TOFAUTI KATI YA DHEHEBU NA KANISA

TOFAUTI KATI YA DHEHEBU NA KANISA

Nakusalimia katika jina la Bwana wetu Yesu kristo. Karibu kujifunza Maneno matakatifu ya Mungu.

Leo tutajifunza Hekima juu ya Dhehebu na Kanisa. Kabla hatujalijua Dhehebu bora tukajua Kanisa kwanza.
Tunasoma mathayo 16;
13 Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana kuwa ni nani?
Mathayo 16:13
14 Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.
Mathayo 16:14
15 Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?
Mathayo 16:15
16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.
Mathayo 16:16
17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
Mathayo 16:17
18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Mathayo 16:18
19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
Mathayo 16:19
Unaona katika mstari wa 17 kuwa Petro alipata kujua kuwa Huyo alikuwa Mwana wa Mungu aliye hai! Kwa hiyo asingeishia tu kusema Mwana wa Mungu lakini anaongeza kwa kusema aliye hai Kumbuka Yesu alikuwa hajasulubiwa bado!

Je ni kwa Damu na Nyama angejua Hilo?

Yesu akamwambia Heri wewe Simoni Bar-yona kwa kuwa Mwili na Damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
Kwa hiyo hapa kipo kitu cha ziada ambacho kilimpa Petro kujua yote haya pengine tofauti na wale wenzake kwa wakati huo. Yesu anasema Baba yake aliye mbinguni ndiye aliyemfanya Petro kujua(aliyempa UFUNUO). Kilicholeta utofauti hapa ni UFUNUO, wanafunzi wote walikuwa pale lakini wakiwa na mashaka pengine miyoni mwao kama kweli huyu ni Mwana wa Mungu kama Yeye mwenyewe anavyodai. Hawakuwa na hakika au uhakikisho dhahiri kuwa Yeye ni Mwana wa Mungu. Isitoshe Neno Mwana wa Mungu lilikuwa msamiati bado kwao kwa Sababu walijua kabisa Mungu hana Mwana.

Lakini Petro kwa Ule UFUNUO kutoka kwa Baba aliweza kujua Huyu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai

Sasa, Mstari wa 18 unasema;
18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Mathayo 16:18
Hapa kuna swali;
Huo Mwamba ni Petro ama Ule UFUNUO aliofunuliwa?

》Tukisema ule Mwamba ni Petro, Basi, Damu na Nyama zilimfanya Petro kujua Yule alikuwa kristo,Mwana wa Mungu aliye hai!
Kwa sababu Yesu aliusifu Mwamba, maana yake ni kwamba Petro hakutegemea upande wa pili Kumtambua Yesu. Bali ni Yeye mwenyewe kwa uweza ama umahiri wake alijua hilo(jitihada binafsi)

》Tukisema UFUNUO ALIOPEWA KUTOKA KWA BABA ndio ule Mwamba, Ina maana kuwa Petro si kwa damu na Nyama zilizomfunulia hilo. Bali ule Mwamba Ndio UFUNUO ambao bila huo hata Yeye mwenyewe Petro asingetamka kuwa Yesu Ndie Kristo Mwana wa Mungu aliye hai.
Angebaki kama wenzake akijipiga kwa wasiwasi mwingi juu Uhalali wa jina hilo la Mwana wa Mungu


Kwa hiyo Kanisa litajengwa juu ya Mwamba na sio Petro.
Kanisa litajengwa juu ya Ufunuo kutoka Juu kwa Baba. Ndio hapo anasema Wala milango ya Kuzimu haitalishinda- HAPA NDIPO PENYE HEKIMA Maana hapa ndipo Ukipakosea Utazalisha Madhehebu hata yasiyo na Idadi; kila Moja likidai lipo Sawa kuliko lingine na halitaki kuchangamana na hilo lingine.


