NI MAKOSA KUSEMA>USIHUKUMU! WEWE HUBILI INJILI TU, MUNGU NDIYE ANAJUA!
Bwana Yesu asifiwe wapendwa katika Bwana. Kwa upendo wa kristo nawaandikia ili kila mmoja aelewe kabla Mwisho haujafika; Kabla mlango wa Neema haujafungwa.
1 Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.Siku hizi za utawala wa shetani; siku za mwisho, hasa Watu WALIOITWA; Ukiwahubiria wazi juu ya Dhambi walizonazo utasikia USIHUKUMU wewe hubiri tu, hakuna asiyekuwa na Dhambi!
Mathayo 7:1
2 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.
Mathayo 7:2
●ukiwaambia viduku, vimini, suruali za kubana, sketi za kubana, kuweka rangi nywele, kusuka, kuvaa wigi, kupaka wanja, kope bandi, Kucha bandia, kupaka kucha Rangi n.k. Watakuambia USIHUKUMU.
●Wanarejea maandiko kama hapo juu yanavyoeleza kwamba usihukumu usije ukahukumiwa.
●Ajabu ni kwamba wamekuwa ni kama watu waliochanganyikiwa katika dhambi licha ya kwamba wanaingia makanisani na kuomba.
Ndugu yangu katika Bwana; Usiipake manukato dhambi kwa kutumia hili Neno pindi unapobubiliwa injili.
Nini maana ya KUHUKUMU
》Chukulia katika hali ya kawaida kabisa katika mahakama zetu. Mtu anaposhikwa kwa kosa, hupelekwa na kufunguliwa mashitaka mahakamani na Jaji baada ya ushahidi wa kutosha HUMUHUKUMU huyo mtu.
huko ndio KUHUKUMU
》Ebu fikilia, Mtu mmoja alikuwa akimwambia huyu Mtu asiendelee kutenda lile kosa maana akikamatwa atafungwa. Lakini yeye asisikie, mpaka siku asiyoijua yeye akakamatwa na hatimaye akahukumiwa
●Ni yupi aliyemhukumu huyu mwenye kosa?
》Je, Ni yule Mtu alimwonya asiendelee kutenda lile kosa asije akafungwa? Au Yule Jaji?
●Kimsingi Ni Yule Jaji ndie aliyetoa Hukumu. Kwa sababu ya Mamlaka yake.
Sasa,
》Kwa nini wahubili mnatuambia Tunahukumu! Sisi ni kama Yule mtu aliyemwonya yule mwenye kosa kwamba asiendelee vinginevyo atahukumiwa. 》Kama mtu amekwambia HUTASAMEHEWA DHAMBI ZAKO KAMWE, UNGALI BADO UNAISHI Mtu huyu kweli amekuhukumu, jambo ambalo ni makosa kwa mhubili. 》Lakini kama ataongelea juu ya dhambi yako kwa kukupa tahadhali juu ya hiyo dhambi kwamba Utaangamia milele kama usipotubu; HAJAKUHUKUMU! Ila kama utakufa katika dhambi hiyo UTAHUKUMIWA siku ya Hukumu na Jaji ambaye ni YESU KRISTO.
Wengine baadhi husema Hakuna mtu asiyekuwa na dhambi hata wewe unazo, unazitenda kwa kujificha bora mimi nazitenda wazi .
》Ni makosa makubwa kutamka hiyo setensi!
Unajua kwa nini? Bila kujali yule amepoteza mda kiasi gani, ameacha kazi ngapi na ameingia hasara ya sh ngapi kwa huo mda aliokufikia kukuhubilia wewe.
Amebeba Sauti ya Mungu, Akijua kabisa Akikuambia utamtukana na Bado hakuthubutu kukuogopa bali akatamka. Kwa sababu asingefanya hivyo ukifa katika dhambi Damu yako itakuwa juu ya huyo mtumishi.
6 Bali mlinzi akiona upanga unakuja, kama hapigi tarumbeta, wala watu hawakuonywa, na upanga ukaja ukamwondoa mtu awaye yote miongoni mwao; ameondolewa huyo katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwa mlinzi(mhubili) huyo.Umeona andiko hilo? Kwa hiyo usiseme hata yeye ana dhambi; mbali na dhambi unazomzania, Asipokuhubili kuacha dhambi zako, nayo ni Dhambi kwake
Ezekieli 33:6
Ni kweli mhubili kabla hajakuhubilia juu ya Dhambi zako anapaswa awe ametoa kila aina Dhambi kwake kwanza. Yaani Kukuambia Usivae VIMINI wakati yeye kavaa MODO ni makosa, Hajui alisemalo;
3 Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?Japo sikuambii usimtii! Maana hata Yesu aliwaambia Watu wawatii mafarisayo na masadukayo kama walimu wao lakini katika matendo yao Wasiige!!
Mathayo 7:3
2 Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa;Kwa hiyo watumishi hao huwa kama mfano wa mafarisayo na masadukayo. Usishangae kuwaona, lakini pia usiwatukane ila kama ni kuwaonya unaruhusiwa kwa upole na kwa upendo!
Mathayo 23:2
3 basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi.
Mathayo 23:3
●Ni kweli wanadamu wote tuna dhambi! 1yohana 1:8
Hata anayekuhubili analijua hilo; Lakini si DHAMBI ZA MAKUSUDI zinazozungumziwa hapo.
