UWE NA UTUNGU, UTAABIKE ILI UZAE!
Jina la Bwana litukuzwe, Salaam wapendwa!
Karibuni katika chakula cha kiroho.
Umewahi kufikilia maumivu gani mwanamke hupata wakati wa utungu? Amewekewa sharti apate utungu ili azae tangu alipoasi Edeni kama moja ya laana Bwana aliyoitoa. Sasa katika unabii mwanamke huwakilisha Kanisa. Tazama kwa makini katika kanisa; Utagundua kuwa jinsi mwanamke alivyo katika jamii ndivyo kanisa lilivyo. Angalia hilo utaliona katika nyakati zote zilizopita na uje uangalie Mwanamke wa sasa na kanisa la Sasa lilivyo. Jinsi mwanamke alivyojiharibu ndivyo kanisa lilivyo (ukahaba, uzinzi, uasherati, mavazi(matendo) machafu n.k), kanisa pia lina tabia za namna hiyo.
Nataka tutazame amri ya utungu kwa mwanamke na kuzaa kwa taabu, Amri hii ni kwa kanisa pia. Tazama kanisa la kale yaani israel; jinsi Mungu alivyolitoa katika hatia ya misri ya kuabudu sanamu(uasherati). Akaliposa na kuwa mke kwa Bwana. Licha ya kwamba Bwana alikuwa nao kuwaongoza njia kufika kanaani lakini aliwapitisha katika maumivu chungu nzima mpaka kufika Kanaani. Bado ulifika wakati akawapeleka utumwani tena, Ashuru na Babeli katika dhiki kubwa na baadae akawatoa huko kwa rehema nao wakamtumikia Bwana.
Leo tunasimama tukimwona Bwana katika Nuru kubwa baada ya israeli kupitia utungu mwingi kutuzaa sisi.Sharti kanisa lipate utungu, litaabike ili lizae. Baada ya Eva kuanguka alizaa kwa utungu; Kanisa lilipoanguka lilizaa kwa utungu.
Mungu alichagua israel kati ya mataifa mengi, baadae akaimega na kuchagua Yuda ambako ndiko mfalme (Yesu) alitoka. Baadae tukazaliwa sisi kama israeli hapo mwanzo. Kanisa lilikuwa moja lenye uweza wa Mungu. Baadae dhambi ikaingia ndani ya Kanisa kama kwa isaraeli. Mungu akamtoa Protestanti(Yuda) kutoka kwa Katoliki.
Kama vile israel alivyoasi na kupelekwa utumwani; vivyo hivyo Yuda naye bila hiana akafanya yale yale israeli aliyoyafanya tena kwa kiburi maana alimwona Israeli wakati anachukuliwa mateka. Ndivyo ilivyo kwa Kanisa la Kiprotestanti, licha ya kuona uasi na dhambi ya kanisa karoliki kwa sanamu zake na uzinzi wa kiroho inaoufanya, akatoka na kujitenga lakini bado akafanya uzinzi kama wa mama yake. Kama vile Yuda naye alivyopelekwa utumwani kama israel ndivyo itakavyokuwa siku za mwisho kwa madhehebu haya yote kwenda katika ile Dhiki kuu.
Yeremia aliihubili sana Yuda iache ouvu lakini aliishia kupigwa makofi na makuhani mpaka yakatimia yote aliyoyatabili. Mungu aliwapeleka kule ili wapate kufahamu makosa yao na kugeuka(wapate dhiki na kugeuka kuacha njia zao mbaya).
Huyo ni Yuda, Leo sisi tupo kanisa la Laodikia, Kanisa la mwisho na tupo kileleni kufika katika ahadi ya Bwana lakini tabia ya kanisa hili usihangaike kuijua bali tazama mwanamke wa leo. Bwana ametutupa kwenye CORONA, huku nako ili tupate dhiki tupate kugeuka. Cha kushangaza ni kuwa Watu hawapo tayari kumtafta Bwana wala hawajui makosa yao. Ilikuwa hivyo kwa Yuda! Yeremia alipohubili waacha dhambi wao hawakujua waache dhambi zipi walizomtenda Bwana!
Ndivyo wakati huu watu wa Mungu walivyo, hawajui dhambi zao na hata wakihubiliwa huwapiga wahubili wa kweli kwa maneno makali maana wanajiona wako sawa licha ya kuwa Roho mtakatifu anawashuhudia dhamiri zao kuwa dhambi imo ndani yao.
Mungu amesema ipo dhiki kuu na siku ya kuogofya ya hasira yake! Lakini hata ukiwahubili umevua nguo bado hawatasikia, wanaishia kukuona UNAEJIFANYA MTAKATIFU. Wala huna nabii mkubwa kama wake ama mtume ama mchungaji ama Papa ama askofu ama chochote kile.
Wanataka kuona unatoka kanisa tajiri kama lao ama zaidi na sio vijikanisa kama wanavyoita.
