nyingi ambalo si kutoka kwa Mungu na lipo lililosahihi. Kanisa la katoliki limegoshi maandiko tena kwa uerevu sana.

Ila sasa mpaka watu wanajitenga ni Kusema, Unajitenge na Uovu ili Bwana usimchukize kwa Sababu ya Makosa ya Nduguyo. Dhambi tunaikimbia sio kuilea👇
Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.
1 Wakorintho 10:14
Sasa kanisa la Mwanzo ambalo ni katoliki lilianzisha Ibada za Uongo na za sanamu.
Ndipo kukatokea kuondoka baadhi ya walioipenda kweli.

Kuhubili kwetu kusiwaudhi ndugu wakatoliki maana kama dhambi ipo tukinyamaza huku tukijua upo uovu, basi Mungu hatakuwa radhi na sisi. Ni kweli lazima tukemee kama Paulo anavyosistiza.
15 Nena maneno hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote.
Tito 2:15
Lakini yoye ni kwa kujengana na kwa upendo, Unajua Yesu akijua watu wake watamkataa, bado alikuja. Na baadhi yao walimkubali. Nasi kwa kujua mtakataa injili tunayowaletea, bado tunaileta maadamu wapo watakaokubali. Kama mafarisayo ama masadukayo mmojawapo angekubali injili ya Yesu na kutubu dhehebu zima; hata leo ningekuwa na uhakika kuwa siku moja katoliki atatubu. Lakini badala yake hatatubu bali baadhi tu katika watu wake.

Tofauti kubwa kati ya Petro na Papa

Nafanya hivi tujue kama kweli mwanzilishi ni Petro. Na kama kweli lazima sifa zao zifanane.
》1. Petro katika nyaraka zake hakumtaja Maria kama Muombezi. Na wala injili yake haimweki mtu awaye yote katika nafasi ya mwana wa Mungu.Bali kristo anamtaja kuwa ndiye mwokozi pekee. Soma nyaraka zake mbili zote, hutaona huo unikolai(upagani) ndani yake.

》2. Petro alibatiza kwa jina la Yesu akijua ufunuo wa mathayo 28:19 kuwa jina la Baba na la Mwana na Roho mtakatifu ni YESU Angalia ubatizo aliofanya Petro; matendo 2:38, 10:46-48, 8:16.
•Papa anaedai Petro ndie Papa wa kwanza anabatiza kwa jina la Baba na Mwana na la Roho mtakatifu.

》3. Petro hakubatiza watoto; tazama biblia nzima hutaona.
Matendo 2:38 anasema TUBUNI NA MKABATIZWE...
Mtoto mdogo anaweza kutubu?? watoto wadogo hubarikiwa. mtoto kabla hajajua mabaya na mema hahukumiwi mabaya yoyote. Kwa hiyo Paulo alibatiza watu wenye ufahamu wanaoweza kutambua baya na jema.

》4. Petro alikataa dhambi na kukemea sana. Mfano;
3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;
1 Petro 4:3
Soma pia 2petro 2:10-22.
•Papa yeye anakwambia kufanya hivyo atawahukumu watu. Kwa hiyo akaamua kufungisha ndoa za jinsia moja yaani USHOGA NA USAGAJI NI RUKSA kanisani! Kiufupi hamna dhambi tena kwa maana hiyo.

》5.Hakuna mtu aliyewahi kutubu dhambi kwa Petro. Petro alionya juu ya fasiri za upotoshaji wa Maandiko katika nyaraka za Paulo na maandiko mengine kwa watu wasio imara. 2petro 3:16.
•Papa anasema anaruhusiwa kusamehe dhambi, akitumia andiko yohana 20:23.
Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.
Yohana 20:23
Maana ya andiko hilo si mtu kutubu kwako, hapana! Bali ni ile mamlaka ya kuwambia umesamehewa dhambi zako kwa jina la Yesu Maana Maandiko yanasema;
17 Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.
Wakolosai 3:17
Ila si kwa mtu kueleza dhambi zake mbele zako, Hapana! Wewe ni nani hapa usikilize dhambi za wengine?? ilihari wewe mwenyewe unatenda hayo hayo?
7 Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?
Marko 2:7

》6. Petro alijitambulisha mtumwa na mtume! Au mzee; Hajawahi kusema yeye ni Baba mtakatifu wala Papa!

