SIKU HIYO JINA LA BWANA LITAKUWA MOJA!

Jina la Bwana libarikiwe; karibu kujifunza Neno la Uzima, Maana ndio Hekima ilipo

Zekaria 14:9
9 Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja.

Kuna vitu vingi vinaendelea katika imani ya Kikiristo mfano; mkanganyiko wa Tafsiri za Maandiko, Mmoja anaamini hivi mwingine vile, na mwingine tofouti na mwingine, Dhehebu moja hadi lingine. Najiuliza, Mungu kweli ni wa ajabu na njia zake hazichunguziki! lakini hali hii ni njia ya Mungu kweli? mbona kama vurugu? Hivi sasa unaweza ukakuta ndani ya kilomita moja makanisa hata matatu, kila mona linajinadi juu ya Mwingine. Hii inafanana sana Ngoma za kwetu usukumani (Bulabuka) hawa hushindana wawili katika eneo kati ya mita 100m hadi 200m, wanachofanya ili ushinde unabidi uwe na watu wengi kuliko mwenzio. Lakimi kutimiza hilo wanaruhusiwa kutumia uganga na uchawi kadri wanavyoweza. Sasa hii inafanana sana na namna madhehebu sasa hivi yanavyofanya kazi. Hata kabla sijaokoka nilijua kuna tatizo na baada ya kuelewa tatizo lenyewe nikawa huru kwa madhehebu, Namshukuru Mungu kwa hilo maana amenitoa huko, Nikaamua kufuata Neno na wala sio Dhehebu! Moja ya mambo ambayo yanakanganya katika Madhehebu ni hili la MUNGU MMOJA KUGAWANYWA VIPANDE VIPANDE. Wengine wanasema ni UTATU MTAKATIFU, wengine wanakataa wakisema haiwezakani bali NAFSI TATU! Hebu tuangalie;

1.Wakatoliki-UTATU MTAKATIFU Kanisa hili lilianza matumizi ya utatu mwaka 325 BK katika baraza la Nikea. Zaidi ya mapadre 300 walikutana kujadili Nafasi ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Waliamua kuuita Utatu. Wakimaanisha Mungu mmoja mwenye nafsi tatu, LAKINI BABA sio Mwana wala Roho mtakatifu na MWANA sio Baba wala Roho mtakatifu, vile vile ROHO MTAKATIGU sio Baba wala Mwana.
Ila wote wana uungu mmoja usiotengana. Bila shaka kwa maelezo hayo machache unaweza kuishia kusema ni MUNGU ASIYELEWEKA! lakini wakati huu ndio ambao unikolai uliingia kanisani na ikumbukwe pia nyakati ya Kanisa la PERGAMO(NDOA) ilianza. Pergamo tafsiri yake ni Ndoa; maana yake ni kwamba UPAGANI uliingia Kanisani na kukubaliwa; na wale ambao walikataa waliuliwa mfano ANTIPA. Kwa hiyo iliwekwa misingi ya imani mbadala. Lakini yote haya Bwana alikuwa ameyasema katika UFUNUO 2:12-17
"12 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili. 13 Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani. 14 Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu(DHEHEBU), yeye aliyemfundisha Balaki(KOSNTANTINI) atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini. 15 Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile. 16 Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu 17 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea."

Sasa.....
Bila shaka utaelewa kwa nini kitabu cha ufunuo kimejaa mafumbo; Ni kwa sababu ili unabii utimie maana Lisingetimia Andiko kama angeliwafumbua macho.
Hata sasa andiko wanalosimamia ni Mwanzo 1:26 ambayo inasema
"26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi."
kwa akili tu ya kawaida hapo hajapambanua alikuwa anaongea na Mungu wenzake ama malaika. Sasa kitu ambacho kipo dhahiri ni kwamba Mbinguni Yupo Mungu na Malaika kwa Sababu Biblia inataja hivo tu.ukisoma Yohana 1:1-3 utaona kuwa hapo alikuwako Neno (wazo la Mungu). kwa hiyo Neno(kigiriki) ni Wazo la Mungu, hivyo Mungu alikuwa Peke yake wakati na hakuitwa Mungu kwa Sababu hakukuwa na wa Kumwita Mungu hadi alipoumba Malaika ndipo akaitwa MUNGU! na baada ya mda mrefu akaumba Binadamu akajulikana kama MUNGU BABA! akamzaa MWANA yaani Yesu ambapo Roho yake MUNGU BABA ilishuka na kuacha mamlaka yake mbinguni na kuuvaa Mwili unaoitwa Yesu kristo.
Yohana 1:14 "14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli."
Kwa hiyo Yesu ni Yule toka Mwanzo maana Yeye anasema ni Mwanzo na Mwisho. alikuwa kabla ya vyote, akaumba na na atatimiliza kazi ya mikono yake. Mwanzo 1:26 na sehemu zingine alizotumia wingi kama mwanzo 3:22; mwanzo 11:7 alikuwa anaongea na Jeshi la Mbinguni yaani MALAIKA siyo Mungu wenzake.

