USHUHUDA WA ALIYEKUWA KUHANI WA KANISA KATOLIKI

USHUHUDA WA MIGUEL VASQUEZ KUTOKA MJI WA MATAGALPA, NIKARAGUA.

ASKOFU WA ZAMANI WA KANISA KATOLIKI ANYAKULIWA KWENDA MBINGUNI NA KUZIMU


Mwaka 2003
Mimi ni Askofu wa kanisa la kiinjilist la Watoto wa Imani. Kabla sijawa Mkristo, nilikuwa Padre wa kanisa la Katoliki ya Kirumi. Nilisherehekea sakramenti 7 kama vile Ubatizo wa kikatoriki, Uthibitisho, Ekaristi, Kitubio, kupaka mafta mgonjwa, ndoa za kikatoliki, na Amri takatifu. Nilibatiza watoto wadogo waliozaliwa na nilipenda picha. Nilitumia maji matakatifu, mshumaa, chumvi, nguo iliyopakwa mafta na vitu vitakatifu. Nilivaa kasula na vazi lililotiwa wakfu. Nilikuwa na uaskofu wa kufundisha na nilimwabudu Maria. Kwangu mimi, alikuwa Mama wa Mungu, Mama wa kanisa, Mpatanishi, malkia wa mbinguni, mwombezi na dhana kamili kabisa. Nilijitolea kwa Maria na kuweka wakfu kila kitu kwake na niliomba sala zote kwake. Kwangu mimi, alikuwa mponyaji, Bikra daima na Mungu mke.

Rafiki yangu wa ujana Carlos kutoka kanisa la pentekoste la kuzaliwa mara ya pili aliniambia kuhusu kuabudu sanamu na mafundisho ya sharti ya kanisa katoliki. Alinihakikishia katika Biblia kwamba kila kitu nilichojifunza hakina msingi wa Biblia. Nilianza kufa moyo kuendelea kuwa askofu. Nilikuwa nimejiingiza kwenye Uasherati kwa sababu ya kiti cha Uaskofu ambacho kinazuia ndoa. Sikuwa na matumaini yoyote ya kuoa na kuwa na watoto ili kuwa na familia. Kaka Carlos amenihakikishia kabisa ndoa inaruhusiwa kisheria kwa wachungaji. Nilijiingiza kwenye uasherati na mwanamke aitwae Belita wakati nikiwa Padre. Leo ni mke wangu. Nilianza kuficha uhusiano huu wa mapenzi kwa maaskofu na maaskofu wakuu. Sikutaka kuharibu sifa yangu. Hatimaye, nilichoka kuficha siri hii na kuamua kuvua kasula na nikaenda kuishi na mke wangu Belita. Nilimuoa na kwenda kujumuika na kanisa la kiinjilisti ambalo halizuii ndoa kwa viongozi. Niligundua kwamba nilikuwa nikiishi kwenye udanganyifu wa kanisa katoliki


Kwangu mimi, Yesu Kristo hakuwa na nguvu sana ya kuokoa nafsi. Siku zote nilimwamini Maria kuniombea katika kukombolewa kwangu. Na nilizidi kuwaomba malaika wote waniombee nikombolewe kutoka katika Jehanamu. Wakati nilipomwomba Yesu kuniponya, nilifanya maombi mengi kwa malaika wote. Niligundua udanganyifu wote wa mafundisho haya, ambayo nilikuwa nimeelekezwa. Nilienda kutubu na nilifanya hivyo katika usiku mzima katika maombi.

