UDHEHEBU; DHAMBI INAYOPOTEZA WATEULE WENGI.
Shalom Mwana wa Mungu; Karibu katika chakula cha uzima, Neno la Mungu likikaa ndani yako hutaona kiu kamwe!
Wapendwa katika Bwana, Tupo mwishoni kabisa katika Majira ya siku za Mwisho. Moja ya siku hizi ambazo tunaruka na kuzurura na Kuyawaza ya dunia Bwana atakuja kama umeme. Ni wakati pekee Bwana atakuja kama Mwizi yaani katika Unyakuo. Alisema tusemapo kuna Amani, Ndipo Uharibifu Uwajiapo 1wathesalonike 5:3
Mwisho wa Dunia Bwana hatakuja kama Mwizi; Hautakuwa wakati wa Amani; Kumbuka Mwisho utakuwa wakati wa Vita, Katika dhiki kuu, siku za giza nene kama ambavyo Nabii Amosi anasema
Amosi 5:18-20.
ndipo hapa;
Ukizingatia Tumetawaliwa na Udhehebu Mwingi kuliko Neno?
Je, Ni wasabato ndio wateule?
Au ni Wakatoliki?
Ama wapentekoste?
Waanglikana? Walutheri? Ama?
Neno la Bwana linasema;
Kuwa MTEULE ni jambo lingine kabisa, Yaani katika waitwao Ndimo wateule hutoka.
Kwa hiyo siyo wote waitwao ni wateule, sio wote wanaosema wakristo wataingia katika ufalme wa Mbinguni.
Sasa hawa wateule si wapentekoste ama wasabato ama waromani ama waanglicana ama walutheri ama chochote kile kiitwacho dhehebu bali WALE WAYATENDAYO MAPENZI YA BWANA. Kumbe wanaweza kutoka kwa wasabato ama wapentekoste ama wakatoliki ama waanglikana ama wowote wa udhehebu lakini si wote katika hilo dhehebu!
Maana yangu ni nini!
Dhehebu sio suluhisho, Na njia ya Kweli tumeiacha kwa kufuata tafsiri za Mwanadamu. Ni kwamba; Theolojia ya Mwanadamu ndio iliyotugawanya; tukaacha kumtegemea Roho mtakatifu ili alijenge kanisa kama alivyosema katika Mathayo 16;15-19
Badala yake tukaingiza mawazo ya Mwanadamu kulijenga kanisa, Hivyo tukamfukuza kanisani. Na baada ya hapo Shetani akapiga vita akishinda.
DHANA YA UDHEHEBU;
Kimsingi kila mwenye dhehebu lake hujaribu kutoa maada ama kuhubili si kuwafanya watu wawe kama kristo (Wakristo) lakini anataka waje katika dhehebu lake.
》Msabato atakuhimiza uishike sabato, ule vyakula fulani
Ila kama unaye roho mtakatifu utashangaa wao maandiko kama Wakolosai 2:16, Waebrani 13:9, wagalatia 4:9-10. Ama warumi 7 kuhusu kutoka kwenye torati na kuja kwenye Neema wanakutafsirije!
Ila kwa sababu wanalo dhehebu wanalazimisha sasa kila andiko liegemee upande wao bila kujali linajipinga kwenye maandiko!
Hakuna mtu mjinga duniani hapa, aingie kanisani na Sanamu tuseme labda ya Mwanamalundi kanisani halafu wakristo wakubali, hapana! Shetani anakuja na Uongo uliokaribu na Ukweli.
Ndio maana ukimwambia mkatoliki juu ya ibada zake za sanamu anakataa katakata kwamba haiabudu ile Sanamu. Na anakusomea maandiko kabisa, Tena yale yale unayoyafahsmu wewe; tofauti ni fasiri.
Sasa biblia inasema;
》Waprotestanti nao jambo lile hamna Roho mtakatifu wanalazimisha kuwa wanae. Wanajitungia ibada kila kukicha tena wakitumia maandiko haya haya. Wanachuma kile kile alichochuma Mkatoliki, Msabato. Wanafuata mle mle, Fasiri ya Seminary
halafu anasema Mungu kasema Nae! Imani yake inamtuma kuwa Nabii tu sio utakatifu.