2.Waprotestanti;
Hawa wanasema Mungu ni nafsi tatu; wanakataa UTATU MTAKATIFU: wanakataa lakini tafsiri inakubali; Ndio maana wanabatiza kwa jina Baba na Mwana na Roho mtakatifu kama wale wa UTATU. Hakuna sehemu yoyoye katika biblia walipobatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho mtakatifu. UTASEMA MATHAYO 28:19.
Hebu tusome mathayao 28:19
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;

Hapo sio anabatiza bali ni agizo la namna ya kwenda Kubatiza, Na hapa Yesu alitoa maagizo kwa wanafunzi wake lakini hao hao ambao walikuwa wanasikia na si kusoma maandiko kama sisi; walitoka na kubatiza kwa jina la Yesu Kristo.
soma Matendo 2:38
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Soma pia Matendo 19:5 matendo 10:46-48, Matendo 8:16, warumi 6:3 Sasa NENO LA HEKIMA HAPA NI LIPI???
walikaidi?
hawakuelewa?
walipata Ufunuo wa jina la Baba na Mwana na Roho mtakatifu?
Ama walitaka kumtangaza zaidi Yesu ili awe maarufu?
Tumrejee Petro ili tuelewe vizuri;
mathayo 16:13-18
15 Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?
Mathayo 16:15
16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.
Mathayo 16:16
17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
Mathayo 16:17
18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba(UFUNUO) huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Unaona hapo? ule UFUNUO kutoka kwa Baba uliomjia Petro kujua yule ni Kristo Mwana wa Mungu ndio huo ambao Waliupata Kujua kuwa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu ni YESU KRISTO. Huo Mwamba ndio ule UFUNUO Na wala sio PETRO" Kanisa (SI DHEHEBU) ni moja nalo Halina VYEO VYA BINADAMU kama paroko, Baba paroko, Papa, Baba mchungaji, Nabii mkuu, Mchungaji mkuu n.k.
LAZIMA KANISA LIJENGWE JUU YA UFUNUO.
UTATU wanasema ndio Kanisa lenyewe linalozungumziwa hapo; HAPANA! badala yake ni KAHABA MKUU;Mama wa Makahaba. Yaani UNIKOLAI aliouingiza katika maandiko hata Waprotestanti nao wakaiga baada ya kuanguka (watoto wa kahaba). waliiga yale yale japo si yote.
Ufunuo 17
3 Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi. Ufunuo wa Yohana 17:3
4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake. Ufunuo wa Yohana 17:4
5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI. Ufunuo wa Yohana 17:5
Kumbuka Mwanamke anawakilisha Kanisa, Sasa angalia sifa za hilo Kanisa. Ndugu zangu sisemi kwa Chuki bali Nahubili juu ya Dhambi. Nina upendo na kila Mtu, Nawapenda wakristo na wasio wakristo.
UTATU wanasema wanaweza kufanya chochote maana MAMLAKA YA KUFUNGA NA KUFUNGUA DUNIANI NA MBINGUNI wanayo wao; HAPANA! kama hujui hiyo mamlaka tutaiongelea siku nyingine lakini nikupe Mfano tu jinsi mamlaka hiyo inavyofanya kazi.
Mfano;
wanafunzi walimpigia kura Mathiya (matendo 1:26). Unajua Mungu alimchagua PAULO katika hiyo nafasi?? lakini kwa sababu walikuwa na hiyo mamlaka Mathiya alithibitika mpaka mbinguni kuwa atajaza nafasi ya YUDA ISKARIOTE. Na Mungu bado akamwita Paulo na kuliacha kusudi la Mitume libaki vile. Hawakubadili neno lolote lakini UTATU WANABADILI MPAKA BIBLIA wakisema wanamamlaka hayo; (Hapana, TUBUNI!)