UZUSHI
Malaika alinitokea na kunishangaza kwa ule utukufu wake. Niliduwaa nikitazama tu ule utukufu ambao ulitoka kwake. Malaika akasema, “Hii ni itikadi katika usitawi wa kiroho kuwadanganya wateule katika hizi siku za mwisho. Hapajakuwepo na Madhehebu na Makanisa ya Uongo mengi kama mliyonayo katika siku hizi za mwisho. Mambo yanazidi kuwa mabaya na shetani amepata nafsi nyingi kwa kutumia mbinu potofu za kiakili. Amepandikiza uongo kupitia kwenye madhehebu, falsafa, sinema, injili za uongo, riwaya, michoro na kila aina ya miziki. Vyote hivi vimefanya udanganyifu katika akili ya mwanadamu na kuindoa imani katika injili ya kweli. Watumishi wa shetani wamekuwa wakisema kwamba Yesu ni mtu wa kudhaniwa na wala hayupo. Hawajaipa thamani nguvu ya ukombozi katika Maandiko. Wanasema Biblia ni kitabu cha historia tu, kinachofanya imani ya watu isifanye kazi. Kinachofanya Neno litofautiane na kitabu kingine ni Imani katika Maandiko. Imani ya maisha ni Neno ambalo litaleta maisha ya uzima wa milele kwa wale ambao wanaamini. Shetani anajua nguvu ya Neno katika kuponya na kuokoa. Anatumia falsafa yake ya mgawanyiko kuondoa maandiko ili ateke umakini wa watu kutoka kwenye Neno la Mungu.
Yesu ametuma ujumbe kwako. Anataka ufungue huduma na uwalete wote wakatoliki uliokuwa unawafundisha wakati ulipokuwa Padre. Bado wanakuamini, japokuwa umekuwa Mkristo. Malaika alipotea na akaondoka siku hiyo. Malengo yangu ya kufungua kanisa yalianza mara moja. Nilipoapisha kanisa langu na kualika wakatoliki wote, nilijishindia asilimia 70 ya watu ambao walikuja kujiunga nami wakati nilipokuwa padre. Na sasa nilifundisha Neno halisi na kuwabadilisha wakatoliki kuwa waamini. Nao sasa wakawa wafanyakazi katika zizi la kondoo. Baada ya kumwona Malaika imani yangu iliongezeka. Nikajua sikuwa peke yangu na kwamba viumbe vya mbinguni viko dhahiri kuliko mwili wangu. Sasa nikapata sababu ya kushindana na shetani. Sikuogopa tena matukano na mateso. Nilikuwa naomba bila kukoma katika milima na ilikuwa tayari usiku umekwenda. Nilianza kuhisi kama upako wa nguvu ya umeme . Kitu cha ajabu kikaanza kutokea katika ule mlima. Roho mtakatifu akachukua mdomo wangu na kuanza kuongea katika lugha ya Rohoni. Sikuweza kujizuia kuongea. Nikachukuliwa katika nguvu kubwa. Na mti ukaanza kuwaka moto na ukaungua katika moto, lakini haukuteketea katika ule mlima. Mti ulibaki bila kuharibiwa. Mwili wangu ulikufa ganzi na sikujaribu kuzuia nguvu ya Mungu iliyonichukua Roho yangu. Nilianguka chini na Yesu akanitokea katika ule mlima. Alikuwa anang’aa mno, ningeweza kumwona Yesu kwa shida sana. Hiyo ilikuwa ni halisi, Roho yangu ilikuwa mbele ya uwepo wa Yesu. Nilimwona hakika, ukijumlisha na mwili wangu ulikuwa umelala pale chini. Yesu akaniita kwenda sehemu. Nilikuwa na furaha na nilidhani ingekuwa ni mbinguni.


KUZIMU
Alianza kutembea na mimi kuelekea shimo refu. Na jinsi tulivyozidi kutembea kuelekea chini, ndivyo giza lilivyozidi kuongezeka. Tulipofika chini, nilihisi harufu mbaya ya uvundo wa nyama zilizooza. Nikaogopa kuona mapepo yanakula nyama za watu. Walikula kwa kuchota ubongo na viungo vya ndani. Walifanya ukatili kwa zile roho wakikwanyua mikono, miguu, na kichwa kujilisha wao wenyewe. Na ule uvundo mbaya wa wafu ulitapakaa sehemu ile.

UVUNDO WA DHAMBI
Nilimuuliza Yesu ambaye alikuwa karibu yangu, sababu ya ule uvundo mbaya kama hazikuwa nyama, lakini roho zilizopotea. Yesu akasema hizo ndizo dhambi walizobeba. Dhambi inanuka kuzimu kama roho yako haikusafishwa kwa Damu ya Yesu. Wakati watu wakifika kuzimu minyoo huanza kutoka katika roho zao. Roho chafu inachipua minyoo ambayo inasababisha uozo na uvundo. Roho ikishafika kuzimu huchanjuliwa kama nyama na muuza nyama. Kuzimu, vitu viko halisi kama hapa duniani. Huko roho hutoa damu na ina mifupa. Kuzimu ni sehemu halisi sawa na hapa duniani. Kila aina ya vifo, vurugu, umwagaji damu na umalaya juu ya uso wa dunia pia vinatokea kuzimu. Dunia ni sehemu tu ya kivuli ya uovu ambao unatokea kuzimu.


ZINAA ILIYO KUZIMU
Mapepo hubaka zile roho na kuzivunja. Yanatumia nguvu kuzilazimisha zile roho kufanya zinaa kwa nguvu. Roho zinateswa kupitia sehemu za siri. Kila kitu unachokifanya duniani kitaendelea kufanyika kuzimu. Hivyo kilichopandwa katika maisha kitakusanywa katika umilele.


