NAO WANIABUDU BURE!
Nawasalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu kristo, Na karibu tujifunze maarifa
ya mbinguni.
Siku tunazoishi ni siku za mwisho, Bwana alisema atakuja kama Mwivi! Sio kwamba anakusudia kuja namna hiyo ili kutukomoa kwamba tusiende mbinguni; bali ni kwa sababu watu wapo gizani, wamelala usingizi wa kiroho, hao ndio atawajilia kama mwivi. watakuwa hawajui majira ya kujiliwa kwao. watakuwa wametingwa na shughuli na masumbusu ya mali. watalewa na mali, watalewa na mvinyo, watakuwa walafi wa mambo ya dunia.
Majira na nyakati tunazoishi sasa hivi ndio majira tutakaposhuhudia kuja kwa pili kwa kristo kama Mwivi, katika tukio lijulikanalo kama UNYAKUO. lakini kuna jambo moja tunapaswa tulifahamu kuwa kanisa la leo ni VUGUVUGU. Na Bwana ameahidi atalitapika Ufunuo 3:14-16 .
Kutapikwa kunakozungumziwa ni kukataliwa/Kukanwa na Kristo. Ni mtu ambaye amemkiri Kristo lakini matendo yake ni kinyume na nuru kwa kujua ama kutokujua. Wapo watu ambao hawajui kama wamemwacha Bwana; hao huenda kanisani pengine kila jumapili lakini wanachokijua hakuna zaidi ya DHEHEBU lake.
Tambua kuwa dhehebu limemwacha ROHO MTAKATIFU na kushika theolojia(mafundisho ya wanadamu). Kila mtu aliyechini ya madhabahu hizo kweli ya Mungu kwake ni Fumbo gumu. Hata anapolisoma Neno la Mungu ni kutafta namna lingeweza kuendana na mawazo yake. Utakuta mtu anasoma Biblia akitaka Biblia imthibitishe Bikira maria, mwingine sabato, mwingine mafuta. Cha ajabu ni kwamba, Hata mwizi akitaka kuhalalisha wizi wake kuwa ni sawa; atapata mistari ya kuunga mkono hoja yake katika Biblia. Yaani unaweza kuhalalisha Dhambi yoyote katika Biblia na unaweza kupata fasiri yoyote unayoitaka wewe, Pasipo Roho mtakatifu huwezi kamwe kuijua kweli ya Mungu hata uwe unakesha na Biblia.
Karne ya 20 mwishoni na karne hii ya 21 kumekuwepo na manabii na makristo wa uongo wengi kama ilivyotabiliwa na hadi sasa wamezaa matunda yao na karibu mahubili yote sasa hivi ni ya manabii na makristo wa uongo. Ndio maana mtu akihubiliwa kweli hasa ya Mungu anabaki kupinga, amezoelea ama amekulia katika maziwa yaliyogoshiwa; hivyo akinywa maziwa halisi anahisi ndiyo yaliyogoshiwa, japo ni kiunafiki maana anakuwa anajua kabisa haya maziwa ni mazito, si mepesi kama niliyozoea. Licha ya kuwa wanashuhudiwa katika dhimiri zao na Roho mtakatifu lakini wanakaza shingo ili kuwapendeza wanadamu.
Tunahesabiwa haki kwa imani na sio kwa matendo! Matendo yetu hata tungefanya mazuri kiasi gani hayawezi kutufikisha mbinguni, lazima kutakuwa na kasoro mahali, hivyo badala yake matendo ya kristo aliyeishi maisha makamilifu ndio sisi tunahesabiwa katika hayo, ndio maana tunapaswa kumwamini Yeye ili yale matendo yake yawe yetu yaani kama vazi letu. Mungu anapokuwa anatutazama ayaone matendo ya Yesu na si yetu. Yeye ndie atatupa uweza wa kushinda nguvu za ibilisi kama alivyoshinda.