Angalia namna ya ibada zilivyogeuzwa na kuwa kitu cha hovyo. Biblia inasema Mwili wako ni hekalu la Mungu, Bado Hilo ni la kijinga mbele ya wahubili hawa,
Angalia mkatoriki anavyojiharibu mwili wake, njoo kwa mlokole wa leo, Angalia msabato wa leo, WOTE NI WAMOJA KATIKA KILA JAMBO BAYA! hii ni kuonesha wanaushirika mahali fulani ila Hawajui ni wapi. Wote ni wa udhehebu!
Dhehebu lako hata kama litakuwa Tajiri kiasi gani, Maarufu kiasi gani, zuri kiasi gani; Halina uhusiano wowote na WOKOVU. Wokovu ni kumsadiki Yesu kristo, Kumpenda kwa kuzitenda sheria zake. Kubatiza kwa Maji na Kwa Roho, Kumtegemea Roho mtakatifu katika Fasili yote ya maandiko. Na Mungu hujifasiria Maandiko hivyo bila Roho mtakatifu ni kazi bure.
Nakumbuka Ushuhuda wa Mtu mmoja anaitwa Miguel vasguz, Katika maono aliambiwa asilimia ya Wateule katika Makanisa; Asilimia kubwa ilitoka kwa Makanisa madogo madogo yasiyojulikana; Na yale makanisa makubwa walitoka asilimia ndogo zaidi.
Kumaanisha Jinsi kanisa linavyozidi kukua, Ndivyo wahubili huliacha Neno ili kukidhi matakwa ya Watoaji ambao mara nyingi ni matajiri, presha ya uchuvu ndio inavamia. Badala injili ya toba, watahubili isitaja toba ili wasiwafukuze hao Watoaji.
NINI CHA KUFANYA!
Badala ya kunyosheana vidole nani ana makosa na wapi kakosea. Turudi kwanza tujue kama Je, Tunatazama kibanzi katika jicho la wengine na kuacha Boriti katika jicho letu??
Maana kama sisi sote ni wakristo iweje hatuna upendo sisi kwa sisi?
Ni kweli hatupaswi kushirikiana na mwenye dhambi. Lakini ni dhehebu lipi lina dhambi na lipi halina??
Tumekuwa kama vipofu, kila mtu anamcheka mwenziwe halafu mbaya zaidi ni Elimu ile ile Ya Mwanadamu(theolojia) ndio inatufanya tusisogeleane. Watu wanazidi kupotea kwa sababu ya Kuiga na kutoelewa Maandiko.
Ikiwa utasimama katika maandiko bila kujali dhehebu lako linaamini nini, utajua kweli ya Mungu, Na utamwona kila mwenye kujigamba juu dhehebu lake kuwa Hajui alisemalo.
Paulo anasema;
Ili mradi tu iendane na theologia yao.
Ili mradi tu wajipe mamlaka kuwa wao ndio wako sahihi sana.
Sasa, Paulo alisema hata ni malaika atoke mbinguni aje ahubiri hapa. Kama hata hubili injili sawa na tunayohubili na alaaniwe!!!!!
Leo akitokea muona maono; anaabudiwa na wanadamu. Na maandiko wanayalazimisha sasa yaendane na fikra za muonaji na sio Muonaji aendane na Maandiko.
Wapendwa sisemi kumponda mtu, Hapana! Nasema kweli ya Mungu kuwa iangalieni njia Yenu. Kutokumfahamu Roho mtakatifu na utendaji kazi wake ndio Kunafanya huu uharibifu.
Kama kweli sote tunataka kuuona ufalme wa mbinguni basi tuwe tayari kupokea injili ya Toba. Na kutoka katika udhebuni maana Bwana amesema tokeni huko watu wangu.
Kuanzia kwa Mama wa makaha(kanisa katoliki) kuja kwa Binti zake ambao ndio hao Wasabato, waprotestanti(Wapentekoste), Warutheli, anglicana na wengine wote
Bibi harusi wa kristo sio Dhehebu la watu fulani, Hapana! Ni wale waliobatizwa katika Roho mtakatifu. Na mtu wa namna hii huwezi kumkuta anajisifia dhehebu.