MAUAJI
Muuaji anaweza kuua watu 100 duniani. Hataweza kulipa kwa ajili ya maisha ya wale watu hapa duniani. Hata kama atakamatwa, sheria ya mwanadamu haitoshi kuchukua uovu wa matendo yake. Lakini atakapokufa, katika umilele sheria ya Rohoni itatumika katika roho yake katika haki. Sheria ya mwanadamu duniani hamna haki, lakini sheria ya Mungu ni moto ulao katika hasira ya Mungu. Tukiwa kuzimu alikuja mwanamme mmoja ambaye aliua zaidi ya watu 20. Hakuwahi kukamatwa kwa sababu haki katika dunia haikuweza kufumbua uhalifu ili kuweza kumkamata huyu mtu. Alikufa akiwa na deni katika haki, lakini hawezi kukwepa moto wa kuzimu. Moto ulichochea wakati unamchoma huyu mtu. Sehemu ambayo huyu mtu alikuwa ametengwa ikawa ziwa la moto.


WANYAMA WALIO KUZIMU
Giza la hii sehemu ni tororo. Hali ya hewa si rafiki, hakuna oksijeni huko. Hakuna maisha, hamna miti, hamna nyasi. Hamna maji na hamna upepo unaovuma. Wanyama niliowaona kuzimu ni wa ajabu na wanakula watu. Watu hawafi japokuwa wanateswa na hawa wanyama wasio wa kawaida. Wadudu wengi wala nyama walikula nyama za watu. Wadudu wa kutisha kama kombamwiko walikula zile roho. Wanaingia kila mahali pa mwili. Hawa wadudu wanajipenyeza kupitia nyama na kuingia mwilini. Wengine wanaingia kupitia mdomo, pua, masikio, na macho. Wale wakorofi zaidi walitoboa tumbo, mgongo na fuvu kuingia. Minyoo ile ilipenyeza katika sehemu za ndani za watu na kuzitafna sehemu zile tokea ndani hadi nje mpaka inaifikia ngozi. Minyoo ilikuwa haitosheki na ndani ya dakika chache roho ililiwa na kubaki mifupa mitupu. Nyoka wenye sumu waling’ata watu na kutema sumu katika mawindo yao. Hawa nyoka waliziadhibu zile roho kwa ming’ato mbalimbali, waliwaadhibu zile roho kwa kufanya dhambi za kuasi walipokuwa hai duniani. Anaconda walijeruhi miili ya zile roho na kuzivunja vunja. Niliweza kusikia sauti ya mifupa ikivunjika.


PAGATORI
Nilipokuwa mkatoliki, niliamini pagatori ni mahali roho za watu husafishwa. Lakini, sasa najua pagatori haipo. Amkeni watu wa katoliki, msimpe shetani nafasi ya kuwadanganya. Usiweke tumaini la kufa na kwenda pagatori kupata nafasi ya pili. Unadhani utaenda pagatori na halafu uende mbinguni. Hakuna nafasi ya pili kama utakufa katika dhambi zako. Unaenda kuzimu moja kwa moja bila kupitia pagatori. Na ukiangukia huko utakuwa umechelewa tayari. Hakuna namna ya kutoka huko. Mlango wa kuzimu umefungwa. Mlango wa kuzimu upo wazi kupokea roho na kila kitu kimefungiwa kiasi kwamba hakuna anayeweza kutoroka. Roho haziwezi kukwepa mateso. Kama hutaniamini mimi na kuamua kuishi katika dhambi, siku moja atakufa na atakumbuka huu ushuhuda. Hupaswi kujutia kama ukiingia huko. Mateso yote haya niliyoyaona huko kuzimu, kama utaenda huko utaona kila kitu nilichokiona. Lakini utakuwa umechelewa sana. Mapepo yatakutosa kwenye moto kama jinsi ambavyo unavyotosa jiwe ziwani.


IBADA YA SANAMU YA KATORIKI
Niliona kuzimu wamsujudio Maria na malaika wa kikatoliki. Waumini wa mtakatifu Petro, mtakatifu Paulo, mtakatifu Yohana na malaika wengine pale. Nimeona mapadre, makuhani na makuhani wakuu wa kikatoliki kuzimu. Niliona ma-sista, mama katika kanisa katoliki, vijana wa kwenye madhabahu na mapapa katika kuzimu. Mapepo yaliwatesa hawa roho kwa kuwachoma na mikuki. Pia walitobolewa kwa kutumia kwata wakitengenezewa mashimo katika miili yao.


