MANABII NA MAKRISTO WA UONGO
Hizi ni siku za mwisho, tena tupo karibu sana na UNYAKUO ambao kimsingi itafuata Dhiki kuu baada ya huo kwa miaka saba. Ndani ya miaka saba hasira za Bwana zitawaka na ulimwengu utashuhudia mapigo ya ghadhabu ya Mwana kondoo.
Sasa kwa nini ghadhabu hiyo inapaswa ije kama Yeye mwenyewe alisema Injili itahubiriwa kila mahali?
Jiulize tu!
Hapajakuwapo na makanisa mengi wakati wowote kama siku hizi za mwisho;
Hapajashudiwa kuwa manabii wengi kama kipindi hiki; lakini ajabu ni kwamba ndio kizazi kitakachoiona ghadhabu ya Mungu!
mapigo ya Ufunuo 16 yatatimizwa lakini Bibi harusi wa kristo atakuwa amenyakuliwa tayari.
Siku ya Bwana ni giza mpendwa:
"18 Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya Bwana; kwani kuitamani siku ya Bwana? Ni giza, wala si nuru.
Amosi 5:18
19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma.
Amosi 5:19
20 Je! Siku ya Bwana haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga.
Amosi 5:20
Hiyo siku ni mapitilizo ya Dhambi. Sasa,kama kila kitu kipo kwenye mstari, tunao Manabii mashuhuri, tunayo makanisa makubwa na Mengi kuliko wakati wowote, Injili imehubiriwa kila mahari;
Ebu sikiliza hapa Anasema nini
21 Mimi nazichukia sikukuu zenu, nazidharau, nami sitapendezwa na makutano yenu ya dini.
Amosi 5:21
Bwana anasema makutano yetu ya dini hayampendezi!
Kwa nini?
Kwa sababu Kweli ya Mungu tumeiacha na kuhubili mapenzi ya Mwanadamu.
Mwanadamu anataka utajiri, fasheni, Starehe, umaarufu, michezo, Maisha mazuri, Baraka. n.k Mambo ambayo Yesu aliyakataa na kusema kama hutajikana kwayo HUMFAI!
Leo wanaojiita manabii mambo hayo ndio injili yao ya kila siku kana kwamba kristo alikufa kwa ajiri tuwe matajiri hapa duniani.Hatukuokolewa kutoka kwenye imasikini, bali kwenye dhambi.Na Neno la Mungu peke ndio ninalowez kututoa huko.
Bila kufikilia Yeye mwenye aliishi katika dhiki mpaka anaondoka; Je, hakusema mimi ndiye njia? Au hamjui majaribu aliyoyapitia kila Mwamini atapitia?
Au je! Mitume walienda kila sehemu wakiwaombea watu kuwa matajiri? na kuwahubili shida na kuponya basi? Kwa nini Basi wapigwe Mawe kama ndio hivyo?
Hawakuhubili injili yoyote ya kiponya kimwili bali kiroho; waliponya kimwili kuwafanya watu waamini kazi ya Mungu. mNa hata leo Uponyaji sio dhambi lakini bila Neno la Mungu ndani yake ni bure.
UNABII UNASEMA
"24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule."
Mathayo 24:24
Hawa Manabii na Makristo wa Uongo ndio hawa tulionao leo hii. KUMBUKA! ni manabii sio Nabii mmjoa, mkrisro(wamebeba jina la kristo na kudanganya watu)
watadanganya hadi wale walio kusudiwa Uzima toka kuwekwa misingi ya Ulimwengu.
Mababii hawa wanapotosha sio kwa uganga bali kwa kuipotosha kweli
Mfano,wanakuambia;
Mungu haangalii mavazi anaangali rohoni
una laana njoo upake mafta utafakiwa
Ulipe fedha ili ufanyiwe maombi (uganga)
kila siku wanataka upokee muujiza. Je unataishi kwa Miujiza au kila Neno la Bwana?
wanapenda kusifiwa na watu.
" 26 Ole wenu ninyi watu wote watakapowasifu, kwa kuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mambo kama hayo.
Luka 6:26"
Wanamjaribu Mungu kwa kuwanywesha tindikali bila sababu ya msingi.