Yesu hayupo pamoja nasi wakati huu kwa maana ya jinsi ya kimwili bali yupo pamoja nasi kwa jinsi ya Roho wake(Roho mtakatifu). Hivyo ukimpokea Yesu na kubatizwa kwa maji mengi na kwa jina la Yesu(Matendo 2:38, 8:16, 10:46-48, 19:3-5) unakuwa halali Roho mtakatifu kuingia kwako. Roho wa Yesu atakufanya kuwa kama alivyo; Yeye ni mtakatifu, ndivyo hata wewe atakufanya kuwa mtakatifu. Na kama unajua umempokea halafu maisha yako ni kuvaa vimini, kunyoa kiduku, kuvaa nguo za kubana, Kuvaa suali(wanawake), kupaka rangi nywele/kucha. kuvaa nguo za kubana, kusuka na kuvaa mawigi, unaishi na mwanaume/mwanamke asiye mkeo; Ujue unajidanganya na nafsi yako. Haijalishi utakuwa unanena kwa lugha, utakuwa unaponya wagonjwa, utakuwa unafufua wafu, utakuwa unaota ndoto ama kuona maono, Ama utakuwa kwenye dhehebu zuri kiasi gani, Hata kama umekalili liturujia zenu zote. Utakuwa unamwabudu Mungu bure!!
Tubu sasa kwa kumaanisha na kuanza kumtafta Mungu wa kweli na utoke katika mila na desturi za kidhehebu. Inawezekana kuacha dhambi ukiwa na roho mtakatifu tu. Tofauti na hapo utakuwa unatubu kila siku na kurudia dhambi tena kesho yake kama mtu asiye na maarifa.
Maran atha!
Mawasiliano; 0755251999.
Pia kama utaona vyema kumtolea Mungu tumia hiyo namba.

4 Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.Walio katika nuru wataitambua siku hiyo. Mwivi huja wakati mwenye nyumba amelala, na kama angekesha asingeibiwa. Ndio maana sisi wenyewe tukeshao; hapa haimaanishi mikesha, bali Kutokusinzia kiroho. Usilale kiroho usiku na mchana. Na Siku inayozungumziwa hapo ni siku ya Unyakuo wa kanisa. Lakini watu wengu kutokana na mafundisho ya wanadamu; hawajui jambo hili na wengine wamesikia na kuamini kuwa kutakuwepo unyakuo lakini hawajui ni kwa namna gani na ni lini hasa. Sisemi kuwa naijua siku ama saa, la! bali majira.
1 Wathesalonike 5:4
Majira na nyakati tunazoishi sasa hivi ndio majira tutakaposhuhudia kuja kwa pili kwa kristo kama Mwivi, katika tukio lijulikanalo kama UNYAKUO. lakini kuna jambo moja tunapaswa tulifahamu kuwa kanisa la leo ni VUGUVUGU. Na Bwana ameahidi atalitapika Ufunuo 3:14-16 .
Kutapikwa kunakozungumziwa ni kukataliwa/Kukanwa na Kristo. Ni mtu ambaye amemkiri Kristo lakini matendo yake ni kinyume na nuru kwa kujua ama kutokujua. Wapo watu ambao hawajui kama wamemwacha Bwana; hao huenda kanisani pengine kila jumapili lakini wanachokijua hakuna zaidi ya DHEHEBU lake.
Tambua kuwa dhehebu limemwacha ROHO MTAKATIFU na kushika theolojia(mafundisho ya wanadamu). Kila mtu aliyechini ya madhabahu hizo kweli ya Mungu kwake ni Fumbo gumu. Hata anapolisoma Neno la Mungu ni kutafta namna lingeweza kuendana na mawazo yake. Utakuta mtu anasoma Biblia akitaka Biblia imthibitishe Bikira maria, mwingine sabato, mwingine mafuta. Cha ajabu ni kwamba, Hata mwizi akitaka kuhalalisha wizi wake kuwa ni sawa; atapata mistari ya kuunga mkono hoja yake katika Biblia. Yaani unaweza kuhalalisha Dhambi yoyote katika Biblia na unaweza kupata fasiri yoyote unayoitaka wewe, Pasipo Roho mtakatifu huwezi kamwe kuijua kweli ya Mungu hata uwe unakesha na Biblia.