Kwa hiyo Kanisa kama limejengwa juu ya Petro haliwezi kushindana na Milango ya kuzimu kamwe
Kanisa katika Biblia ni hekalu; Hekalu linaanzia kwenye mwili wako wewe.
Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
1 Wakorintho 6:19
Unaona hapo? lakini pia alisema mkikusanyika wawili watatu nipo katikati Yenu.
20Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.
Mathayo 18:20
Huo mwamba tunaouzungumzia mda wote unatoka kwa Yesu, Roho wa Yesu ndie Roho mtakatifu
Yesu alikuja kwa jina Baba yake; maana yake Baba yake anaitwa Yesu
Pia Roho alisema atakuja kwa jina lake; Maana yake Roho mtakatifu jina lake Yesu.
Ndio maana maandiko yanasema Siri ya Utawa ni kuu! maana watu wamemgawanya Mungu katika vipande Vitatu.Hilo ni Makosa na Mungu anasema siku za Mwisho Tutajua kuwa jina lake ni Moja na Yeye ni Mmoja. Zekaria 14:9 Kwa hiyo tunajua Kanisa Linajegwa juu UFUNUO tofauti na hapo ni Kumkana Roho mtakatifu na kumfukuza kanisani
Hii ya Petro kuwa Mwamba ndio iliyozaa MADHEHEBU

MADHEHEBU
Mgawanyiko ndio kulileta Madhehebu. Mfano wa madhehebu ni Wasabato, ANGLIKANA, LUTHERANI,MOROVIANI, MENONITE, madhehebu ya walokole kama TAG,EAGT, FULL GOSPEL,N.K

Je ni mpango wa Mungu?
Hapana!
Kwa upande mmoja ni mpango wa Mungu kwa sababu kila linalofanyika, liwe baya au zuri ni Mungu kaliruhusu; na ndio maana Biblia inasema Mema na Mabaya yatoka kwa Bwana. Lakini hilo kaliruhusu kwa sababu Mwanadamu alikataa Uongozi wa Roho (Ufunuo) akachagua Uongozi wa Mwanadamu. Wakaweka madaraja ya masomo ili uweze kuhudumu kanisani na Elimu ya mwanadamu ikawa kipimo cha ujazo wa Roho; Kitu ambacho ni makosa makubwa!

Sasa katika madhehebu haya, Nani aliye sahihi?
Hamna hata mmoja! Wote wamekataa mpango wa Mungu. Si msabato wala mlokole wala Mkatoliki n.k
Ndio maana UFUNUO sasa hivi haupo katika Kanisa bali Mtu mmoja!
Alisema Ufunuo 3:20.
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
Ufunuo wa Yohana 3:20
Mlango huo unaozungumziwa ni wa MTU binafsi sio wa Kanisa. Maana kanisa limemkataa Mpatanishi (Roho mtakatifu)

Madai ya Potofu ya Madhehebu;

WASABATO;
Wasabato na Jumamosi yao, kila wanachoongea lazima wakulete kwenye Sabato. Hata Unabii wa Danieli na Ufunuo(Sanamu ya Mnyama, na mpinga kristo kubadili majira) wanautafsiri kwa kuunganisha na Sabato tu. Ni kweli Sabato ya Iliazimishwa kama siku(siku ya Saba-Jumamosi) katika Agano la kale, Yaani TORATI
Nasema TORATI kwa sababu kabla ya Torati hakukuwa na Kushika Sabato.

Lakini kimsingi Agano letu lilianza kwa Baba wa Imani, yaani IBRAHIMU
Basi ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazao, kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo.
Wagalatia 3:16
Unaona hapo, agano letu la Kuishi kwa imani kutoka kwa Ibrahimu halikuwa kwa Wana wa Israeli kwa Sababu wao hawakwenda kwa Imani bali kwa Matendo ya Sheria.
IBRAHIMU si kwamba hakuwa na Sabato, Hapana!
Alikuwa Nayo ambayo ndio hii ya Rohoni. Yaani kuenenda katika Roho na Pumziko (Sabato) la Rohoni! Alelluyah!!
Sabato ya kwenye Torati na vitu vingine katika Torati si kwamba vililetwa kimakosa hapana!
Huko nyuma kwa Ibrahimu Sabato ilikuwa haijanenwa waziwazi na ndio Maana ikafunuliwa katika Torati na wakaishika katika hali ya Matendo ya Mwili.
Ili sisi tuliofikiliwa na MIISHO ya zamani tupate kuielewa na kuiadhimisha katika Roho kama Ibrahimu, Katika mzao wake wake wa YESU KRISTO.