Sasa CORONA hii Bibi harusi atajitakasa sana kwa sababu anatambua majira ya kujiliwa kwake huku wengine wakiendelea kutafta manabii na mitume na wengi kujitahidi kuwa manabii na mitume ili watu wawasifu!!!
Leo nimeota ndoto moja, namwomba Mungu aghairi mabaya haya. Siku kadhaa nyuma baada ya kifo cha mkapa, Katika ndoto nilisikia mshindo wa kitu kutoka juu kikaanguka chini kwa mshindo mkuu. Nikasogea karibu na rafiki yangu nikimuuliza kama amesikia ule mshindo. Akiwa anatazama akasema itakuwa CORONA hiyo, akimaanisha mtu mkuu amefariki kwa ugonjwa huo. Hata mimi nilikubaliana nae. Baada ya ndoto Nilimwomba Mungu Amwepushe na hiyo Roho ya mauti japo sikumjua lakini nilimsihi pia ikimpendeza nimjue. Usiku wa kuamkia leo Nikaota tena ndoto, nilikuwa napita karibu na barabara ya lami karibu na kituo cha mwendokasi nikamwona msanii akifanya maonyesho bila watu (diamond) na pembeni yake kuna picha ya kiongozi aliyefariki. nilipoiona nikastaajabu, sikuwa na taarifa ya kifo chake maana inaonekana ana siku kadhaa toka afariki na sababu ilikuwa dhahiri kwangu kuwa ni CORONA. Moyoni nikawa nawaza kumbe ndio huyu niliyeoneshwa atafariki? Jina la huyo kiongozi linaanza na N na linalofuata linaanza na Nn. Kimsingi natambua jukumu ni kumwomba Mungu aghairi maana mpaka ananionesha kabla ina maana anataka apone(nazidi kumwomba Mungu) na ninapoandika hapa nataka na wewe uombe na kutubu na pia kumfikishia huyo mlengwa ujumbe ili atubu! Nataka rehema wala sio mauti. Katika hiyo ndoto nilitoka pale nikakutana na mtu mmoja alionekana kuwa mbunge akawa anaongea na mbunge mwenziwe kwa njia ya simu akimpa taarifa ya vifo wa watu waliofariki kwa ugonjwa huu wa Corona. Ni kama ugonjwa ulirudi mara ya pili. Waliokuwa wamefariki kwa mjibu wa ripoti yake wengi ni madaktari na viongozi. Wakati nikiwa pale nasikiliza Nikakumbuka kuwa nina jukumu la kuhubili lakini sijafanya hivyo, Roho yangu ikararuka. Kumbuka nahubili sana mtandao ukilinganisha na ana kwa ana. Hivyo nikasema ole wangu mimi Bwana akija sijahubili ama nikifariki na huo ugonjwa sijahubili. Nikajionea aibu na kuondoka kwenda kuhubili mitaani.
Nasema haya utafakari wewe unayekaza shingo, Lakini ewe ambaye unamcha Bwana uombe juu ya kiongozi huyu na Taifa zima kwa ujumla. Omba bila kukoma. Bwana hughairi maovu.
Tupo karibu na unyakuo Usikose siku hiyo maana siku ya Bwana ni siku ya kuogofya mno Amosi 5:18-20. Na Bwana amesema tuutafte unyenyekevu na haki huenda akatuficha(akatunyakua) siku hiyo.
Shalom!

9 Sasa mbona unapiga kelele? Je! Hakuna mfalme kwako, mshauri wako amepotea, hata umeshikwa na utungu kama mwanamke wakati wa kuzaa?
Mika 4:9
10 Uwe na utungu, utaabike ili uzae, Ee binti Sayuni, kama mwanamke mwenye utungu; maana sasa utatoka mjini, nawe utakaa katika mashamba; utafika hata Babeli; huko ndiko utakakookolewa; huko ndiko Bwana atakakokukomboa katika mikono ya adui zako. Mika 4:10
Huyo ni Yuda, Leo sisi tupo kanisa la Laodikia, Kanisa la mwisho na tupo kileleni kufika katika ahadi ya Bwana lakini tabia ya kanisa hili usihangaike kuijua bali tazama mwanamke wa leo. Bwana ametutupa kwenye CORONA, huku nako ili tupate dhiki tupate kugeuka. Cha kushangaza ni kuwa Watu hawapo tayari kumtafta Bwana wala hawajui makosa yao. Ilikuwa hivyo kwa Yuda! Yeremia alipohubili waacha dhambi wao hawakujua waache dhambi zipi walizomtenda Bwana!
6 Nalisikiliza nikasikia, lakini walisema yasiyo sawa; hapana mtu aliyetubia maovu yake, akisema, Nimefanya nini? Kila mtu hurudia mwendo wake mwenyewe, kama farasi aendavyo kasi vitani.