MATESO
Mapepo yalitumia visu kukata na kuchana zile roho. Niliona kipindi pepo lilipata mashine ya kusagia nyama na kuweka zile roho ndani ya ile mashine. Zile roho zilipotoka kwenye ile mashine, zilionekana kama nyama zilizosagwa. Upande mwingine wa kuzimu, mapepo yalikuwa na misumeno. Walizikata zile roho vipande vipande. Hapa duniani, hamna hata filamu ya kutisha kulinganisha na yale mateso.


MASHOGA NA WALIOBADILISHA JINSIA
Niliona pia mapepo yakitengeneza madangulo na sehemu za starehe za kuzimu pamoja na zile roho. Waliwabaka Malaya wanaofanya wanaofanya ngono kinyume na maumbile na waliobadili jinsia. Ndani ya dakika chache, ziwa la moto lenye minyoo lilikuja kama tsunami na kufunika sehemu yote. Wimbi la ndimi za moto likachukua ile sehemu na kusababisha harufu ya ajabu ya nyama zilizochomwa. Machozi yalitoka katika macho ya Yesu. Hafurahii kuona mateso ya zile roho. Watu waliochagua njia zao, wakimsahau Yule ambaye hutoa maisha ya uzima wa milele. Ni ngumu kwa Yesu kuona hayo mateso. Alinipeleka tu kuzimu kunionesha hali ilivyo kwa zile roho ili kwamba niiambie dunia na kuzuia roho zaidi kupotea. Ile sehemu hutoa harufu ya kifo na hofu. Ni sehemu ya kupiga makelele, manong’ono, kutoa jacho, damu, machozi, kusaga meno na mateso yote ya kila aina.


WATU MAARUFU
Na kisha Yesu akanichukua sehemu nyingine huko kuzimu. Bango kubwa liliandikwa KARIBU WATU MAARUFU NA POKEENI MAPOKEZI MAKUBWA. Nilipoingia katika mlango wa lile bango, niliona waimbaji, waigizaji, na watu maarufu wengi pale. Niliwatambua wanamziki 2 wa mziki wa rock na mwigizaji wa kike. Nilimwona mwanamziki wa mziki wa rock Bill Haley akijirusha rusha kwa nguvu kwa sababu ya ndimi za moto zilizomchoma. Mpiga gitaa Jimmy Hendrix alikuwa analia katika maumivu, alihisi kiu sana na njaa katika ile sehemu. Mapepo yalimfanya acheze gitaa la moto mpaka vidole vyake vilipo mong’onyoka. Wanamziki wengi wa mziki wa rock waabudu shetani ambao walifanya maagano sasa wanateswa na mapepo. Nilimwona mwigizaji wa kike Thuy Trang ambaye alishiriki katika filamu ya Power rangers series. Alipomwona Yesu alianza kulia atolewe mle ndani. Watu wote hawa maarufu wapo kuzimu kwa sababu ya umaarufu na pesa. Maagano waliyofanya na shetani yaliwapeleka katika sehemu hii. Ni huzuni kuona waigizaji wengi wa kiume na wa kike na watengeneza filamu katika sehemu ile. Wengi katika hawa watu maarufu sikuwajua. Njia ya wote wanopenda kutambulika na kupenda pesa ni kuzimu. Wamekufa duniani na kusahaulika, lakini kuzimu wanaishi. Wanateseka mateso mengi mbalimbali. Ni huzuni kuona sura za kutisha nyusoni mwao. Hakuna kitu cha kutisha duniani kama hii sehemu. Eneo la utesaji wa hizi roho ni la kutisha. Niliona kwa macho yangu filamu ya kutisha iliyo ya kweli. Yesu alinichukua kutoka kuzimu na tukapanda duniani wote. Nilipokuwa padre nilikuwa na mahusiano na mke wangu. Bado tulikuwa hatujaweka kiapo kwa sababu nilikuwa padre. Mtoto wangu Jorge alizaliwa wakati ule. Nilikuwa nikificha hii siri kwa maaskofu kwa miaka miwili. Nilipokuja kuwa mkristo, nilimwoa mke wangu na tukajumuika kanisani. Nililea familia na nikapata mtoto mwingine wa kike jina lake Clare. Alizaliwa wakati mtoto wangu wa kiume Carlos akiwa na miaka 11.


