NIMEWAPELEKEA TAUNI KAMA YA MISRI (CORONA) LAKINI HAMKUNIRUDIA MIMI

Nakusalimu katika Jina la Yesu kristo. Tumshukuru Bwana maana fadhili zake ni za milele.
Mungu wetu ni mmoja na Jina lake ni YESU(YEHOVA MWOKOZI).

Kuna mitazamo mingi kuhusu ugonjwa wa CORONA, wengine wakisema ni uzushi, wengine wakisema ni njama za Kutafta New (one) world govt kwamba chanjo yake itaambatana na kuwekewa microchip (TRACKING DEVICE). Na wengine ni watumishi wa Mungu (mitume na manabii wa hiari) wakasema wamewekwa kwa ajili ya saa kama hii na Wakatabili ugonjwa huo hautafika Tanzania; lakini ajabu ukafika na watu wakaendelea KUWAINUA na Kuwasifu (Luka 6:26)
Hiyo ni baadhi ya mitazamo, lakini kwangu mimi CORONA ni tauni kutoka kwa Bwana(hasira ya Bwana) juu ya maovu yetu. Nakumbuka katika ndoto 30/5/2020, niliota ugonjwa ugonjwa ule umenipata na hali yangu ilikuwa ya kawaida na wala sikuwa na hofu yoyote; wakati huo alikuwepo kondakta wa daladala mmoja tumekaa naye tukimsubili konda mwenzake ambaye alikuwa ametoka na ndio nilikuwa namdai chenji yangu iliyonifanya nimsubili stand. Huyu konda niliyekuwa naye pale alikuwa mkenya, alipokea simu kutoka kwa ndugu yake akimwelezea hali ya huko kwao juu ya Corona, akaeleza juu ya hofu kuu iliyoko huko na jinsi wanavyopata taabu maana wamefungiwa. Ndoto hii sikuielewa mwanzoni lakini hivi karibuni nikaielewa maana Tanzania hatukuwa na lockdown, pia Mungu amesema tutakanyaga ng'e na nyoka wala hakuna kitakachotuzuru; kumaanisha kuwa ni kweli mabaya yatatufika, Corona itanifikia lakini Haitanidhuru.

Lakini kwa nini Bwana ameruhusu hii tauni?(CORONA)???

7 Tena nimeizuia mvua msiipate, ilipobaki miezi mitatu kabla ya mavuno; nami nimenyesha mvua juu ya mji mmoja, nikaizuia mvua isinyeshe juu ya mji mwingine; sehemu moja ilipata mvua, na sehemu isiyopata mvua ilikatika.
Amosi 4:7

8 Basi kutoka miji miwili mitatu walitanga-tanga kuendea mji mwingine wapate kunywa maji, wasipate ya kuwatosha; lakini hamkunirudia mimi, asema Bwana.
Amosi 4:8

9 Nami nimewapiga kwa ukavu na koga; wingi wa bustani zenu na mashamba yenu ya mizabibu, na mitini yenu na mizeituni yenu imeliwa na tunutu; Lakini hamkunirudia mimi, asema Bwana.
Amosi 4:9

10 Nimewapelekea tauni, kama tauni ya Misri; vijana wenu nimewaua kwa upanga, na farasi wenu nimewachukulia mbali; nami nimeupandisha uvundo wa matuo yenu na kuuingiza katika mianzi ya pua zenu; lakini hamkunirudia mimi, asema Bwana.
Amosi 4:10

Hiyo ndio sababu Bwana analeta mabaya, ni kwa sababu tupate KUMRUDIA. Amesema Yeye hufisha naye HUHUISHA! Anatupiga na Tauni ili tupate kugeuka na kuacha njia zetu mbaya. Sasa kumbuka kuwa Mpaka Bwana anafikia kukuangamiza lazima awe amekuonya, na Bwana hakuadhibu mara tu unapokosea ama pindi unakosea; bali wakati huo huwa anakuonya kwa njia mbalimbali tena kwa msisitizo. Soma kitabu cha Yeremia utaona jinsi alivyotoka mapema kuwahubilia Israeli waache dhambi, la wataenda utumwani. Lakini wao hawakusikia mpaka ulipofika wakati ambao Asitake kuwaponya tena, israeli ikachukuliwa kwenda Ashuru na Yuda akaenda Babeli.