Basi kama wewe ni unahitaji kumjua Yesu katika kweli yote, Unachopaswa kufanya ni kugeuka kutoka katika njia mbaya pamoja na udhehebu. Simama kwa kutaka kujua kweli na si kutaka kujua dhehebu lipi lipo sahihi; HAUTALIPATA. Maana dhehebu halitatubu mpaka mwisho Bali Bwana anasema;1
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; MTUakiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
Ufunuo wa Yohana 3:20
Kwa nini hajasema kanisa likitubu, hapo nyuma utaona makanisa saba yanaambiwa yatubu. Lakini hapa anamwambia Mtu akisikia sauti yake na si kanisa tena.
Maana kanisa(dhehebu) katika kitabu hiki linaenda moja kwa moja mpaka kwenye dhiki.
Kahaba mkuu na binti zake hawatatubu, ndivyo maandiko yanavyosema. Kwa hiyo usiangalid hilo dhehebu lako. Bali ni wewe ndie waweza kutubu!
Bwana Yupo hapi ulipo akibisha umfungulie mlango. Kufungua mlango ni kutubu dhambi zako
Kwa maana ya kugeuka na kuacha dhambi. Sio kutubu kwa Maneno bali kwa vitendo; halafu ndio Maneno yanafuata. Na wali si kwa kuomba tu bali Kuchukua hatua ya kuacha dhambi. Hapo ndio Roho mtakatifu ataingia ndani yako na kukuficha katika dhambi zote, naye ndiye Muhuri wako hata milele.
Mtu aliye na Roho mtakatifu
•Huwezi kumkuta,ananyoa denge, kiduku.
•Huwezi kumkuta anapaka rangi nywele
•Huwezi kumkuta anavaa wigi
•Huwezi kumkuta ni mwanamke anavaa suruali.
•Huwezi kumkuta anaweka kucha bandia.
•Huwezi kumkuta anavaa vimini.
•huwezi kumkuta anavaa modo na sketi za kubana kwa mwanamke.
•Huwezi kumkuta anatazama Video za ngono.
•Huwezi kumkuta anatumia mda mwingi kuchati na kuangalia Movie kuliko kutafta uso wa Bwana.
•Huwezi kumkuta Ni mseng'enyaji.
•Huwezi kumkuta ni mwasherati.
•Huwezi kumkuta ni Mzinzi.
•Huwezi kumkuta anasema Unabii usiotoka kwa Bwana.
•Huwezi kumkuta anahubili mafanikio tu kana kwamba Mtu ataishi kwa mkate tu.
•Huwezi kumkuta anahangaika na Siasa.
•Huwezi kumkuta anatii ya dhehebu kuliko ya Mungu.
•Huwezi kimkuta ni mgomvi ama mwenye hasira.
•Huwezi kumkuta mchawi, mganga wa kienyeji.
•Huwezi kumkuta anabashiri michezo ya Bahati na simu, kama kubeti.
•Huwezi kumkuta anatukana kisa dhehebu lake limesemwa vibaya.
Yapo mengi mno yasiyo ya mtu aliye na Roho wa Yesu.
Mambo haya ukiyaangalia kila mtu anajua ni makosa na Hakika HAYAMWONGEZEI mtu chochote lakini cha ajabu ni kwamba Huku akijua Ni dhambi bado anatamani kuyafanya.
Na ni haya haya yatakufanya uingie katika Dhiki kuu. Na hata kuukosa kabisa ufalme wa mbinguni hasa nyie MLIOITWA
Amri iliyo kuu ni KUMPENDA MUNGU KWA MOYO WETU WOTE NA KWA AKILI ZETU ZOTE mathayo 22:36-37. Jiulize ukiyafanya hayo kukowapi kumpenda Yeye kwa Moyo wote. Bali Umempenda Nusu na kwa akili kidogo
Nawasalimu Nyote! Upendo wa Yesu uzidi kuwa Nanyi.
Wapendwa katika Bwana, Tupo mwishoni kabisa katika Majira ya siku za Mwisho. Moja ya siku hizi ambazo tunaruka na kuzurura na Kuyawaza ya dunia Bwana atakuja kama umeme. Ni wakati pekee Bwana atakuja kama Mwizi yaani katika Unyakuo. Alisema tusemapo kuna Amani, Ndipo Uharibifu Uwajiapo 1wathesalonike 5:3
Mwisho wa Dunia Bwana hatakuja kama Mwizi; Hautakuwa wakati wa Amani; Kumbuka Mwisho utakuwa wakati wa Vita, Katika dhiki kuu, siku za giza nene kama ambavyo Nabii Amosi anasema
Amosi 5:18-20.