TORATI Wapendwa ilikuwa INAFUNUO AGANO JIPYA linavyopaswa kuwa. Kwamba kule vitu walivyotenda Kimwili Huku tunatenda Kiroho!
Mungu ni ROHO, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika ROHO na kweli.
Yohana 4:24
Imekuaje basi watu wengine wanasema TUMEIACHA SABATO.
Hebu soma hapa;
Wakolosai 2:16 “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au SABATO; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.”
Soma pia;
Wagalatia 4:9 “Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena? Mnashika SIKU, NA MIEZI, NA NYAKATI NA MIAKA.”
Kutokulielewa Neno halikupi nafasi ya kuwa Sawa. Huu ndio Udhehebu kulazimisha Neno ilimradi tu liendane na dhehebu lako. Hata kama linajipinga.(UKISIMAMA NJE YA UDHEHEBU UTALIONA VIZURI; HALIJIPINGI).

Kwa hiyo wana wa KAHABA (KAHABA MKUU NI DHEHEBU KATOLIKI) ni madhehebu Yote ambayo yamekataa Uongozi wa Roho mtakatifu.
Yaani wameweka Karama zaidi ya zile za Biblia.
Soma waefeso 4:11
Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; Waefeso 4:11
Hakuna Baba mchungaji, Hakuna paroko, Hakuna padre, Papa, Mama kanisa, Mchungaji mkuu.
Katika madhehebu Cheo cha Roho mtakatifu kimechuliwa na Vyeo vya Kibinadamu na mwanadamu akijisifu kwa Theolojia anakataa Uongozi wa Ufunuo kutoka kwa Roho mtakatifu Madhehebu tanajitambulisha pia kwa KUBATIZA KWA JILA LA BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU tofauti na Biblia inavyobatiza Katika Matendo 2:38. 10:46-48. 19:5. ULE ULE MWAMBA wa mathayo 16, Uliwafunulia kuwa waliagizwa wakabatize kwa jina la Baba na la Bwana na La Roho mtakatifu lakini Wakijua Hilo sio JINA bali CHEO cha Mungu ambaye Jina lake ni YESU KRISTO. ndipo wakabatiza kwa jina la Yesu kristo. HUO NI UFUNUO;

THEOLOJIA IKASEMA; walibatiza kwa jina la Yesu ili KULITANGAZA ZAIDI JINA LA YESU MAANA WAYAHUDI WALIMKANA.
Kama inaleta maana kiasi lakini Elfu kumi bandia na Halisi tofauti yake sio Rangi au Muonekano. ukiichunguza zaidi ufaigundua Bandia. Ndio hiyo pia Tofauti yao.
Moja halina Uvuvio wa Roho mtakatifu na jingine Linao. Haleluyah!

Hayo ni makosa makubwa. Na makosa yenyewe yanaanza kwa kutojua kanisa nini halafu Wasabato kwa Kuegemea katika maandishi ya MKATOLIKI ambayo kweli yalioana na UNIKOLAI. Wanathibitisha kuwa ALAMA YA MNYAMA ni KUABUDU SIKU YA JUMAPILI.

Hii nadharia Ni POTOFU kwa Sababu;
1.Mpinga kristo atakuja kubadili majira na Nyakati katika MIAKA 7 ya mwisho.Wanasema huu wakati ndipo atatangaza rasmi SIKU YA JUMAPILI KUWA SIKU YA KUABUDU. ambako ndiko kuipokea sanamu ya Mnyama. Hivi kwa akili ya kawaida; Hiyo Sanamu itasimamishwa wakati huo kama Biblia ilivyosema. Mda wote huu tunaenda Jumapili kanisani ambayo ni Sanamu, Halafu isiwe SANAMU kwa sasa, mpaka tu ATANGAZE MPINGA KRISTO? Hiyo ni akili ndogo tu!