》7.Petro alikataa cheo! 1petro 5:3
Tena alimkatalia kornelio asimsujudie akisema yeye ni mwanadamu kama yeye.
•Huyu mwingine anasema yeye ni papa (badala ya Mwana), kufuru kubwa hii!!!

》8.Petro hajui kitu kinachoitwa utatu mtakatifu! Bali anamjua Baba ametukuzwa katika Mwana maana alijua Ni Mungu Mmoja katika ofisi ya Mwana. Na jina la Baba ni Yesu. Ndio maana amebatiza kwa jina la Yesu matendo 2:38, 10:46-48.
•Papa akamgawanya Mungu kuwa watatu.
•Papa akasasema Roho mtakatifu na Yesu ni vitu viwili tofauti. Japo wote ni Mungu.

》9.Petro anamjua Mwamba mmoja tu; naye ni kristo 1petro 2:8
•papa anasema Petro ndiye Mwamba kulingana na maandiko ya Mathayo 16:18.

》10.Petro hajawahi kuomba kwa wafu, wala kwa Maria, wala rozali, wala sala ya imani. Anasema;
3 Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa MANENO YALIYOTUNGWA; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii.
2 Petro 2:3

》11. Petro mpaka kesho hajui kitu kama PAGATORI. anajua kuzimu ni halisi.
Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;
Waebrania 9:27
Hamna mangojeo ambapo unaweza kuombewa na ukatoka kuzimu na kuingia Peponi. Hamna!

》12.Petro hakuwa na ibada za wafu hata siku moja. Wala kuomba kutoka kwa watakatifu wa zamani hata kuwafanya wawe watakatifu baada ya kufa.

HITIMISHO
Tofauti kubwa kiujumla iliyopo hapa ni NI MMOJA KUENENDA KATIKA ROHO (PETRO) na mwingine katika MWILI (PAPA)
Maana hata huyo Roho mtakatifu hajui kuwa ni Roho wa Yesu. Papa anajua Roho mtakatifu ni Mungu wa Tatu

29 Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi;
Matendo ya Mitume 20:29
Mbwa wakali ni hao walioleta upagani ndani ya kanisa. Walileta mambo ambayo hata mitume wenyewe walisema kabla hawajaondoka hapa duniani kwa uvuvio wa Roho mtakatifu

Kimsingi kanisa la mitume sio katoliki. Mitume walianzisha kanisa sio dhehebu! Mpaka mwaka 321BK, ndipo Ukatiliki Na ndoa kati yake na UPAGANI ikafungwa.

Sikilizeni wana wa Kahaba; Si kwa damu na nyama mtaokolewa ama kwa mapenzi yenu wenyewe ama dhehebu. Bali ni kila nafsi inayomkili Yesu. Halafu ikabatizwa kwa jina la Yesu.
Bila Ubatizo wa Roho mtakatifu mtu hataweza kuingia katika ufalme wa mbinguni, huyo ndiye Roho wa Yesu. Bila huyo huwezi kitu na wala si wake. Na yesu hakai na mtu mwenye udhehebu na ibada za sanamu hata siku moja.

Tubu leo ili umrudie Mungu wa kweli, ukitubu kwa kumaanisha kabisa na kugeuka na kiziacha dhambi zako kabisa. Ndipo Roho wa Mungu atakutengeza uwe mrithi wa agano sawa na Neno lake.
Vinginevyo, utafika wakati ambao kila mwenye mwili atasimama katika hukumu ya kiti cha Enzi peke yako. Na Biblia ndio kitabu kitakachofunguliwa sio dhehebu na Liturujia zake, katekisim, wala maria ama petro ama chochote kile. Ni wewe na matendo yako. Ndipo utajua kuwa huyo uliyekuwa unamwita Baba mtakatifu, papa, paroko, hutasimama naye.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NAO WANIABUDU BURE!

NIMEWAPELEKEA TAUNI KAMA YA MISRI (CORONA) LAKINI HAMKUNIRUDIA MIMI

JE! NAWEZA KUWA SAFI NAMI NINA MIZANI YA UDHALIMU!!