18 Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya Bwana; kwani kuitamani siku ya Bwana? Ni giza, wala si nuru.Bila shaka Unaona hapo kwamba hamna amani hata kidogo. Kwa hiyo mpaka wakati huo WATEULE watakuwa wamenyakuliwa,
Amosi 5:18
19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma.
Amosi 5:19
20 Je! Siku ya Bwana haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga.
Amosi 5:20
ndipo hapa;
Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;Lakini sasa WATEULE hao ni wapi?
Mathayo 24:40
wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.
Mathayo 24:41
Ukizingatia Tumetawaliwa na Udhehebu Mwingi kuliko Neno?
Je, Ni wasabato ndio wateule?
Au ni Wakatoliki?
Ama wapentekoste?
Waanglikana? Walutheri? Ama?
Neno la Bwana linasema;
Kwa maana waitwao ni wengi, bali WATEULE ni wachache.kama wewe umeisikia injili na kuingia kanisani ujue UMEITWA!
Mathayo 22:14
Kuwa MTEULE ni jambo lingine kabisa, Yaani katika waitwao Ndimo wateule hutoka.
Kwa hiyo siyo wote waitwao ni wateule, sio wote wanaosema wakristo wataingia katika ufalme wa Mbinguni.
Sasa hawa wateule si wapentekoste ama wasabato ama waromani ama waanglicana ama walutheri ama chochote kile kiitwacho dhehebu bali WALE WAYATENDAYO MAPENZI YA BWANA. Kumbe wanaweza kutoka kwa wasabato ama wapentekoste ama wakatoliki ama waanglikana ama wowote wa udhehebu lakini si wote katika hilo dhehebu!
Maana yangu ni nini!
Dhehebu sio suluhisho, Na njia ya Kweli tumeiacha kwa kufuata tafsiri za Mwanadamu. Ni kwamba; Theolojia ya Mwanadamu ndio iliyotugawanya; tukaacha kumtegemea Roho mtakatifu ili alijenge kanisa kama alivyosema katika Mathayo 16;15-19
Badala yake tukaingiza mawazo ya Mwanadamu kulijenga kanisa, Hivyo tukamfukuza kanisani. Na baada ya hapo Shetani akapiga vita akishinda.
DHANA YA UDHEHEBU;
Kimsingi kila mwenye dhehebu lake hujaribu kutoa maada ama kuhubili si kuwafanya watu wawe kama kristo (Wakristo) lakini anataka waje katika dhehebu lake.
》Msabato atakuhimiza uishike sabato, ule vyakula fulani
Ila kama unaye roho mtakatifu utashangaa wao maandiko kama Wakolosai 2:16, Waebrani 13:9, wagalatia 4:9-10. Ama warumi 7 kuhusu kutoka kwenye torati na kuja kwenye Neema wanakutafsirije!
Ila kwa sababu wanalo dhehebu wanalazimisha sasa kila andiko liegemee upande wao bila kujali linajipinga kwenye maandiko!
Hakuna mtu mjinga duniani hapa, aingie kanisani na Sanamu tuseme labda ya Mwanamalundi kanisani halafu wakristo wakubali, hapana! Shetani anakuja na Uongo uliokaribu na Ukweli.
Ndio maana ukimwambia mkatoliki juu ya ibada zake za sanamu anakataa katakata kwamba haiabudu ile Sanamu. Na anakusomea maandiko kabisa, Tena yale yale unayoyafahsmu wewe; tofauti ni fasiri.
Sasa biblia inasema;
6 Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana ANDIKO HUUA, bali ROHO huhuisha.Unaona, kumbe pasipo Roho mtakatifu kila mtu atachuma jinsi atakavyo, Na andiko linamfisha Huyo mtu si kimwili bali Kiroho! Ndipo analeta tafsiri aijue mwenyewe imetoka wapi, si kwa roho bali kwa Mwili na Nyama (Akili za Mwanadamu-Seminary).
2 Wakorintho 3:6
》Waprotestanti nao jambo lile hamna Roho mtakatifu wanalazimisha kuwa wanae. Wanajitungia ibada kila kukicha tena wakitumia maandiko haya haya. Wanachuma kile kile alichochuma Mkatoliki, Msabato. Wanafuata mle mle, Fasiri ya Seminary
halafu anasema Mungu kasema Nae! Imani yake inamtuma kuwa Nabii tu sio utakatifu.
