Machapisho

UDHEHEBU; DHAMBI INAYOPOTEZA WATEULE WENGI.

Picha
Shalom Mwana wa Mungu; Karibu katika chakula cha uzima, Neno la Mungu likikaa ndani yako hutaona kiu kamwe! Wapendwa katika Bwana, Tupo mwishoni kabisa katika Majira ya siku za Mwisho. Moja ya siku hizi ambazo tunaruka na kuzurura na Kuyawaza ya dunia Bwana atakuja kama umeme. Ni wakati pekee Bwana atakuja kama Mwizi yaani katika Unyakuo. Alisema tusemapo kuna Amani, Ndipo Uharibifu Uwajiapo 1wathesalonike 5:3 Mwisho wa Dunia Bwana hatakuja kama Mwizi; Hautakuwa wakati wa Amani; Kumbuka Mwisho utakuwa wakati wa Vita, Katika dhiki kuu, siku za giza nene kama ambavyo Nabii Amosi anasema Amosi 5:18-20. 18 Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya Bwana; kwani kuitamani siku ya Bwana? Ni giza, wala si nuru. Amosi 5:18 19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma. Amosi 5:19 20 Je! Siku ya Bwana haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga. Amosi 5:20 Bila shaka Unaona hapo k...

NI MAKOSA KUSEMA>USIHUKUMU! WEWE HUBILI INJILI TU, MUNGU NDIYE ANAJUA!

Picha
Bwana Yesu asifiwe wapendwa katika Bwana. Kwa upendo wa kristo nawaandikia ili kila mmoja aelewe kabla Mwisho haujafika; Kabla mlango wa Neema haujafungwa. 1 Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Mathayo 7:1 2 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa. Mathayo 7:2 Siku hizi za utawala wa shetani; siku za mwisho, hasa Watu WALIOITWA; Ukiwahubiria wazi juu ya Dhambi walizonazo utasikia USIHUKUMU wewe hubiri tu, hakuna asiyekuwa na Dhambi! ●ukiwaambia viduku, vimini, suruali za kubana, sketi za kubana, kuweka rangi nywele, kusuka, kuvaa wigi, kupaka wanja, kope bandi, Kucha bandia, kupaka kucha Rangi n.k. Watakuambia USIHUKUMU. ●Wanarejea maandiko kama hapo juu yanavyoeleza kwamba usihukumu usije ukahukumiwa. ●Ajabu ni kwamba wamekuwa ni kama watu waliochanganyikiwa katika dhambi licha ya kwamba wanaingia makanisani na kuomba. Ndugu yangu katika Bwana; Usiipake manukato dhambi kwa kutumia hili Neno pindi unapobubiliwa...

TOFAUTI KATI YA DHEHEBU NA KANISA

Picha
TOFAUTI KATI YA DHEHEBU NA KANISA Nakusalimia katika jina la Bwana wetu Yesu kristo. Karibu kujifunza Maneno matakatifu ya Mungu. Leo tutajifunza Hekima juu ya Dhehebu na Kanisa. Kabla hatujalijua Dhehebu bora tukajua Kanisa kwanza. Tunasoma mathayo 16; 13 Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana kuwa ni nani? Mathayo 16:13 14 Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. Mathayo 16:14 15 Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? Mathayo 16:15 16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Mathayo 16:16 17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. Mathayo 16:17 18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Mathayo 16:18 19 Nami nitakupa we...

USHUHUDA WA ALIYEKUWA KUHANI WA KANISA KATOLIKI

USHUHUDA WA MIGUEL VASQUEZ KUTOKA MJI WA MATAGALPA, NIKARAGUA. ASKOFU WA ZAMANI WA KANISA KATOLIKI ANYAKULIWA KWENDA MBINGUNI NA KUZIMU Mwaka 2003 Mimi ni Askofu wa kanisa la kiinjilist la Watoto wa Imani. Kabla sijawa Mkristo, nilikuwa Padre wa kanisa la Katoliki ya Kirumi. Nilisherehekea sakramenti 7 kama vile Ubatizo wa kikatoriki, Uthibitisho, Ekaristi, Kitubio, kupaka mafta mgonjwa, ndoa za kikatoliki, na Amri takatifu. Nilibatiza watoto wadogo waliozaliwa na nilipenda picha. Nilitumia maji matakatifu, mshumaa, chumvi, nguo iliyopakwa mafta na vitu vitakatifu. Nilivaa kasula na vazi lililotiwa wakfu. Nilikuwa na uaskofu wa kufundisha na nilimwabudu Maria. Kwangu mimi, alikuwa Mama wa Mungu, Mama wa kanisa, Mpatanishi, malkia wa mbinguni, mwombezi na dhana kamili kabisa. Nilijitolea kwa Maria na kuweka wakfu kila kitu kwake na niliomba sala zote kwake. Kwangu mimi, alikuwa mponyaji, Bikra daima na Mungu mke. Rafiki yangu wa ujana Carlos kutoka kanisa la pentekoste la kuzaliwa ...

MANABII NA MAKRISTO WA UONGO

Mpendwa karibu tujifunze Maneno ya Uzima ambayo ndimo utokapo uzima wa milele. Hizi ni siku za mwisho, tena tupo karibu sana na UNYAKUO ambao kimsingi itafuata Dhiki kuu baada ya huo kwa miaka saba. Ndani ya miaka saba hasira za Bwana zitawaka na ulimwengu utashuhudia mapigo ya ghadhabu ya Mwana kondoo. Sasa kwa nini ghadhabu hiyo inapaswa ije kama Yeye mwenyewe alisema Injili itahubiriwa kila mahali? Jiulize tu! Hapajakuwapo na makanisa mengi wakati wowote kama siku hizi za mwisho; Hapajashudiwa kuwa manabii wengi kama kipindi hiki; lakini ajabu ni kwamba ndio kizazi kitakachoiona ghadhabu ya Mungu! mapigo ya Ufunuo 16 yatatimizwa lakini Bibi harusi wa kristo atakuwa amenyakuliwa tayari. Siku ya Bwana ni giza mpendwa: "18 Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya Bwana; kwani kuitamani siku ya Bwana? Ni giza, wala si nuru. Amosi 5:18 19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma. Amosi 5:19 ...

SIKU HIYO JINA LA BWANA LITAKUWA MOJA!

Jina la Bwana libarikiwe; karibu kujifunza Neno la Uzima, Maana ndio Hekima ilipo Zekaria 14:9 9 Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja. Kuna vitu vingi vinaendelea katika imani ya Kikiristo mfano; mkanganyiko wa Tafsiri za Maandiko, Mmoja anaamini hivi mwingine vile, na mwingine tofouti na mwingine, Dhehebu moja hadi lingine. Najiuliza, Mungu kweli ni wa ajabu na njia zake hazichunguziki! lakini hali hii ni njia ya Mungu kweli? mbona kama vurugu? Hivi sasa unaweza ukakuta ndani ya kilomita moja makanisa hata matatu, kila mona linajinadi juu ya Mwingine. Hii inafanana sana Ngoma za kwetu usukumani (Bulabuka) hawa hushindana wawili katika eneo kati ya mita 100m hadi 200m, wanachofanya ili ushinde unabidi uwe na watu wengi kuliko mwenzio. Lakimi kutimiza hilo wanaruhusiwa kutumia uganga na uchawi kadri wanavyoweza. Sasa hii inafanana sana na namna madhehebu sasa hivi yanavyofanya kazi. Hata kabla sijaokoka nilijua kuna tatizo na baa...