Yeremia 8:6
Ndivyo wakati huu watu wa Mungu walivyo, hawajui dhambi zao na hata wakihubiliwa huwapiga wahubili wa kweli kwa maneno makali maana wanajiona wako sawa licha ya kuwa Roho mtakatifu anawashuhudia dhamiri zao kuwa dhambi imo ndani yao.
18 Hapo ndipo waliposema, Njoni na tufanye mashauri juu ya Yeremia; maana sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye hekima, wala neno halitampotea nabii. Njoni, na tumpige kwa ndimi zetu, wala tusiyaangalie maneno yake yo yote.
Yeremia 18:18
Mungu amesema ipo dhiki kuu na siku ya kuogofya ya hasira yake! Lakini hata ukiwahubili umevua nguo bado hawatasikia, wanaishia kukuona UNAEJIFANYA MTAKATIFU. Wala huna nabii mkubwa kama wake ama mtume ama mchungaji ama Papa ama askofu ama chochote kile.
Wanataka kuona unatoka kanisa tajiri kama lao ama zaidi na sio vijikanisa kama wanavyoita.
Sasa CORONA hii Bibi harusi atajitakasa sana kwa sababu anatambua majira ya kujiliwa kwake huku wengine wakiendelea kutafta manabii na mitume na wengi kujitahidi kuwa manabii na mitume ili watu wawasifu!!!
Leo nimeota ndoto moja, namwomba Mungu aghairi mabaya haya. Siku kadhaa nyuma baada ya kifo cha mkapa, Katika ndoto nilisikia mshindo wa kitu kutoka juu kikaanguka chini kwa mshindo mkuu. Nikasogea karibu na rafiki yangu nikimuuliza kama amesikia ule mshindo. Akiwa anatazama akasema itakuwa CORONA hiyo, akimaanisha mtu mkuu amefariki kwa ugonjwa huo. Hata mimi nilikubaliana nae. Baada ya ndoto Nilimwomba Mungu Amwepushe na hiyo Roho ya mauti japo sikumjua lakini nilimsihi pia ikimpendeza nimjue. Usiku wa kuamkia leo Nikaota tena ndoto, nilikuwa napita karibu na barabara ya lami karibu na kituo cha mwendokasi nikamwona msanii akifanya maonyesho bila watu (diamond) na pembeni yake kuna picha ya kiongozi aliyefariki. nilipoiona nikastaajabu, sikuwa na taarifa ya kifo chake maana inaonekana ana siku kadhaa toka afariki na sababu ilikuwa dhahiri kwangu kuwa ni CORONA. Moyoni nikawa nawaza kumbe ndio huyu niliyeoneshwa atafariki? Jina la huyo kiongozi linaanza na N na linalofuata linaanza na Nn. Kimsingi natambua jukumu ni kumwomba Mungu aghairi maana mpaka ananionesha kabla ina maana anataka apone(nazidi kumwomba Mungu) na ninapoandika hapa nataka na wewe uombe na kutubu na pia kumfikishia huyo mlengwa ujumbe ili atubu! Nataka rehema wala sio mauti. Katika hiyo ndoto nilitoka pale nikakutana na mtu mmoja alionekana kuwa mbunge akawa anaongea na mbunge mwenziwe kwa njia ya simu akimpa taarifa ya vifo wa watu waliofariki kwa ugonjwa huu wa Corona. Ni kama ugonjwa ulirudi mara ya pili. Waliokuwa wamefariki kwa mjibu wa ripoti yake wengi ni madaktari na viongozi. Wakati nikiwa pale nasikiliza Nikakumbuka kuwa nina jukumu la kuhubili lakini sijafanya hivyo, Roho yangu ikararuka. Kumbuka nahubili sana mtandao ukilinganisha na ana kwa ana. Hivyo nikasema ole wangu mimi Bwana akija sijahubili ama nikifariki na huo ugonjwa sijahubili. Nikajionea aibu na kuondoka kwenda kuhubili mitaani.
Nasema haya utafakari wewe unayekaza shingo, Lakini ewe ambaye unamcha Bwana uombe juu ya kiongozi huyu na Taifa zima kwa ujumla. Omba bila kukoma. Bwana hughairi maovu.
Tupo karibu na unyakuo Usikose siku hiyo maana siku ya Bwana ni siku ya kuogofya mno Amosi 5:18-20. Na Bwana amesema tuutafte unyenyekevu na haki huenda akatuficha(akatunyakua) siku hiyo.
3 Mtafuteni Bwana, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya Bwana.
Sefania 2:3
Shalom!
Maoni
Chapisha Maoni
Tafadhali, share kwa wengine ili kuisambaza injili kwa watu wote na Mungu wa mbinguni atakubariki.
Unaweza kutumia namba hii 0755251999 kuwasiliana kwa njia ya whatsapp