Angalia namna ya ibada zilivyogeuzwa na kuwa kitu cha hovyo. Biblia inasema Mwili wako ni hekalu la Mungu, Bado Hilo ni la kijinga mbele ya wahubili hawa,
Angalia mkatoriki anavyojiharibu mwili wake, njoo kwa mlokole wa leo, Angalia msabato wa leo, WOTE NI WAMOJA KATIKA KILA JAMBO BAYA! hii ni kuonesha wanaushirika mahali fulani ila Hawajui ni wapi. Wote ni wa udhehebu!
Dhehebu lako hata kama litakuwa Tajiri kiasi gani, Maarufu kiasi gani, zuri kiasi gani; Halina uhusiano wowote na WOKOVU. Wokovu ni kumsadiki Yesu kristo, Kumpenda kwa kuzitenda sheria zake. Kubatiza kwa Maji na Kwa Roho, Kumtegemea Roho mtakatifu katika Fasili yote ya maandiko. Na Mungu hujifasiria Maandiko hivyo bila Roho mtakatifu ni kazi bure.
Nakumbuka Ushuhuda wa Mtu mmoja anaitwa Miguel vasguz, Katika maono aliambiwa asilimia ya Wateule katika Makanisa; Asilimia kubwa ilitoka kwa Makanisa madogo madogo yasiyojulikana; Na yale makanisa makubwa walitoka asilimia ndogo zaidi.
Kumaanisha Jinsi kanisa linavyozidi kukua, Ndivyo wahubili huliacha Neno ili kukidhi matakwa ya Watoaji ambao mara nyingi ni matajiri, presha ya uchuvu ndio inavamia. Badala injili ya toba, watahubili isitaja toba ili wasiwafukuze hao Watoaji.
NINI CHA KUFANYA!
Badala ya kunyosheana vidole nani ana makosa na wapi kakosea. Turudi kwanza tujue kama Je, Tunatazama kibanzi katika jicho la wengine na kuacha Boriti katika jicho letu??
Maana kama sisi sote ni wakristo iweje hatuna upendo sisi kwa sisi?
Ni kweli hatupaswi kushirikiana na mwenye dhambi. Lakini ni dhehebu lipi lina dhambi na lipi halina??
Tumekuwa kama vipofu, kila mtu anamcheka mwenziwe halafu mbaya zaidi ni Elimu ile ile Ya Mwanadamu(theolojia) ndio inatufanya tusisogeleane. Watu wanazidi kupotea kwa sababu ya Kuiga na kutoelewa Maandiko.
Ikiwa utasimama katika maandiko bila kujali dhehebu lako linaamini nini, utajua kweli ya Mungu, Na utamwona kila mwenye kujigamba juu dhehebu lake kuwa Hajui alisemalo.
Paulo anasema;
Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.Kama Paulo asingesema haya Maneno, bila shaka kuna watu wangemkana. Wengine wangesema huyu bwana alikosea ilitakiwa iwe hivi na sio alivyosema.
Wagalatia 1:8
Ili mradi tu iendane na theologia yao.
Ili mradi tu wajipe mamlaka kuwa wao ndio wako sahihi sana.
Sasa, Paulo alisema hata ni malaika atoke mbinguni aje ahubiri hapa. Kama hata hubili injili sawa na tunayohubili na alaaniwe!!!!!
Leo akitokea muona maono; anaabudiwa na wanadamu. Na maandiko wanayalazimisha sasa yaendane na fikra za muonaji na sio Muonaji aendane na Maandiko.
Wapendwa sisemi kumponda mtu, Hapana! Nasema kweli ya Mungu kuwa iangalieni njia Yenu. Kutokumfahamu Roho mtakatifu na utendaji kazi wake ndio Kunafanya huu uharibifu.
Kama kweli sote tunataka kuuona ufalme wa mbinguni basi tuwe tayari kupokea injili ya Toba. Na kutoka katika udhebuni maana Bwana amesema tokeni huko watu wangu.
Kuanzia kwa Mama wa makaha(kanisa katoliki) kuja kwa Binti zake ambao ndio hao Wasabato, waprotestanti(Wapentekoste), Warutheli, anglicana na wengine wote
Bibi harusi wa kristo sio Dhehebu la watu fulani, Hapana! Ni wale waliobatizwa katika Roho mtakatifu. Na mtu wa namna hii huwezi kumkuta anajisifia dhehebu.