MAUAJI
Mtoto wangu alipotimiza miaka 15 nilimnunulia zawadi ya saa. Alinisaidia sana katika kazi na alikuwa motto wangu wa kiume pekee. Nilikuwa tayari nimeanzisha Huduma na Carlos alinisaidia wakati wote akiwa karibu nami. Siku moja akiwa anatoka shule alikabwa. Mtu aliyemkaba Carlos alimpiga risasi ya kifuani na kupora saa ya mtoto wangu. Alikufa wakati huo huo, nilihisi maumivu makali sana kwa kifo cha Carlos.
Mapepo yalikasilika sana kwamba nilienda kuzimu na kushuhudia kile nilichokiona. Walijaribu kunifikia kwa kuzuru nilichokipenda sana-mke wangu na watoto wangu. Lakini nilisimama imara, sikumnung’unikia Mungu. Kwa sababu anawapa maisha wale wanaomtumikia kwa moyo. Hachukui maisha ya kijana ambaye alijtolea katika kazi yake. Shetani alikuja kuua, kupora na kuharibu.
Mwaka mmoja na miezi kadhaa baadae, niligundua ni nani alikuwa muuaji wa mtoto wangu. Nilimwendea kujifunza sababu iliyompelekea kuua. Hakufahamu kama nilikuwa baba yake na Carlos. Huyu bwana mdogo alikuwa anaitwa osca. Ni maskini mno na alitaka saa ya mtoto wangu kwenda kuuza. Nilielewa hitaji lake la kuiba saa ya Carlos, lakini sikuridhika kunipora hazina yangu ya thamani kutoka kwangu. Bwana mdogo osca alikuwa na miaka 20. Nilitaka nimpeleke kwenye vyombo vya dola, lakini sikuwa na ushahidi wa uhakika kumshitaki. Bwana mdogo hakujua sababu iliyonifanya nimwendee. Alinichukulia kama rafiki yake.
Roho mtakatifu aliniambia, Hubiri Neno kwake. Nilipinga sauti yake na kuuliza maswali katika sala yangu. Nilisema, “ni muuaji wa mtoto wangu ambaye nilimpenda. Yeye hana cha ziada kutofautisha na wauaji wengine nimewaona kuzimu na anastahili mwisho wa safari sawa na wale.”
Nilienda kitandani na malaika akanitokea. Alinyosha mkono wake uelekeo wangu katika urefu wa pua. Alivuta roho yangu kupitia matundu yake ya pua. Roho yangu ikakaa na malaika. Alienda na mimi mawinguni. Malaika akanionyesha sayari, dunia ilikuwa inatetema katika mzunguko wake na kujizungusha kwa mwendokasi mkubwa sana na mseleleko wa kasi. Malaika akasema, “mtetemo na mzunguko wa dunia unazidi kuongezeka kwa haraka sana. Siku za dunia zimefupishwa, miaka itaenda kwa haraka.


DHIKU KUU
Malaika akanionyesha siku za dhiki kuu, mtu mkubwa wa kidini sana akatoa kafara kwa shetani kuachilia mapepo. Shetani akapokea nguvu na kufungua shimo la kuzimu. Jeshi la mapepo likavamia dunia na kutoa hukumu juu ya dhambi. Watu wakawa vichaa, wenye kuyumba, kukandamizwa, na kumilikiwa na mapepo. Walikuwa na vidonda visivyoweza kuponywa vikastawi mahali pote. Kulikuwa na ugonjwa wa kuua wenye kutisha ambao haukuua watu. Hawa watu walichukua umbo mithili ya mazombi na kupata shida ya kujimudu kiakili; walikuwa watumwa wa serikali.
Nilitazama katika mto efrati, malaika 4 waliachiliwa na kuharibu sehemu kubwa ya idadi ya watu duniani katika vita, magonjwa na njaa. Na kutokana na hizi mamlaka, mamilioni ya wanajeshi kutoka kuzimu yaliachiliwa kuharibu wanadamu. Watu wote na wayahudi ambao hawakuwa na muhuri wa Mungu waliangamizwa. Vikosi vya kuzimu viliiandama dunia na kusababisha uhalibifu. Wanadamu waliokuwa wanamilikiwa na mapepo wakawa mashine za kuua. Silaha za nyukilia zilirushwa katika dunia na kusababisha uharibifu mkubwa. Mamilioni ya watu na wayahudi waliuwa katika uso wa dunia. Wale waliokuwa na ile alama katika nyuso zao waliwasulubisha wakristo.
Gadhabu ya Mungu imeshuka kutoka mbinguni juu ya wezi, wachawi, wauaji na Malaya. Wafalme na mpinga kristo hawakuweza kuongoza, kote ni machafuko na uharibifu.