Karne ya 20 mwishoni na karne hii ya 21 kumekuwepo na manabii na makristo wa uongo wengi kama ilivyotabiliwa na hadi sasa wamezaa matunda yao na karibu mahubili yote sasa hivi ni ya manabii na makristo wa uongo. Ndio maana mtu akihubiliwa kweli hasa ya Mungu anabaki kupinga, amezoelea ama amekulia katika maziwa yaliyogoshiwa; hivyo akinywa maziwa halisi anahisi ndiyo yaliyogoshiwa, japo ni kiunafiki maana anakuwa anajua kabisa haya maziwa ni mazito, si mepesi kama niliyozoea. Licha ya kuwa wanashuhudiwa katika dhimiri zao na Roho mtakatifu lakini wanakaza shingo ili kuwapendeza wanadamu.
6 Akawaambia, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa, Watu hawa huniheshimu kwa midomo Ila mioyo yao iko mbali nami;Haijalishi utakuwa na jengo zuri kiasi gani, haijalishi utakuwa unaitwa jina kubwa kiasi gani; Papa, nabii, nabii mkuu, baba mchungaji, Askofu, askofu mkuu ama chochote kile na umewafanya watu wakuone wewe kama ndio kristo, uyafanyayo ni bure. Vipofu wenu hawamjui kristo bali ninyi, wanakanyaga sheria za Yesu lakini mafundisho yenu wanatii. Mtu ametii mafundisho ya mwanadamu, hata asile nyama siku aliyosulubiwa Yesu(wanaita ijumaa kuu), Lakini anamwomba maria kama mpatanishi wake; ni unafiki uliyopitiliza! huli nyama ili iweje sasa? wakati mpatanishi wako ni mwingine? Yesu alisema Yeye ndiye njia, lakini wewe umefanya Mariamu awe njia, mwingine Kushika siku fulani(akaibatiza kwa kivuli cha sabato) ndio njia. Yaani hata mkiwaambia wafuasi wenu wawaite Mungu watawaita, jaribuni muone kama watagoma, wao wana kiu, hata mkiwapa maji ya tope watakunywa tu. Isaya alitabili pia;
Marko 7:6
7 NAO WANIABUDU BURE, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu, Marko 7:7
1 Ole wa watoto waasi; asema Bwana; watakao mashauri lakini hawayataki kwangu mimi; wajifunikao kifuniko lakini si cha roho yangu; wapate kuongeza dhambi juu ya dhambi;Jiulize leo, mchungaji/nabii/mtume wako ni mkuu kuliko Yesu? watu wa kanisa la kwanza waliwajaribu hao wajiitao ni mitume wakawajua kuwa sio. lakini leo utaambiwa Mungu atakupiga ukijaribu jambo kama hilo. Ndio Kanisa letu Laodikia ni Vuguvugu maana tumechukuliana nao na tumewaona wanatufaa, japo ni kwa unafiki. Tofauti na kanisa la kwanza ambalo lilisifiwa. Leo utamhubilia mtu wa udhehebu halafu swali lake atakuuliza "Upo chini ya askofu/mchungaji nani?" ukisema Yesu atakuona wa ajabu? pengine atabadili swali "Baba yako wa kiroho ni nani?" anachotaka ni kulinganisha huyo wako na wake! Na usipotaja atakuona takataka. Hizo ndizo fumbo za shetani!
Isaya 30:1
13 Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walicho nacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa;Nakushauri, Ondoa kiambaza cha Udhehebu/udini na uanze kusoma Neno kwa kutegemea ufunuo wa Roho mtakatifu. Bila Yesu ndani yako hata ingekuwa na dini nzuri kiasi gani hutaingia mbinguni.