Wanawazuia watu wasioe
wanawapendelea watu matajiri kanisani
Kuombea safari za nje
kuhubili chuki kwa watu yaani wanawaambia watu wanowahubilia kuwa kuna watu hawawapendi na kuwachukia ndio maana hawafanikiwi!!! kwa hiyo hawa watu utawakita wakiomba maombi kama hayo hayo ya kuwachukia majirani kwa sababu wanamfanya asifanikiwe. Tena wanakemea kabisa. Je! huyo ni Mungu gani, Leo aseme mpende jirani yako kama nafsi yako kesho amlaani jirani yako kwa sababu umemwomba!
Injili ya kweli ya wokovu haipo tena,
Leo nguo za kwenye Madanguro ndio fasheni kanisani.
Kupaka rangi kanisani, Kunyoa viduku, uasherati, kuangalia video za ngono, kufanya masterbation, kusuka nywele, Kuvaa mawigi, Nyimbo za kidunia, kuchora tatoo, Kupata rangi uso kama yezebeeli n.k. vyote hizi Watu wanaojiita wakristo wa madhehebu haya wanavifanya na wakiwa makanisani, Injili yao ni kukemea pepo na utajiri basi.
Matunda ya hawa mababii yanaonekana dhahiri hata kwenye mitandandao, Mtu ukimwambia injili ya kweli na kumkosoa udhehebu wake hachelewi kurusha tusi. Wao dhehebu ni kama Yesu kwao, Bora useme lolote juu ya Yesu lakini sio Dhehebu lake wakati Maandiko yako wazi.
UDHEHEBU NI DHAMBI
"12 Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo.
1 Wakorintho 1:12
13 Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?
1 Wakorintho 1:13"
Kama haupo kuubeba Msabala wako Nguvu ya upotevu kutoka Kwa Mungu itakupekeleka kuzimu.Amesema ujikane kama alivyojikana katika mambo ya dunia hii.
HAWA MANABII NA MAKRISTO WA UONGO WAPO WA NAMNA ZOTE
wainjilisti, wachungaji n.k yaani katika karama zote tano wapo waongo wakitumia hizo karama kuipotosha kweli
1 Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia.
" 2 Petro 2:1
2 Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa.
2 Petro 2:2
3 Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii.
2 Petro 2:3"
unaona? ni watu amabao katika kutamani watajipatia faida kwenu.
Hawawezi kuhubiri kweli kwa sababu wanaogopa matajiri watawakimbia; wanajua watu wazulumaji ndio wenye mali na wao hawapendi kweli bali Neno la falaja, Kama "utanunu gari, utasafiri nje,utabarikiwa mpaka watu watashangaa"
Nawaambia iliyo kweli ya Bwana; Sehemu yao ni lile ziwa la Moto.
KWA NINI MUNGU AMEWARUHUSU?
Injili inasema liache Gugu limee pamoja na Ngano. wakati wa mavuno ndipo magugu yatakusanywa pamoja na kuchomwa moto. huko kutakiwa na kulia na kusaga meno.
Lakini pia, Mungu ameruhusu kuwajaribu wenye mwili kama wanampenda na kushika amri zake
" 3 wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote.
Kumbukumbu la Torati 13:3"
Ndugu zangu ufalme wa Mungu u karibu, Moja ya siku hizi Unyakuo utafanyika, Njoo kwa Bwana watu wake. Muikane dunia na mambo yake. Yakimbieni madhehebu na manabii wa Uongo;
maana Bwana awapima kupenda kwenu!
Alisema siku za mwisho mtapunguza kumpenda, Na leo ushuhuda tosha wa Waumini wa leo.
Tubu leo kwa kumaanisha kuziacha dhambi zako zote kabisa na Roho mtakatifu atakuongoza katika kweli. Ukatie bidii kuutafta ufalme wa mbinguni. HUTAJUA BIBLIA IMEGOSHIWA WAPI KAMA BADO UPO HUKO.
Maoni
Chapisha Maoni
Tafadhali, share kwa wengine ili kuisambaza injili kwa watu wote na Mungu wa mbinguni atakubariki.
Unaweza kutumia namba hii 0755251999 kuwasiliana kwa njia ya whatsapp