KANISA LA KIINJILISTI
Malaika akanionyesha majina ya madhehebu yanayofanya huduma ya wokovu. Baadhi ya makanisa yalifikia asilimia 50 ya watu waliokolewa, wakati mengine yalifikia asilimia 40 na asilimia 30. Makanisa ambayo hayakujitolea sawasawa yalifikia asilimia 20 na asilimia 10. Wakati makanisa yenye rushwa yalifikia asilimia 5 na asilimia 2. Makanisa madogo na yasiyojulikana yalifikia asilimia kubwa ya wokovu. Na makanisa makubwa yalifikia asilimia ndogo zaidi ya wokovu.
Malaika akasema, “Jinsi watu wanavyozidi kuongezeka makanisani, ndivyo wanavyokua kifedha na ndivyo wanavyokuwa na hofu ya kuhubili injili ya wokovu.”


MBINGUNI
Mimi na malaika tukaingia Paradiso. Ni pazuri, eneo lenye ustawi likiwa na Majumba mazuri kwa kanisa kuishi ndani yake. Yote yalikuwa ya dhahabu yenye utukufu mkubwa ambayo hung’aa kama jua katika ile sehemu. Malaika akanyosha kidole chake katika umati wa watu. Akasema, mtazame mtoto wako Carlos.” Niliangalia na kuona kwamba wote walikuwa wanafanana. Malaika akafungua macho yangu ya rohoni na nikamtambua mtoto wangu. Alikuwa tofauti, mwenye furaha kubwa. Malaika akaniruhusu kukutana na mtoto wangu. Nilimpa busu murua na kusema “nakupenda.” Busu ambalo hajawahi kupewa wakati akiwa duniani. Nilimshindia mtoto wangu kwa kumpitisha njia takatifu. Sikutaka kunyoosha mkono wangu juu ya kichwa chake kwa hofu ya kupoteza katika dunia. Busu katika fikra zangu lingekufanya uburudike. Nilikosa kumpa mtoto wangu upendo zaidi. Mbaya zaidi ni kwamba wengi hukumbuka kuwapenda wakati wakiwapoteza wanaowapenda. Ipende familia yako, wapende watoto wako, wapende wazazi wako na wazazi wa wazazi wako wakati wakiwa bado hai. Wakifa, hamna maana yoyote kujuta kwa kile walichokifanya.


KITABU CHENYE MAAJABU
Nimeona kitabu cha dhahabu kimejaa siri za ajabu zilizofichwa ambazo bado hazijafunuliwa. Malaika akasema Biblia ni muhimu sana kumkomboa mwanadamu, lakini sio ajabu zote za Mungu zimewekwa kwenye Biblia. Kuna vitabu mbinguni vimeandikwa vitu ambavyo viko nje ya uwezo wetu wa kufikiri.