2.Halafu, Kanisa litanyakuliwa kabla ya Dhiki kuu; Je, Wanaobaki si wale wana wali wapumbavu? wasio na mafuta? mathayo 25.
Sasa huko kushika Sabato kukoje katika yale mateso ya Ufunuo 16?
wasio na Roho mtakatifu ndio watajongea katika DHIKI KUU ya wakati huo; Si msabato wala mrutheli, wala mlokole, wala mkatoliki na dhehebu lingine lolote. Maadamu hukuwa na Mafta(Roho mtakatifu) utaenda katika dhiki.
JAMANI NAWAAMBIA KWELI HILI JAMBO SI LA KIJISHIKIZA KATIKA DHEHEBU BALI NENO
Sanamu ya mnyama ni kweli itatangazwa na Mpinga kristo lakini ni AMRI JUU YA KUTII DINI MOJA DUNIANI KOTE AMBAYO ITAAMBATANA NA SERIKALI MOJA YA ULIMWENGU.
Watu watawekewa DIGITAL ID; wengine wanasema ID2020, mimi sina uhakika kama ndio Yenyewe ama la!

Tufanye hamwamini katika UNYAKUO(Lazima mkane kwanza hili andiko kuwa ni uongo MATHAYO 24:40-41).
Kama ni hivyo, Basi mathayo 25 haitakuwa na Maana, Maana tofauti kati ya kutwaliwa na siku ya mwisho ni KUTWALIWA kutatokea katika hali ya Amani kabisa (Watu wasemapo kuna Amani ndipo Bwana aja kama Mwivi) Siku ya mwisho HAKUTAKUWA NA AMANI; NI GIZA (AMOSI 5:18-20).
18 Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya Bwana; kwani kuitamani siku ya Bwana? Ni giza, wala si nuru. Amosi 5:18 19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma. Amosi 5:19 20 Je! Siku ya Bwana haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga. Amosi 5:20
Hii sio siku ya kuisubili hata kidogo na walio watakatifu Watanyakuliwa Kabla.

3.Wasabato husema MPINGA KRISTO-PAPA(NI KWELI NDIYE) ATABADILI MAJIRA NA NYAKATI NDIO KUSEMA KUTOKA KUABUDU JUMAMOSI HADI JUMAPILI.
Danieli 7:25

Ni kutokuelewa Maandiko ama kulazimisha Maandiko Yaendane na kile Unachotaka wewe.
Sisemi hivi kukuvuta kwenye dhehebu langu, hapana! Mimi sipo Kwenye Dhehebu lolote.
Nataka Utoke Udhehebu na Kuingia Katika Kanisa Halisi. Ukisoma
Luka 12:54-55. Luka 21:7-8, 18, 23-25, 29-31. utaona MAJIRA HUMAANISHA NINI SIO SIKU BALI MDA FULANI, ambao unaweza kuwa miaka, miezi ama siku kadhaa bali sio siku Moja

Soma;
Luka 21: 7 ‘’Wakamwuliza wakisema, Mwalimu, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini ishara ya kuwa mambo hayo ya karibu kutukia? 8 Akasema, Angalieni, msije mkadanganyika, kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye; tena, MAJIRA YAMEKARIBIA. Basi msiwafuate hao’’.
Katika mstari huo unaona neno MAJIRA lilivyotumika hapo, sio kipindi cha SIKU MOJA MAALUMU.
Luka 12:54 ‘’Akawaambia makutano pia, Kila mwonapo wingu likizuka pande za magharibi mara husema, Mvua inakuja; ikawa hivyo. 55 Na kila ivumapo kaskazi, husema, Kutakuwa na joto; na ndivyo ilivyo.Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa nchi na mbingu; imekuwaje, basi, kuwa hamjui kutambua MAJIRA haya?’’
kwa hiyo MAJIRA atakayobadili Mpinga kristo ni MAJIRA YA NEEMA YA YESU KWENDA KWENYE MAJIRA YA DHIKI KUU