●Dhambi ya Makusudi ni Dhambi unayoitenda kwa kujua na kwa akili zako timamu ukijua ni dhambi tena si kwa kulazimishwa bali kwa tamaa zako tu.
●Kwa hiyo ukisema hata yeye ana dhambi; Ni kweli anayo, hawezi kukosa dhambi hata hiyo ya kukufanya uudhike wakati anakuhubiri nayo ni dhambi, lakini kwa sababu ya dhambi yako hiyo ndiyo uliudhika. Maana laiti kama usingetaka kuikumbatia hiyo dhambi wala Usingeudhika. Kwa hiyo ndio maana Yeye akijua ni nini kikufanyacho uuzike, Hakuogopa kukuudhi! ili tu akuponye na mauti (na huo ndio Upendo kuzidi namna alivyokuudhi kama ungelijua).
HILI NENO USIHUKUMU, WEWE HUBILI TU INJILI. huwa lina maana gani kwenu? Hivi mtu kukuambia uzinzi unaoufanya ni dhambi hajakuhubili??? Au huwa mnamaanisha nini?
Hii ndiyo kusema watu wameiacha injili ya TOBA na kutaka injili ya isiyo na TOBA!
●Watu leo hii injili wanayoijua ni ile Isiyojulikana imetoka wapi! (utafanikiwa, Utakuwa tajiri, Utasafiri nje, utanunua gari, utamiliki nyumba.) yaani ni mwanzo mpaka mwisho hamna Neno la TOBA; Hiyo naona ndio mnataka kila mtu ahubili na ndio maana unapokutana na injili ya TOBA unahisi UNAHUKUMIWA!
Na wahubili wa aina hii ndio mnaowaona wahubili wanaofaa kwenu! Na makristo wa Uongo watakuwa wa kina basi????
Yoyote anayehubili injili ya Toba huchukiwa. Maana walio wengi hawataki kuacha dhambi zao na kuubeba msalaba wa kristo; Bali wanataka mafanikio ili wapate sifa kubwa kwa Watu.
Hawajui injili ni Msalaba.
•Hawajui kuna Ubatizo wa Moto
•Hawajui njia ya Mbinguni ni Nyembamba
•Hawajui kupenda mali ni kufarakana na Bwana 1timotheo 6:10
•Hawajui, Kutotii sheria ya Bwana halafu ukaenda Mbele yake Kumtaka shauri ni Unajiangamiza mwenyewe. Ezekieli 14:1-10.
Kwa hiyo huyu mtu anayesema Usihukumu bila kujua maana ya kuhukumu na Kumtaka mhubili ahubiri injili tu. Hajui alisemalo. Maana wakati huo anasema hivyo Anaikataa injili. Yule mtu akikung'uta miguu na kuondoka itakuwa kilio na Kusaga meno!
•Maana umemkataa Roho mtakatifu aliyekuja kwa njia ya Huyu mtu, ukadhani ni huyu mtu anajidai kuwa mtakatifu kupita wengine. Usitambue kwamba yeye mwenyewe anatimiza wajibu kuufikia utakatifu. Bwana wetu Yesu alisema Mti usipozaa matunda hukatwa na kutupwa nje.
•Kwa hiyo hapa si yeye tu hata wewe baada ya kuipokea injili umekuwa mwanafunzi na mti katika kristo ili watu wavune kutoka kwako. •Sasa, Kama hayo unayoambiwa uyaache na hutaki bali unataka asiendelee kukuonya ukidhani anakuhukumu; Siku utakuja kutoa hesabu yake. Na matunda yako yatakuja hapo maana utakuwa umepoteza wengi kwa tabia zako kama mfano wa mtu aliyeokoka.
•Utakuwa umewazuia wadogo katika Yesu (wachanga wa kiroho) kumjua na Kumtii wakienenda kwa kukuiga uchafu wako wakijua Si dhambi.Utafungiwa jiwe la kusagia na kutupwa baharini.
Wapendwa wakati ni mchache mno tuliobakiwa nao. Moja ya siku hizi Unyakuo utatokea; Na kama bado utaendekea kukataa injili ya Toba kwa kisingizio Wanakuhukumu, Hukumu inakuja na wakati si kama huu Ukiwa na kiburi cha Uzima. wakati huo Huna hata nafasi ya kupiga magoti na Kuomba.
Biblia inasema
14 Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.Usijidanganye na injili ya Mafanikio, Utaishia kuitwa na kuhudhuria kanisani tu na Moto utakuwa sehemu yako.
Mathayo 22:14
Hakuna filamu hata moja ya kutishwa inayoweza kufananishwa na Kuzimu ilivyo.
Ni mahali pa mateso na pa kutisha mno. Duniani utateseka na utakufa. KULE KUZIMU HUFI na mateso yake hayajatokea mfano wake hapa duniani.
Fanya imara kuitwa kwako na kuimarisha uteule wako
Bila utakatifu huwezi kuuona ufalme wa mbinguni.
11 Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.Soma vizuri mstari wa 11.
Waebrania 12:11
12 Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza,
Waebrania 12:12
13 mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe.
Waebrania 12:13
14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
Waebrania 12:14
Ubarikiwe!



Maoni
Chapisha Maoni
Tafadhali, share kwa wengine ili kuisambaza injili kwa watu wote na Mungu wa mbinguni atakubariki.
Unaweza kutumia namba hii 0755251999 kuwasiliana kwa njia ya whatsapp