HATIMA
Kabla hatujazaliwa, Yesu alikuwa amechora njia kwa kila mtumishi mwaminifu. Yesu hajaweka siri zako zote kwenye Biblia ili kwamba tutakuja kwa Mungu na kuomba tutakuwa na ufunuo.
Malaika akasema, “kijana osca ambaye alimuua mtoto wako ni mteule kwa kazi kubwa. Shetani alikuwa anajaribu kuchukua roho yake.” Malaika akanifunulia kwamba kupitia yeye watu wengi wataokolewa.
Malaika akasema, “kama hutamhubiria injili, hakuna mtu atasema naye. Wokovu wake upo mikononi mwako kama hutamhubiria Neno; atakufa na kwenda kuzimu. Damu yake itakuwa juu yako na nafsi zote ambazo huyu kijana angeziokoa kama angekuwa mkristo. Kila kitu unachokifanya katika ulimwengu wa kawaida unaakisi katika ulimwengu wa kiroho. Ukiishika roho ya kijana huyu, watu wengi wataokolewa kupitia yeye. Ukimwacha afe huu umati wa watu hawatatubu na wataenda kuzimu.” Malaika alinionyesha katika maono itakuaje kama kijana osca atakuwa mkristo. Osca alikuwa na Biblia mkononi na akiongea kuhusu Yesu. Umati mkubwa ulisikia ujumbe wake. Alikuwa mchungaji wa kanisa kubwa. Akili yangu ilielewa kwamba huyu kijana ni muhimu kwa kazi ya Mungu. Malaika akanionyesha huyu kijana duniani. Na wakati huo alikuwa kwenye hatari kubwa ya kuuawa. Mashetani walikusanyika kuvuna maisha yake kabla hajakombolewa. Mapepo walikuwa na hisi kubwa juu ya kazi ya Mungu katika haya maisha. Hatari ya mapepo kuikosa hiyo roho ilikuwa ni hatua yangu kumwendea huyu kijana. Nilimuuliza malaika kwa nini mtoto aliruhusiwa afe. Malaika akanionyesha maono ya wakati ujao. Mtoto wangu alikuwa katika maono na alikuwa na miaka 18. Imekuwa miaka mitatu baadae, alikufa mwenye miaka 15. Mtoto wangu katika maono alikua katika hali ya ubaridi katika imani na akaamua kuishi maisha yake. Aliikana njia ya Yesu na kujiingiza kwenye unywaji pombe na madawa ya kulevya. Alianza mahusiano na msichana aliyekutana naye kwenye dunia ya uraibu. Na kwa sababu ya wivu, alimilikiwa na pepo. Alimuua mchumba wake kwa kumchoma na kisu na aliamuka na ule mwili. Punde baadae, aliuliwa na kaka wa yule binti. Sikumtambua mtoto wangu, kwa sababu katika maono ya wakati ujao alikuwa mtu mwingine. Shetani alibadili muonekano wake. Malaika akasema, “kama angeishi miaka 3 baadae, angekuwa mtu ambaye angeleta maumivu mengi kwa wazazi wake. Na bado angeenda kuzimu. Mungu alimruhusu kufa wakati hali yake ya rohoni ikiwa nzuri. Wakati mzuri zaidi ambao alimtafakari Mungu kwa moyo wake wote, huu ulikuwa wakati wake mzuri zaidi katika maisha yake. Shetani alikuwa tayari amepanga kuiba maisha yake.”
Hapo nilielewa jinsi Mungu anavyofanya kazi. Wakati mwingine nilimtilia mashaka Mungu kwamba hakuwa sawa kuruhu tukio. Mungu anajua mambo yote na sisi hatujua kitu chochote. Akiruhusu kifo cha mpendwa, Mungu anajua anachokifanya. Mtoto wangu, kama angeishi miaka mitatu zaidi, angekuwa kuzimu. Na Mungu angempeleka tu mtoto wangu sehemu ya mateso.


BARAKA
Nilimuuliza malaika kwa sababu mshahara wangu ulikuwa mdogo. Nilitaka upandishwe na ustawi tele. Malaika akanijibu, “Michael, moyo wako haujaandaliwa kupokea mateka ya kidunia. Mali yoyote ya thamani itakuwa kizuizi kati yako na Yesu. Hii itachangia kugeuka kwako kutoka njia ya wokovu. Ni Baba gani angempa kitu ambacho kitamzuru mtoto wake? Ndivyo hivyo na Mungu wetu.” “kuna mambo ya Baraka ambayo yatakupelekea kufa kiroho. Baraka ambazo zitasababisha maisha yako ya kiroho kujiua na kutupwa kuzimu. Unaomba Baraka ya kifedha ambayo itakuua. Hizi Baraka kama utazipata sasa zitaua maisha yako ya kiroho. Moyo wako bado unatamani vitu vya ulimwengu huu, ambavyo vinafanya iwe ngumu kwako kupokea. Wakati ukiwa umejiandaa kiroho utapokea, Mungu anaujua moyo wako. Wakati shauku ya kumiliki mali itakapokufa ndani yako kiasi cha kufikia kutojali tena vitu vya ulimwengu, Mungu atakupa kila kitu unachotaka. Lakini wakati huo ukifika haitabadilisha kitu chochote kwako. Wakati vitu vya mwilini vikizaliwa kiroho, hakutakuwa na matendo maovu katika maisha yako.”
Naelewa alichokisema malaika. Sasa nafahamu kwa nini wakristo wengi hufanya kampeni nyingi za maombi hawajapokea bado Baraka zao. Na baada ya miaka mingi ndio wanapokea. Wengine hawawezi kuvumilia na kuondoka kwenye njia kwa sababu hiyo. Inapokuja kwenye mali inachukua mda. Kila kitu ambacho ni sehemu ya hii dunia ni hatari. Mungu hutoa Baraka na hatawanyima watoto wake. Lakini kila kitu kina mda wake. Siri ni jinsi ulivyo zaidi wa kiroho, ndivyo utakavyobarikiwa na mali zaidi. Kama tu moyo wako ukiwa umeshikiliwa na vitu vya ulimwengu huu, Baraka itacheleweshwa.