KWA HIYO;
Ubatizo ni kwa jina la Yesu Kristo
ule Mwamba ndio UFUNUO wala sio Petro!
Kama huo Mwamba ni jina la Mtume basi PAULO Ndiye angekuwa huo Mwamba maana Kanisa linalozungumziwa hapo sio LA WAYAHUDI BALI MATAIFA na mjumbe wa kanisa la Kwanza alikuwa PAULO.
THIBITISHO ZAIDI
Zekaria 14:9
9 Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja.
Kwa nini BWANA aseme siku yaja watu wote tujajua jina Lake Moja naye mmoja? Inamaana lazima iwe imejulikana VIBAYA kabla. Watu waseme UTATU yaani wapo WATATU, wengine waseme ni NAFSI TATU wengine waseme jina lake ni YEHOVA SIO YESU (WASABATO) na wengine wakisema ni mmoja wala Yesu sio Mungu.

TATIZO KUBWA NINALOLIONA;
Watu Hawamjui ROHO MTAKATIFU NA UTENDAJI KAZI WAKE. Ndio maana kila anayeandika kumkosoa mwingine utasikia UNAJIANDIKIA TU BILA ROHO MTAKATIFU. Yaani mtu hapa ukisoma post yake unajua kabisa hapa anatetea UDHEHEBU TU sio kiti kingine. Mtu anaamini anaye sio mwingine kisa tu ameelezea kupinga Dhehebu lake haijalishi Yupo sawa kimaandiko kiasi gani; Je, Mbinguni tutaenda kwa sababu ya Dhehebu tulilonalo? HAPANA! kwa hiyo Roho mtakatifu ameeleweka vibaya.
Kama mtu amesoma THEOLOGIA ama shule za wachungaji UNATEGEMEA atamjua Roho saa ngapi maaana Yeye amejaa tafsiri ya Maandiko kutoka Walimu wanadamu. Hata ungempa Ufunuo kiasi gani hawezi kuelewa, anachotaka ni kila kitu kiwe kama alivyofundishwa, mbaya zaidi TAFSIRI walizopewa haziwezi Kukaa katika ukamilifu kwenye Biblia (Wazo la mwanadamu si wazo la Mungu). Sasa hawawezi kukubali ufunuo na tafsiri zao haziwaleti, zinakataa Roho mtakatifu. TUBUNI!
Madhehebu yamemkataa Roho mtakatifu
Manabii wa UONGO wameenea kwa Yule mtoto wa kahaba; hawahubili injili badala yake wanasema OKOKA ILI UPATE UTAJILI, HAWAKEMEI DHAMBI maana wao Bora sadaka kuliko UTAKATIFU(INJILI YAO NI TUMBO). Uasherati, wanawake kuvaa suruali, kupaka rangi nywele, kupaka wanja, kunyoa viduku, usagaji, ulawiti, ushoga, masturbation, nguo zenye kubana, vimini, zote zimehamia makanisani sasa,na wao hawajali. Sasa Dhambi inafugwa badala ya kufukuzwa! hapajakuwepo na wakati wa Dhambi kama huu Na ndio maana Yesu alisema Wakati huu utakuwa kama ulivyokuwa SODOMA NA GOMORA PAMOJA NA WAKATI WA NUHU. Cha ajabu hawaoni hilo wakakemea Dhambi, wanachokiona ni WIMBO WA BARAKA TU MAFANIKIO. Hivi hata hakili ya kawaida unaweza kupambanua mambo haya INAKUAJE WANABII WANAIBUKA KILA KUKICHA wakati ndio wakati wa NEEMA KUFIFIA? Neno lazima litimie. Lazima!
Jihadhali wewe uliye Muumini maana WALIOITWA NI WENGI LAKINI WATEULE NI WACHACHE. Maana yake kwamba kwenda kanizani sio UTEULE bali KUTII NENO LAKE KULIISHI KWA MATENDO.
BILA KUSAHAU HEKIMA IWE ZAIDI YA MATAIFA.
Mungu akubariki na akupe Nguvu kuyaelewa Maandiko kama ipasavyo. Wakati ni sasa, Tubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa Maana mda ni mfupi mno kuliko unavyoweza kufikiri, Tupo kileleni mwa Neema na UNYAKUO upo karibu sana kutokea.
MWANA WA ADAMU AKIJA ATAIKUTA IMANI?
MTAYARISHAJI- Mashibe Elias-0755251999

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NAO WANIABUDU BURE!

NIMEWAPELEKEA TAUNI KAMA YA MISRI (CORONA) LAKINI HAMKUNIRUDIA MIMI

JE! NAWEZA KUWA SAFI NAMI NINA MIZANI YA UDHALIMU!!