Isaya 29:13
14 kwa sababu hiyo mimi nitafanya tena kazi ya ajabu kati ya watu hawa, kazi ya ajabu na mwujiza; na akili za watu wao wenye akili zitapotea, na ufahamu wa wenye busara wao(wachungaji/manabii/maaskofu/mapadre/mapapa wao) utafichwa.
Isaya 29:14
Tunahesabiwa haki kwa imani na sio kwa matendo! Matendo yetu hata tungefanya mazuri kiasi gani hayawezi kutufikisha mbinguni, lazima kutakuwa na kasoro mahali, hivyo badala yake matendo ya kristo aliyeishi maisha makamilifu ndio sisi tunahesabiwa katika hayo, ndio maana tunapaswa kumwamini Yeye ili yale matendo yake yawe yetu yaani kama vazi letu. Mungu anapokuwa anatutazama ayaone matendo ya Yesu na si yetu. Yeye ndie atatupa uweza wa kushinda nguvu za ibilisi kama alivyoshinda.
Yesu hayupo pamoja nasi wakati huu kwa maana ya jinsi ya kimwili bali yupo pamoja nasi kwa jinsi ya Roho wake(Roho mtakatifu). Hivyo ukimpokea Yesu na kubatizwa kwa maji mengi na kwa jina la Yesu(Matendo 2:38, 8:16, 10:46-48, 19:3-5) unakuwa halali Roho mtakatifu kuingia kwako. Roho wa Yesu atakufanya kuwa kama alivyo; Yeye ni mtakatifu, ndivyo hata wewe atakufanya kuwa mtakatifu. Na kama unajua umempokea halafu maisha yako ni kuvaa vimini, kunyoa kiduku, kuvaa nguo za kubana, Kuvaa suali(wanawake), kupaka rangi nywele/kucha. kuvaa nguo za kubana, kusuka na kuvaa mawigi, unaishi na mwanaume/mwanamke asiye mkeo; Ujue unajidanganya na nafsi yako. Haijalishi utakuwa unanena kwa lugha, utakuwa unaponya wagonjwa, utakuwa unafufua wafu, utakuwa unaota ndoto ama kuona maono, Ama utakuwa kwenye dhehebu zuri kiasi gani, Hata kama umekalili liturujia zenu zote. Utakuwa unamwabudu Mungu bure!!
4 Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.Sharti uwe mtakatifu kama alivyo maana ndiyo kazi yake akiingia kwako. Usiuige ulimwengu bali iga matendo ya kristo. Penda kumjua Mungu zaidi ya ulivyokuwa unamfahamu hapo kwanza. Epuka injili zinazo kutazamisha kwenye baraka pekee(HAMNA BARAKA KWA MWENYE DHAMBI, BADALA YAKE NI LAANA. Epuka injili zinazokufanya umchukie adui badala ya kumpenda(kumwombea). Injili inakufanya uutazame ulimwengu badala ya mbinguni ni ya ibilisi. Mungu sio mganga wa kienyeji kwamba akuponye ili ukaendelee na dhambi zako; hivyo injili zinazojikita na uponyaji tu bila kuhubili toba juu ya wale watu. Ni ya manabii/makristo wa uongo. Ukiona madhabahu kama hizo kimbia, ukiona mavazi yanayovaliwa na waumini hayana tofauti na wasanii wa dunia ama malaya wajiuzao; usisubili muujiza kimbia.
Yakobo 4:4
Tubu sasa kwa kumaanisha na kuanza kumtafta Mungu wa kweli na utoke katika mila na desturi za kidhehebu. Inawezekana kuacha dhambi ukiwa na roho mtakatifu tu. Tofauti na hapo utakuwa unatubu kila siku na kurudia dhambi tena kesho yake kama mtu asiye na maarifa.
Maran atha!
Mawasiliano; 0755251999.
Pia kama utaona vyema kumtolea Mungu tumia hiyo namba.
Maoni
Chapisha Maoni
Tafadhali, share kwa wengine ili kuisambaza injili kwa watu wote na Mungu wa mbinguni atakubariki.
Unaweza kutumia namba hii 0755251999 kuwasiliana kwa njia ya whatsapp