HASIRA
Malaika alinirudisha duniani. Maumivu ya moyo ambayo nilikuwa nayo ndani ya moyo wangu yaling’olewa na yule malaika. Malaika aliyang’oa maumivu moyoni mwangu. Mkono wake uliingia kifuani mwangu na kutoa tope jeusi kutoka ndani ya moyo wangu. Ukitunza hasira ndani ya moyo wako kwa sababu ya mtu aliyekufanya uteseke hautaokolewa. Mwombe Mungu na usahau; muombe akuponye moyo wako. Kulea hasira ndani ya moyo wako unatuhumu watu na kuwaongoza kwenda kuzimu. Katika mateso kuna watu wengi wenye moyo wa uchungu. Nilienda kuhubili injili kwa kijana aliyemuua mtoto wangu. Na pia nilimwambia kwamba kijana aliyemuua ni mtoto wangu. Yule kijana akajawa na wasiwasi na akadhani nitamsemea kwenye vyombo vya dola. Nilimtuliza kijana na kumwambia kwamba nimemsamehe kwa uharifu aliofanya. Kijana akalia kwa sababu hakutegemea ukarimu wangu wa upendo, ukilinganisha alimuua mtoto wangu. Kijana akaniomba msamaha. Aligeuka na kupiga goti, akimkabidhi Yesu maisha yake. Ukarimu wangu wa upendo ulikuwa na matokeo zaidi kuliko maneno 1,000.
Yule kijana akawa mfanyakazi katika kanisa langu. Ndani ya mwaka mmoja Mungu alimwinua huyu kijana na hakuwa kama alivyokuwa awali. Aliona aibu kwa maisha yake ya awali na alijutia kwa kusababisha maumivu ndani yangu kwamba nilikuwa mchungaji wake. Alinisaidia kazini na kujaribu kuziba pengo lililoachwa na mtoto wangu katika familia. Nilimwambia asijtoe sadaka kwa kutaka kurekebisha ambacho hakiwezi kurekebishika. Nilimwambie awe na amani na kuwa na hofu juu ya kazi ya Mungu. Aliniaga na akaenda nchi ya mbali kufanya kazi ya Mungu. Na hatujawahi kuonana tena. Ukweli mwingine uliotokea ulikuwa dhidi ya rafiki yangu mmishenari. Alisafiri katika amerika ya kilatini mpaka siku moja ndege ilipoanguka. Nilimuuliza Mungu kwamba kwa nini alimuuruhusu mmishenari afe. Yesu akanitokea, siku hiyo ilikuwa usiku nasali aliponitokea. Alisema “kila mtu kwenye ile ndege alienda kuzimu, lakini mtumishi wangu yupo hapa pamoja nami. Usiwe na wasiwasi juu yake, yupo sehemu nzuri kuliko ulipo wewe. Hofu juu ya roho zilipotea ambazo bado zinaishi.
Yesu akanionesha duara na ndani yake kulikuwa na watu wengi wakitembea. Hii duara ni sayari ya dunia na umati wa watu wanatembea ndani ya mji.
Bwana akasema, “mwanangu, hawa watu hawajui njia wanayotembelea, wanaonekana kama watoto waliopotea, yatima wasio na wazazi. Nawapenda wote walio uumbaji wangu. Tazama watu hawa kwa macho yangu na uhisi jinsi ninanyohisi juu yao.”
Yesu akanishika, nilianza kuwatazama wale watu kwa mtazamo wa upendo. Kilikuwa kitu cha ajabu kilichotoka ndani ya moyo wangu na kuchipuka kutoka katika nafsi yangu. Nilihisi upendo wa Yesu ndani yake kwa kila mtu katika dunia. Upendo wote ukikusanywa wa wazazi jinsi wanavyowapenda watoto wao bado hautazidi upendo wa Yesu. Hata kama utakusanya upendo wote duniani, bado utakuwa mdogo na hauwezi kulinganishwa na upendo wa Yesu.
Yesu alisema, “litunze kundi langu katika upendo na kulijenga katika adabu ya mazuri yako.”
Yesu akapotea, nina ujumbe mdogo kwa watu wa Mungu. Kanisa la Yesu, jaribu kuweka vitu katika matendo. Chukua siku kutoa sadaka kwa masikini na watu wasio na makazi. Chukua siku kusafisha nyumba ya mtu asiyemwamini bado. Chukua siku kutembelea wagonjwa hospitalini. Chukua siku kumshukuru Mungu katika maombi yako na utahisi msisimko mzuri.
Huu ni ushuhuda wa kushinda ambao Mungu amenipa.

Source:
http://www.theheavenandhell.net/ex-catholic-priest-testimony/

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NAO WANIABUDU BURE!

NIMEWAPELEKEA TAUNI KAMA YA MISRI (CORONA) LAKINI HAMKUNIRUDIA MIMI

JE! NAWEZA KUWA SAFI NAMI NINA MIZANI YA UDHALIMU!!