WA-PROTESTANTI. Hapa ndipo tunapata Madhehebu Lukuki na Manabii wa Uongo! Injili hapa ni kama WAGANGA WA KIENYEJI; Ni udhindani wa madhehebu. Kila Mtu anataka kuwa zaidi ya Mwenzie Tena kwa Jina UTAJIRI
Wanaitambua SABATO KWAMBA IPO ROHONI- hilo ni sawa. hawashiki siku na wala hawajisumbukii katika kuishika Siku. Naamini Wanasali Jumapili si kwa Maana ya kushika siku ya Jumapili kama Sabato kwao; Kama ambavyo nami naamini.
Wengi hapa hawajui maandiko; hukimbilia madhehebu kwa Jina la Muujiza, Utajiri, mafanikio.
Hawa watu wengi wao Hubeba ASHERA zao na kwenda kwa Mungu kuhitaji BARAKA. Wameizima injili ya TOBA na kuleta tusiyojua imetoka wapi!
WANAAMINI ROHO MTAKATIFU NI KUNENA KWA LUDHA Na kunena kwa Lugha wanenavyo si kwa Uvuvio wa Roho mtakatifu, Bali MANENO YAO ambayo hata mnenaji mwenyewe HAJUI ANACHOKIONGEA! wala hakuna awezaye KUFASILI. maana ni AKILI ZA MTU WALA SI ROHO MTAKATIFU.
Ni makosa makubwa; Toka uvuvio wa mwaka 1906 ambao ulikuwa ni wa Roho mtakatifu; Leo wanaiga na hawajui mtu anawezaje Kunena Kweli kweli. Kazi ya Roho mtakatifu si Kukufanya Unene kwa Lugha, hiyo ni ishara na sio kwamba inatokea kwa kila Mtu.
Lakini pia Wengi humtafta Mungu kwa Moyo wa Utaftaji na Ujasiri katika Kuipeleka Injili.
lakini bado ni MTOTO WA KAHABA!

<>WAKATOLIKI<> Huyu ndie Chimbuko la Mgawanyiko wa Makanisa baada kuingiza UNIKOLAI yaani Upagani ndani ya Kanisa. Dhehebu hili lina vitu hutavikuta kwenye Biblia na lilijiwekea Msingi wa hizo sheria. Walioanisha Upagani na Maandiko.
》Waliunda Sehemu yao wakifa wanaenda iitwayo Pagatori (upagani wa zamani). Hakuna kitu kama hicho bali KUZIMU TU NDO UKIFA UNAENDA.Mti uangukapo ndipo Ulalapo; Kama ulikufa katika dhambi Kuzimu inakusubili.
Hamna nafasi ya pili
》Walianzisha Sala zao Kama Rozari! Sala za kuombea Wafu. HAZIPO KTK MAANDIKO NA NI DHAMBI KABISA.
》Wanaabudu watakatifu na kuwaomba wawaombee, Kwao jina la Yesu halina Nguvu kabisa bali MARIA mama yake na Yesu.
》Waliweka Mtu mkuu wa kuwaongoza badala ya Yesu, (PAPA) ambaye ndie Kiti cha MPINGA KRISTO
》Wamemweka badala ya Mwana wa Mungu.
》Papa ndio anawasamehe dhambi zao. (kufuru) Dhehebu hili ndio
MKUU (MAMA WA MAKAHABA)

1 Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi; Ufunuo wa Yohana 17:1 2 ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake. Ufunuo wa Yohana 17:2
Mwanamke katika Biblia Huwakilisha Kanisa. Ndio hata sisi huitwa Bibi harusi; Kanisa litakalo nyakuliwa (wakiwa hai) kwa maana Mume wetu ni Yesu na tumeposwa kwa Damu yake na mateso yake.
Mwanamke Kahaba maana Yake ni MZINZI Kanisa likishikamanishwa na UPAGANI(UNIKOLAI) ndivyo jinsi HUFANYA UZINZI MBELE ZA BWANA(MME WA KANISA).

Mara nyingi waumini wake hawasomi maandiko; wao hupelekwa na Viongozi wao. Kanisa ndio mwamzi wa kila kitu.

NAWAPA SHAURI; HAKUNA MWENYE MWILI ATASIMAMA NA KANISA LAKE SIKU YA HUKUMU
Mkatubu! NDUGU ZANGU KATIKA KRISTO MKATUBU! MWISHO UPO KARIBU MNO.

LAKINI KWA SABABU UNABII WA BIBLIA LAZIMA UTIMIE HAMTATUBU, MSIJE MKAOKOLEWA.
Katika kizazi hiki hatufi wote mpaka SIKU YA BWANA IJE(UNYAKUO UNAANZA)

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NAO WANIABUDU BURE!

NIMEWAPELEKEA TAUNI KAMA YA MISRI (CORONA) LAKINI HAMKUNIRUDIA MIMI

JE! NAWEZA KUWA SAFI NAMI NINA MIZANI YA UDHALIMU!!