Basi kama wewe ni unahitaji kumjua Yesu katika kweli yote, Unachopaswa kufanya ni kugeuka kutoka katika njia mbaya pamoja na udhehebu. Simama kwa kutaka kujua kweli na si kutaka kujua dhehebu lipi lipo sahihi; HAUTALIPATA. Maana dhehebu halitatubu mpaka mwisho Bali Bwana anasema;1
Ufunuo wa Yohana 3:20
Kwa nini hajasema kanisa likitubu, hapo nyuma utaona makanisa saba yanaambiwa yatubu. Lakini hapa anamwambia Mtu akisikia sauti yake na si kanisa tena.
Maana kanisa(dhehebu) katika kitabu hiki linaenda moja kwa moja mpaka kwenye dhiki.
Kahaba mkuu na binti zake hawatatubu, ndivyo maandiko yanavyosema. Kwa hiyo usiangalid hilo dhehebu lako. Bali ni wewe ndie waweza kutubu!
Bwana Yupo hapi ulipo akibisha umfungulie mlango. Kufungua mlango ni kutubu dhambi zako
Kwa maana ya kugeuka na kuacha dhambi. Sio kutubu kwa Maneno bali kwa vitendo; halafu ndio Maneno yanafuata. Na wali si kwa kuomba tu bali Kuchukua hatua ya kuacha dhambi. Hapo ndio Roho mtakatifu ataingia ndani yako na kukuficha katika dhambi zote, naye ndiye Muhuri wako hata milele.
Mtu aliye na Roho mtakatifu
•Huwezi kumkuta,ananyoa denge, kiduku.
•Huwezi kumkuta anapaka rangi nywele
•Huwezi kumkuta anavaa wigi
•Huwezi kumkuta ni mwanamke anavaa suruali.
•Huwezi kumkuta anaweka kucha bandia.
•Huwezi kumkuta anavaa vimini.
•huwezi kumkuta anavaa modo na sketi za kubana kwa mwanamke.
•Huwezi kumkuta anatazama Video za ngono.
•Huwezi kumkuta anatumia mda mwingi kuchati na kuangalia Movie kuliko kutafta uso wa Bwana.
•Huwezi kumkuta Ni mseng'enyaji.
•Huwezi kumkuta ni mwasherati.
•Huwezi kumkuta ni Mzinzi.
•Huwezi kumkuta anasema Unabii usiotoka kwa Bwana.
•Huwezi kumkuta anahubili mafanikio tu kana kwamba Mtu ataishi kwa mkate tu.
•Huwezi kumkuta anahangaika na Siasa.
•Huwezi kumkuta anatii ya dhehebu kuliko ya Mungu.
•Huwezi kimkuta ni mgomvi ama mwenye hasira.
•Huwezi kumkuta mchawi, mganga wa kienyeji.
•Huwezi kumkuta anabashiri michezo ya Bahati na simu, kama kubeti.
•Huwezi kumkuta anatukana kisa dhehebu lake limesemwa vibaya.
Yapo mengi mno yasiyo ya mtu aliye na Roho wa Yesu.
Mambo haya ukiyaangalia kila mtu anajua ni makosa na Hakika HAYAMWONGEZEI mtu chochote lakini cha ajabu ni kwamba Huku akijua Ni dhambi bado anatamani kuyafanya.
Na ni haya haya yatakufanya uingie katika Dhiki kuu. Na hata kuukosa kabisa ufalme wa mbinguni hasa nyie MLIOITWA
Amri iliyo kuu ni KUMPENDA MUNGU KWA MOYO WETU WOTE NA KWA AKILI ZETU ZOTE mathayo 22:36-37. Jiulize ukiyafanya hayo kukowapi kumpenda Yeye kwa Moyo wote. Bali Umempenda Nusu na kwa akili kidogo
Nawasalimu Nyote! Upendo wa Yesu uzidi kuwa Nanyi.

Maoni
Chapisha Maoni
Tafadhali, share kwa wengine ili kuisambaza injili kwa watu wote na Mungu wa mbinguni atakubariki.
Unaweza kutumia namba hii 0755251999 kuwasiliana kwa njia ya whatsapp