Kama ni dhambi tulishatenda, kinachotakiwa ni KUTUBU! Na CORONA iwe imetengenezwa maabara ama imetokea kwa Popo; Ni mapenzi ya Mungu iwepo ili kumfanya kila mwenye mwili amgeukie mwokozi. Ilitabiliwa katika maandiko matatifu kuwa kutakuwa na tauni,

kutakuwa na matetemeko makubwa ya nchi; na njaa na TAUNI mahali mahali; na mambo ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.
Luka 21:11

Rais wetu ametuepusha na Lockdown, akasema CORONA imeisha, Amina! Tumeshinda kwa IMANI. Lakini lipo jambo moja Mungu anataka watu wamgeukie Yeye kwa matendo ya haki na Kumjua Yeye. Lakini Rais yeye hajui hilo. Ametangaza amani amani wakati hamna amani. Mambo yale yale yaliyotendeka huko katika wafalme ambao hawakutaka kutabiliwa mabaya ila mazuri. Leo anakusanya manabii vipofu na manabii wa baali(wasiomjua na kumkiri Yesu yaani Mungu) kuja kuombea nchi!!!!

Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
2 Wakorintho 6:14

Kwa maarifa ya mwanadamu yanaona hapo ni Busara maana Raisi analeta usawa maana Mungu ni mmoja. Ni kweli Mungu ni mmoja naye ni Yesu. Ni Mungu wa wote maana ndiye aliyetuumba lakini haina maana mchawi anamwabudu Mungu kwa uchawi wake.
Mungu ameifanya Hekima ya dunia hii kuwa upumbuvu!! Hekima ya kuingia kwenye kanisa na kuchangisha michango ya kujenga madhabahu za Baali. Namwombea Kila siku Apate maarifa na hekima ya mbinguni lakini zaidi ATUBU! Maana amehubili amani badala ya Upanga! Nao watu wamerudi nyuma wasitubu dhambi zao, Je mtaokoka na upanga wa Mungu kwa sababu aliwaponya na Corona?

Tubuni na kugeuka na kuacha njia mbaya. Siku hizi ni siku za Mwisho, Siasa ni kujilisha Upepo, Jambo linalofuata ni Unyakuo na baada ya hapo ni Siku ya Bwana iliyokuu na ya kuogofya. Maasi yanaongezeka ili kumfanya Bibi harusi azidi kujitakasa. Ina maana kama unatenda maovu unamsaidia bibi harusi(kanisa) lizidi kujitakasa. Mpumbavu atazidi kuamnini dhehebu na kuabudu sanamu kazi ya mikono ya mwanadamu. Mpumbavu atazidi kuvaa vimini na mavazi ya kahaba, kuweka kope, kucha, bandia na huku akiingia hekaluni kuabudu. Mungu amesema uchague moja Moto(kuyatenda mapenzi yake) ama baridi(kuwa mpagani) na sio Vuguvugu(nusu kwa Mungu nusu kwa shetani). Unapoteza mda na hao manabii wako wa uongo waliokudanganya na kukutumainisha uongo. Wakakwambia hamna shida kuvaa wigi,kuvaa suruali(vazi la mwanaume), kunyoa kiduku, kuhubili siasa, kwenda uchi, kunywa pombe, kuabudu sanamu ya maria na watakatifu waliolala, kuabudu siku, jua,mwezi na jeshi lote la mbinguni. Ni kweli biblia ilisema;

3 Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;
2 Timotheo 4:3

4 nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.
2 Timotheo 4:4

Hao makundi ya walimu na elimu zao wapo na wamefanya wengi kujitenga na imani kwa maneno ya uongo. Kuna kazi kama unataka kuingia mbinguni huwezi kuzifanya kama Usanii, uigizaji, kucheza mpira ama kuwa shabiki, kuuza baa, guest, kubeti ama kufanya kazi kwenye hizo kampuni, salooni za kike. Na wale wanaonyoa viduku na mitindo katika saloon za kiume, kwa sababu ni kazi ambazo zipo chini ya kiti cha enzi cha shetani, hayo yote kwa walimu hao waliotajwa kwao watakwambia haina shida. Na ndio maana watu wanoshindana na Mungu leo kwa asilimia kubwa ni wakristo. Hawataki injili ya kweli bali maneno laini.

9 Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya Bwana;
Isaya 30:9

10 wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo;
Isaya 30:10

By Mashibe Elias Ntinginya

Shalom!

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NAO WANIABUDU BURE!

JE! NAWEZA KUWA SAFI NAMI NINA MIZANI YA UDHALIMU!!